CCM yaishukia CHADEMA suala la TUHUMA za Rushwa kwa wabunge

Jamii forum liko biased, ukitoa maoni mazito ya kupinga kauli za wana cdm, hutaiona thread hewani lakini matusi ya wana cdm yanapewa kipaumbele. Naomba yeyote ambaye si pro-cdm aniunganishe na mtandao mwingine wa uwazi zaidi ambao unatoa fursa sawa kwa wote kutoa na kujibu huja hasa za wapuuzi hawa wa cdm. I HATE JAMII FORUM FOR THEIR BIASNESS. Fu*&*&*

sijui nikutukane vipi?! SSRA we
 
Nape anaongozwa na tumbo lake, mwache apige akadabra zake wenzake wanaenda na facts!
 
Swala la kuwavua magamba Lowasa na Chenge amemaliza? Mbona ameanza kurukia mengine!?


nape alizunguka nchi nzima kutangaza hizo siku 90 walizowapa mafisadi wajipime watoke wenyewe ...leo kaufyata ila ameshavuta posho kwa siku laki nane kodi zetu
 
Tuhuma za rushwa zimetolewa dhidi ya wabunge toka pande zote. Tofauti na CCM, CHADEMA wao wameshakaa chini na kohoji wale waliotuhumiwa. CCM wanaishia kutoa kauli za kulaani! Hapa ndipo tofauti inaanza kuonekana juu vya hivi vyam viwili vya siasa. CCM wanaonekana kuendeleza ngonjera za kutoa matamko wakati wenzao wameshamaliza internal investigation!

Na ni jambo la kusikitisha mwanasiasa kijana kama Nape anaonekana kuwa na akili za kizamani. Watanzania hawalalamikiii rushwa tu ila wanaudhika na tabia ya viongozi kutochukuwa hatua pindi tatizo linapotekea. Sasa hivi kuna bungeni kuna mbunge wa CCM ana kesi mahakamani ya rushwa, je, Nape alishafanya utaratibu ndani ya chama chake kumhoji? Na hawa wengine waliotajwa kwenye saga ya Tanesco, Nape anadhani njia sahihi ni kutoa kauli? mara ngapi watatoa kauli?

Mkuu mpotezee huyo, ni vuvuzela la magamba.
 
--Yadai orodha yake inalenga kupotosha tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.
--yadaiwa kutaka kuwaokoa wabunge wa Chadema katika sakata hilo.
--Yasema suala la tuhuma za rushwa kwa wabunge lisigeuzwe kuwa la kisiasa.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani juhudi zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kupotosha na kuuficha ukweli juu ya tuhuma za rushwa zinazowakabili baadhi ya wabunge.

Akizungumza na waandishi a habari leo mjini Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema, zipo juhudi za baadhi ya wanasiasa na vyama vya siasa kujaribu kulifanya suala la tuhuma za rushwa kwa baadhi ya wabunge kuwa la kisiasa kwa malengo yao.

"Mfano mzuri wa juhudi hizi ni kitendo cha Tundu Lissu, ambaye ni mbunge wa Chadema na Mnadhimu Mkuu wa Kkambi ya upinzani Bungeni cha kutoa aliyoiita orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kufanya biashara na TANESCO na kwamba ndio watuhumiwa wa rushwa inayozungumziwa", Alisema Nape na kuongeza;

"Cha kushangaza orodha yake ilikuwa na wabunge wa CCM peke yake wakati wote tunajua kuwa yapo majina ya baadhi ya wabunge wa vyama vingine hasa Chadema, yanayotajwa katika orodha ya wabunge wanaotuhumiwa kwa rushwa hii".

Nape alisema juhudi hizo za Lissu na wenzake zinalengo la kuuficha ukweli na kujaribu kuwalinda watuhumiwa wa uhalifu wanaotokana na Chadema.

"Tunamtaka Lissu na wengine wanaofanya juhudi hizo kuacha mara moja, na badala yake tuvipe nafasi vyombo vinavyohusika vichunguze na matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani ili tuwajue wabunge waliotusaliti", alisena Nape.

Alisema CCM inalaani vitendo vya rushwa hasa vinapohusishwa na viongozi ambao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa na kwamba rushwa ya namna hiyo inavuruga sana uchumi wa nchi, hivyo wanaohusika nayo haitoshi kuwaita wala rushwa tu bali ni zaidi ya wahujumu uchumi.

"Wakikithibitika ni muhimu hatua kali zichukuliwe kulikomesha kabisa hili na iwe fundisho kwa wengine", alisema Nape.

