CCM yajipanga kwa ushindi wa mezani

Ngwananzengo

JF-Expert Member
Jul 28, 2012
1,911
1,312
Zoezi la Uandikishaji wapiga kura au ubooreshaji wa daftari la wapiga kura limegeuzwa kuwa mkakati wa ushindi wa mezani kwa chama tawala. Nikiwa wilaya ya Manyoni ktk mji mdogo wa Mitundu nimeyashuhudia haya. Kwanza Uandikishaji ulianza kimya kimya Bila taarifa yoyote ya msingi kwa umma. Shukrani kwa gari la matangazo la CHADEMA lililokuja jumamosi jioni na kuzunguka likihamasisha watu kujiandikisha. Pili ni Tatizo la mashine, siku ya jumamosi Uandikishaji ulianza kwa mashine moja tu na ya pili ilianza kazi saa 11 jioni, saa 1kabla ya kusitisha Uandikishaji. Tatu ni utaratibu unaotumika, mtu akifika kituoni anajiandikisha na kusubiri kuitwa jina. Yule anaeita majina amekuwa akiita majina kwa mlengo wa kiitikadi zaidi na si nani kawahi. Nne ni mkakati ulioandaliwa kuwaandikisha Muda wa usiku wapenzi, mashabiki na wanachama wa Chama tawala. Kituo hiki kitaandikisha watu kwa siku 7 na mji mdogo wa Mitundu una watu zaidi ya elfu nane wenye sifa za kuandikishwa. Sijui ni kwa muujiza upi wataweza kuandikisha watu wote hawa kwa mashine 2 tu zilizopo hadi sasa. Binafsi naona huu ni mkakati wa ushindi wa mezani kwa CCM. UKAWA mna wajibu wa kulitupia jicho suala hili na kulitafutia ufumbuzi wenye tija.
 
inachofanya ccm ni kuhonga migodi,gesi na wanyama kwa mataifa yenye nguvu ili wasiondolewe madarakani na mataifa hayo!!!
 
Kama ni kweli basi viongozi wa chadema tarafa ya ITIGI wanatakiwa kwenda kuweka kambi mitundu na mgandu kwa ajili ya kuhasisha wapiga kura.
 
Gari la CHADEMA lilikuja Jumamosi jioni Mitundu kufanya PA na kwa kiasi kikubwa limesaidia sana uhamasishaji. Bahati mbaya nimepata safari ya kurudi Kanda ya Ziwa ningeendelea kuleta yanayojiri na faulo zinazofanyika
 
  • Thanks
Reactions: Gor
Zoezi la Uandikishaji wapiga kura au ubooreshaji wa daftari la wapiga kura limegeuzwa kuwa mkakati wa ushindi wa mezani kwa chama tawala. Nikiwa wilaya ya Manyoni ktk mji mdogo wa Mitundu nimeyashuhudia haya. Kwanza Uandikishaji ulianza kimya kimya Bila taarifa yoyote ya msingi kwa umma. Shukrani kwa gari la matangazo la CHADEMA lililokuja jumamosi jioni na kuzunguka likihamasisha watu kujiandikisha. Pili ni Tatizo la mashine, siku ya jumamosi Uandikishaji ulianza kwa mashine moja tu na ya pili ilianza kazi saa 11 jioni, saa 1kabla ya kusitisha Uandikishaji. Tatu ni utaratibu unaotumika, mtu akifika kituoni anajiandikisha na kusubiri kuitwa jina. Yule anaeita majina amekuwa akiita majina kwa mlengo wa kiitikadi zaidi na si nani kawahi. Nne ni mkakati ulioandaliwa kuwaandikisha Muda wa usiku wapenzi, mashabiki na wanachama wa Chama tawala. Kituo hiki kitaandikisha watu kwa siku 7 na mji mdogo wa Mitundu una watu zaidi ya elfu nane wenye sifa za kuandikishwa. Sijui ni kwa muujiza upi wataweza kuandikisha watu wote hawa kwa mashine 2 tu zilizopo hadi sasa. Binafsi naona huu ni mkakati wa ushindi wa mezani kwa CCM. UKAWA mna wajibu wa kulitupia jicho suala hili na kulitafutia ufumbuzi wenye tija.

Aagh! Chadema hii sasa sifaaa! Kila kitu nyie ni kulalamika tu na kuandaa mazingira ya vurugu, tumewachoka!! Adhabu yenu sanduku la kura oktoba.
 
Bora CHADEMA "tumechokwa" na CCM, je, nyie mliochokwa na wananchi. Maana si kwenye nyumba za ibada wala za burudani, si kwa wasomi wala wasiosoma, si kwa vijana wala kina mama. Kama mnajiamini kwa nini hamfanyia Uandikishaji ktk namna ambayo utaleta tija na ufanisi.
 
sidhani kama hii habari yako ni reliable. hebu jifunzeni basi kuandika kitu kama kilivyo bila kuleta ushabiki. mara useme wanaitwa watu kwa itikadi zao! porojo hizi ni ngumu kumeza. nullified.

Zoezi la Uandikishaji wapiga kura au ubooreshaji wa daftari la wapiga kura limegeuzwa kuwa mkakati wa ushindi wa mezani kwa chama tawala. Nikiwa wilaya ya Manyoni ktk mji mdogo wa Mitundu nimeyashuhudia haya. Kwanza Uandikishaji ulianza kimya kimya Bila taarifa yoyote ya msingi kwa umma. Shukrani kwa gari la matangazo la CHADEMA lililokuja jumamosi jioni na kuzunguka likihamasisha watu kujiandikisha. Pili ni Tatizo la mashine, siku ya jumamosi Uandikishaji ulianza kwa mashine moja tu na ya pili ilianza kazi saa 11 jioni, saa 1kabla ya kusitisha Uandikishaji. Tatu ni utaratibu unaotumika, mtu akifika kituoni anajiandikisha na kusubiri kuitwa jina. Yule anaeita majina amekuwa akiita majina kwa mlengo wa kiitikadi zaidi na si nani kawahi. Nne ni mkakati ulioandaliwa kuwaandikisha Muda wa usiku wapenzi, mashabiki na wanachama wa Chama tawala. Kituo hiki kitaandikisha watu kwa siku 7 na mji mdogo wa Mitundu una watu zaidi ya elfu nane wenye sifa za kuandikishwa. Sijui ni kwa muujiza upi wataweza kuandikisha watu wote hawa kwa mashine 2 tu zilizopo hadi sasa. Binafsi naona huu ni mkakati wa ushindi wa mezani kwa CCM. UKAWA mna wajibu wa kulitupia jicho suala hili na kulitafutia ufumbuzi wenye tija.
 
chadema kwenye suala hili la uandikishaji mkiwategemea sana NEC hii ya ccm mmekwisha. fuatilieni sana hujuma hizi zinazofanywa na tume hii ya kiccm.
 
sidhani kama hii habari yako ni reliable. hebu jifunzeni basi kuandika kitu kama kilivyo bila kuleta ushabiki. mara useme wanaitwa watu kwa itikadi zao! porojo hizi ni ngumu kumeza. nullified.
Mimi nimetaja kituo cha Uandikishaji, siku husika na utaratibu unaotumika. Sasa hapo ushabiki wangu upo wapi. Ingekuwa vyema ukajipa Muda wa kufuatiria taarifa kwenye vyanzo vingine ili kufanya ulinganifu, vingenevyo unachosema wewe ndio sio"reliable".
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom