CCM yaishukia CHADEMA suala la TUHUMA za Rushwa kwa wabunge

Naendelea kupoteza imani na Bunge, pamoja na wabunge wote. Sioni nani msafi, wote wameoza. "WOTE NI CHUKUA CHAKO MAPEMA"
 
Nape ningekuona unaakili kama ungewataja wewe sasa kama Lissu kawaficha. Acha propaganda kaka.
 
Bunge limeundwa na siasa, habari za bunge na ruswa ni issue za siasa, Tundu Lissu na hayo majina yametokana na wabunge na taasisi yao (bunge) ambayo ni source yake ni siasa. Sasa Nape sikupati unaposema kuwa hili jambo si la kisiasa? atuambie sasa hili jambo ni la nini?
 
Nape nape; watu wazima hawatishiwi nyau! shutuma hizo za wabunge wa CCM kula rushwa ni sahihi; mbona mliowaita magamba mpaka leo bado umewakumbatia??!!
 
CCM imeanza lini kuchukizwa na rushwa? Nape usituone sisi kuwa wafupi wa kufikiri kama ulivyo wewe. Eti tunachukizwa na viongozi wanaojihusisha na rushwa, Kamdanganya mtoto wako wa mwisho. Kama imekuuma Lisu kuwataja anaowafahamu, na wewe wataje wa CHADEMA unaowafahamu. Nani asiyefahamu kuwa rushwa ndio utamaduni wenu?
 
Hana mvuto kwa hoja za ajabu ajabu. Hivi Nape alitaka kusema nini hasa?

Tuhuma ni tuhuma. Hiyo List ya Mh. Lissu ni mwanzo sio complete/mwisho. Mimi namfahamu Mbunge wa Bumbuli, J. Makamba kuwa ni mla rushwa mzuri. Kijana anahusika sana na michezo michafu iliyochezwa pale Wizarani na Tanesco. Lazima apewe nafasi kwenye list kamili.
 
Sara Msafiri na Munde Tambwe wote wawili ni wabunge viti maalum.....hebu ona hasara kubwa inayotakana na sheria na mifumo iliyooza. Mzigo mzito wa mishahara na marupuru yao ni hasara kubwa kwa Taifa.

Na kama haitoshi, si tu kwamba hawana tija in any positive way, bali wana huge negative impact in a costly way; ni MAFISADI.

Jamani, ni nani aliyeilaani nchi hii?
 
technique aliyotumia jana lissu imewasumbua sana ccm.....spika mwenyewe anapewa maelekezo ya nini afanye
 
Akili ndogo kuongoza akili kubwa hapa inaendelea kujionyesha. Tundu Lisu kawataja kwa majina na namna wanavyohusika, labda Tundu Lisu kwenye ile orodha alitakiwa awaongeze Pinda na Makinda kwani kwenye ule mgao wa kipindi kile cha Jairo, Pinda na Makinda nao walikula chao.
My take:
kwakuwa wahusika wengi inaonekana ni wabunge wa CCM msitegemee lolote la maana tena kuendelea hapa watakuja na kusema jambo liko kwenye uchunguzi tusubiri uchunguzi na utakluwa ndiyo mwisho wake, na baadaye watasema kulijadili jambo hilo ni kuingiklia mhimili wa bunge basi.
 
Kama anawafahamu wabunge wa Chadema wanaofanya biashara na Tanesco awataje.
Kama anawafahamu wabunge wa Chadema waliopokea rushwa toka Tanesco ama wafanya biashara ili wawatetee awataje pia. Vinginevyo akae kimya, aache kupiga kelele awaache wazalendo wafanye kazi zao.

Kama majina ya watu waliotajwa na TL kufanya biashara na Tanesco kwahiyo kuwa na mgongano wa kimaslahi ingekuwa si kweli, nadhani nape angetoa utetezi wake, lakini kwa kuangalia aina ya majibu aliyoyatoa ni dhahiri kwamba TL amepiga mule mule.

Wangeomba mwongozo jana jana....
 
Mwehu ameanza tena,nape utalaani sana lakini laana zinakimaliza cha chako.si nawewe utaje tukusikie kuliko kutishia na kujiongezea laana.
 
Na wewe nape wataje wote wa ccm na cdm kama unaujasiri!kama huwezi shut up ur mouth!ACHA UNAFIKI CCM NA RUSHWA DAMUDAMU
 
umeniwahi jibu langu Mpwa, yeah yaani kama wewe mwenzio kawataja kwanini na wewe usiwataje hao wa upande wa pili
..sasa na yeye si angewataja kwa majina wabunge wa CDM wanaotuhumiwa kwa rushwa? Nape aache unafiki.
 
Mimi naamini katika kweli na nasimamia katika Uzalendo na dhana ya upendo kwa Taifa hili, katika suala hili ni kuwa kila upande unajaribu kuvutia kwake ktk kuhakikisha kuwa wanabaki salama hata pale itakapobainika kuwa watu wao walihusika kwa namna moja ama nyingine katika hili la ufisadi.
Alichofanya Lisu ni kulivua jambo hili na kuwavisha CCM katika mantiki ya list aliyoitaja na alichokifanya Nape ni kulikataa joho hilo la ukoka wa miiba na kulitaka libaki bila mvaaji.
 
Jamani, au mimi sikuelewa? Mbona Lissu alizungumzia mgongano wa kimaslahi kwa baadhi ya wajumbe wa kamati. Sikuona tamko kuwa wamepewa rushwa! Sasa hili suala la rushwa limetoka wapi?
 
Back
Top Bottom