Nape alisema CCM inawapongeza watendaji wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini wakiongozwa na Waziri wao Prof. Sospeter Muhongo, Manaibu wake, Massele na Simbachawene na Katibu Mkuu, Maswi kwa uzalendo, ujasiri na umahiri wao mkubwa waliouonyesha kwa muda mfupi waliokaa kwenye wizara hiyo.

"Tunaamini uzalendo walioonyesha katika kusimamia wizara hii,utaigwa na watumishi wengine wa umma katika kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimali za nchi zinalindwa ili kuhakikisha maisha bora kwa kila Mtanzania yanatimia. Tunaunga mkono jitihada zao", alisema Nape.

Alisema, pia CCM inalipongeza bunge kwa kuendelea kusimamia serikali na rasilimali za nchi katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa ya maendeleo.

"Tunawaomba waheshimiwa wabunge wazidi kutanguliza masilahi ya taifa mbele na uzalendo mkubwa katika shughuli zao za kila siku", alimalizia.
wanataka kusema CCM sio wala rushwa au? haiwezekani kuoga maji ya tope utakate, mwambie atupe list aliyokiri yeye mwenyewe kwamba chama chao kina wala rushwa na wakajiangalie wenyewe, na mpaka sasa hatua iliyofikiwa huyu jamaa kweli nepi
 
tuhuma za rushwa zimetolewa dhidi ya wabunge toka pande zote. Tofauti na ccm, chadema wao wameshakaa chini na kohoji wale waliotuhumiwa. Ccm wanaishia kutoa kauli za kulaani! Hapa ndipo tofauti inaanza kuonekana juu vya hivi vyam viwili vya siasa. Ccm wanaonekana kuendeleza ngonjera za kutoa matamko wakati wenzao wameshamaliza internal investigation!

Na ni jambo la kusikitisha mwanasiasa kijana kama nape anaonekana kuwa na akili za kizamani. Watanzania hawalalamikiii rushwa tu ila wanaudhika na tabia ya viongozi kutochukuwa hatua pindi tatizo linapotekea. Sasa hivi kuna bungeni kuna mbunge wa ccm ana kesi mahakamani ya rushwa, je, nape alishafanya utaratibu ndani ya chama chake kumhoji? Na hawa wengine waliotajwa kwenye saga ya tanesco, nape anadhani njia sahihi ni kutoa kauli? Mara ngapi watatoa kauli?
great thinker so clever
 
Tundu Lisu kasema ambayo anayoyajua,tunayoyahitaji kuyasikia,yanayoogopwa kusemwa na wengine,

Nape na wewe tuambie unayoyajua kama unaweza?
 
Nape amesikika akisema, kiongozi yeyote au mbunge yeyote atakaye thibitika kala rushwa hafai kuwa mwanacham wa CCM, na amezungumza hivi baada ya tuhumu za rushwa zinazo ikabili baadhi ya kamati ndani ya bunge, na wanakamati wengi wakiwa CCM,

Ila nataka nimkumbushe huyu bwana kwamba baadhi ya wanachama wa CCM si tu kwamba wamekuwa wakituhumiwa kwa kupokea rushwa, ila wamekuwa wakithibitika kupokea rushwa,na hao hao waliothibitika kupokea rushwa,tunawaona bado wanadunda ndani na nje ya CCM, na CCM inajigamba nao kwa kuwapatia nyadhifa mbalimbali,

Na wengine kupewa hata kuongoza kamati muhimu kabisa ndani ya bunge,halafu Nape anasimama kifua mbele,mbele ya kadamnasi na kukiri udhaifu,wanadhania bado watanzania ni legelege kama yeye na ccm.
 
Nape amesikika akisema,kiongozi yeyote au mbunge yeyote atakaye thibitika kala rushwa,hafai kuwa mwanacham wa ccm,na amezungumza hivi baada ya tuhumu za rushwa zinazo ikabili baadhi ya kamati ndani ya bunge,na wanakamati wengi wakiwa ccm,ila nataka nimkumbushe huyu bwana kwamba baadhi ya wanachama wa ccm si tu kwamba wamekuwa wakituhumiwa kwa kupokea rushwa,ila wamekuwa wakithibitika kupokea rushwa,na hao hao waliothibitika kupokea rushwa,tunawaona bado wanadunda ndani na nje ya ccm,na ccm inajigamba nao kwa kuwapatia nyadhifa mbalimbali,na wengine kupewa hata kuongoza kamati muhimu kabisa ndani ya bunge,halafu Nape anasimama kifua mbele,mbele ya kadamnasi na kukiri udhaifu,wanadhania bado watanzania ni legelege kama yeye na ccm.


