CCM yaishukia CHADEMA suala la TUHUMA za Rushwa kwa wabunge

the horse

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
652
441
--Yadai orodha yake inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
--yadaiwa kutaka kuwaokoa wabunge wa Chadema katika sakata hilo.
--Yasema suala la tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe kuwa la kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

"Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;

"Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".

Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.

"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.

"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.

Nape alisema CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.

"Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.

Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.
 
wanaongea nini hawa mafisadi wala rushwa na wasioweza kukemea rushwa??!
tuangalie historia............
karamagi
msabaha
balali
ngeleja
mkulo
nyoni
......
......
sijui wanakataa nini sasa?
 
jamani,kwani kumtaja mwizi mpaka ubembelezwe.spika alipaswa ataje mapema hayo majina.sasa chadema wao wametaja,na nyie si muwawataje.wizi na siasa haviwezi kwenda sambamba ndio maana mmeona wanasiasa wanavyoumbuka mapema na mishe zao za wizi.huwezi kutojulikana ,inaweza chukua mda,lakini soe days yote yatajulikana.
 
Kama anawafahamu wabunge wa Chadema wanaofanya biashara na Tanesco awataje.
Kama anawafahamu wabunge wa Chadema waliopokea rushwa toka Tanesco ama wafanya biashara ili wawatetee awataje pia. Vinginevyo akae kimya, aache kupiga kelele awaache wazalendo wafanye kazi zao.

Kama majina ya watu waliotajwa na TL kufanya biashara na Tanesco kwahiyo kuwa na mgongano wa kimaslahi ingekuwa si kweli, nadhani nape angetoa utetezi wake, lakini kwa kuangalia aina ya majibu aliyoyatoa ni dhahiri kwamba TL amepiga mule mule.
 
Si nayeye awataje kuna ubaya gani akiwataja wabunge wala rushwa kama anaona wametajwa wa CCM tu basi ataje naye wa vyama vingine!!

Tena aanze na wale wa jengo linalodaiwa kuwa la uvccm makao makuu.
Ccm imezungukwa na sintofahamu kila kona kiasi kwamba kwa sasa haijitambui.
 
wanaongea nini hawa mafisadi wala rushwa na wasioweza kukemea rushwa??!
tuangalie historia............
karamagi
msabaha
balali
ngeleja
mkulo
nyoni
......
......
sijui wanakataa nini sasa?

mramba,
chenge,
lowasa,
makamba senior,
........
........
 
na yeye c awataje? Anabwabwaja nini kama ni zito aseme then atoe ushaidi, magamba bana wanatapatapa sana...
 
Ataje ataweza maana Ushaidi hawana wataambiwa wathibitishe hapo ndiyo timbwili litakapoanza na wao kuumbuka wanajribu kucheza kila aina lafu ili kuweza kujiokoa, walisema wametumiwa ujumbe wa kutishiwa kuuwawa lakini walipoambiwa kuna kifaa kimenunuliwa toka mashariki ya kati na mtoto wa kigogo wa serikali wakawa wakali na kukanusha kichama zaidi si wangeacha serikali kupitia huyo kigogo na ambaye hakutajwa ili akanushe, kisiasa CCM Inacheza Midundo ya Chadema. Waangalie sana huu muda ni wa kuteleza ilani yao ya chama na kufanya maisha bora na kama siyo mabovu kwa watanzania.
 
Mimi sioni kama KAWASHUKIA kwa namna yoyote hapo...Ninachoona hapo ni kulialia tu kama kawaida ya NAPE!
 
sasa wao CCM wanashindwa nini kuwataja hata hao wa CCM? kama Lissu kasema wa CCM, Basi nao CCM wasaweme wa CDM
 
Kweli Tundulisu ni kichwa yan kawa wekea mtego! Alujua Nape ataanza kupayuka kama kawaida yake!

Sasa Nape kama umeona list ijatimia na una ushahidi si umalizie!
 
huyo mropokaji wa serikali dhaifu hana sera ndo maana ameshindwa kuwataja wanaM4C waliopokea rushwa.
alivyokuwa na kiherehere angekuwa tayari kasharopoka ila amepigwa buti la uso haoni kitu.
 
Tuhuma za rushwa zimetolewa dhidi ya wabunge toka pande zote. Tofauti na CCM, CHADEMA wao wameshakaa chini na kohoji wale waliotuhumiwa. CCM wanaishia kutoa kauli za kulaani! Hapa ndipo tofauti inaanza kuonekana juu vya hivi vyam viwili vya siasa. CCM wanaonekana kuendeleza ngonjera za kutoa matamko wakati wenzao wameshamaliza internal investigation!

Na ni jambo la kusikitisha mwanasiasa kijana kama Nape anaonekana kuwa na akili za kizamani. Watanzania hawalalamikiii rushwa tu ila wanaudhika na tabia ya viongozi kutochukuwa hatua pindi tatizo linapotekea. Sasa hivi kuna bungeni kuna mbunge wa CCM ana kesi mahakamani ya rushwa, je, Nape alishafanya utaratibu ndani ya chama chake kumhoji? Na hawa wengine waliotajwa kwenye saga ya Tanesco, Nape anadhani njia sahihi ni kutoa kauli? mara ngapi watatoa kauli?
 
The same OLD STORY, Debe tupu haliachi KUTIKA!

Kama TL ametaja Wabunge tu wa CCM na kuacha wa CDM, kwanini Nape naye asiwataje wa CDM waliochwa?

Kati ya TL na Nape nani anayelinda ufisadi? TL aliyewataja kwa majina watuhumiwa au Yeye Nape
anayeficha majina ya watuhumiwa?.

Hivi mpaka hapa Nape na CCM bado hawajaona tofauti ya utendaji kazi wa CDM na CCM. Endeleeni kutumia vichwa vyenu kufunga nywele wakati wenzenu CDM wanatumia pia kwa kufikiri!
 
Back
Top Bottom