Msamehe! Hajui atendalo, chama kimeshakufa!
 
Nape amesikika akisema,kiongozi yeyote au mbunge yeyote atakaye thibitika kala rushwa,hafai kuwa mwanacham wa ccm,na amezungumza hivi baada ya tuhumu za rushwa zinazo ikabili baadhi ya kamati ndani ya bunge,na wanakamati wengi wakiwa ccm,ila nataka nimkumbushe huyu bwana kwamba baadhi ya wanachama wa ccm si tu kwamba wamekuwa wakituhumiwa kwa kupokea rushwa,ila wamekuwa wakithibitika kupokea rushwa,na hao hao waliothibitika kupokea rushwa,tunawaona bado wanadunda ndani na nje ya ccm,na ccm inajigamba nao kwa kuwapatia nyadhifa mbalimbali,na wengine kupewa hata kuongoza kamati muhimu kabisa ndani ya bunge,halafu Nape anasimama kifua mbele,mbele ya kadamnasi na kukiri udhaifu,wanadhania bado watanzania ni legelege kama yeye na ccm.

Mfano nani ambaye alithibitika kupokea rushwa na anaongoza kamati bungeni? Wewe naye wale wale tu mbona humtaji huyo? Hatutaki wanafiki humu JF.
 
Mfano nani ambaye alithibitika kupokea rushwa na anaongoza kamati bungeni? Wewe naye wale wale tu mbona humtaji huyo? Hatutaki wanafiki humu JF.
Chenge "vijisenti' na Radar. Ila serikali ya CCM imeamua kutouona ushahidi. Waingereza wanao uko waziwazi ni swala la kuuomba na kuutumia. Lowasa je? Bado mnadhani kuna anayeamini kuwa alijiuzuru kwa kuwajibika kisiasa tu?

Richmond/Dowans/Rostam Aziz zinamuuunganisha moja kwa moja Lowasa na sakata la rushwa katika dili ya hiyo mitambo. Mkapa je? Kiwira alipitia mchakato gani wa wazi uliompa huo mgodi? Hata kama umerudishwa (au ameiuzia tena serikali na kuvuna faida mara dufu) bado aliupata kwa rushwa.

Na TANESCO na NETGROUP SOLUTIONS!!!!! Nadhani hoja yako imejibiwa.
 
Hata magamba alituhakikishia yatang'oka....mpaka leo yameng'ang'ania.....na ni moja tu LILIJITOA nalo likapigiwa magoti baadae!
 
Si nayeye awataje kuna ubaya gani akiwataja wabunge wala rushwa kama anaona wametajwa wa CCM tu basi ataje naye wa vyama vingine!!

chama kichozoea kulinda wakwapuaji wezi, mafisadi, wanataka hilo lisiguswe nalinyamzishwe kimyakimya kama kova alivyolizima sual la ulimboka.Kuwataja hadharani ccm haikutaka sababu ati itaonekana ni mbaya kwenye macho ya kijamii.lakini nape anamdaganya nani?kila kukicha maovu ya serikali na wanachama wake yakiendele.wana ccm wengi wamekuwa wakilindwa wanapofanya ufisadi.kagoda iko wapi ,meremeta, deep green yako wapi?ndo sera ya ccm kulinda wanachama wake wasionekane wanakichafua chama
 
Huyu aliyeliyesema haya lengo lake nini? Kwamba hawa si wabunge wa ccm naingelikuwa raha kwake kusikia na chadema wamo? alichoandika siasa, walarushwa waliokamatwa ni wanaccm alafu tusiusiche suala hili na siasa?....Aliyewaloga hawa sijui nani?...
 
Dah, kumbe Rushwa ndani ya Siku ilianza siku nyingi sana. Je ni kiasi gani cha fedha kimetumika kama rushwa? Na je ile mil 200 ya Sherehe ya kufungua Bunge baada ya Magufuli kuhutubia, haipo kwenye kundi hilihili la Rushwa.
Watu wananufaika sana na ndo maana inatumika nguvu nyingi sana watu waweze rudi Bungeni. Refers; Uchaguzi wa Kongwa mwaka jana kuna mmoja wa wagombea ndani ya chama furani anaondekana akimtandikanbakora mwenzake.
 
Back
Top Bottom