CCM yahitimisha kampeni zake za Jimbo la Chalinze kwa kishindo

CCM yahitimisha kampeni zake za Jimbo la Chalinze kwa kishindo

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2013
Posts
5,536
Reaction score
2,268
MMG29423.jpg

MMG29338.jpg

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na Mkewe Bi. Arafa Kikwete wakiwapungia mikono wananchi wa Jimbo la Chalinze waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze wakiwasili kwa ajili ya kufunga Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
MMG29383.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,tayari kwa kufunga Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
MMG29289.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,leo April 5,2014 tayari kwa kufunga kampeni za CCM.Kulia ni Mke wa Ridhiwani Kikwete,Bi. Arafa Kikwete.
[img]http://4.bp.blogspot.com/-rXzmmcb91Mk/U0AZyQaeq7I/AAAAAAAFYrQ/tTnz1L1ZE_E/s1600/MMG29404.jpg
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa kufunga Kampeni za CCM,zilizofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze.


MMG29677.jpg

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa Mkutano wa kufunga Kampeni za CCM,zilizofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze.

STAY TUNED, HABARI ZAIDI ZIKO MBIONI KUWAIJIA KUPITIA JAMIIFORUMS (The Home of Great Thinkers. Where we Dare to Talk Openly!)
 
CCM imejaliwa hazina ya wanachama na viongozi wapenda wananchi na Taifa. Katika kujaliwa huko, ndiyo maana mpaka sasa ni chama kinachoendelea kupewa ridhaa ya kuwaongoza wananchi ili kuyafikia malengo yao ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Kuna baadhi ya wananchi waliaminishwa kilaghai kuwa uchaguzi wa Jimbo la Chalinze utakuwa ni nafasi ya kipekee ya kuanika uchafu wote ambao baadhi ya watu waliaminishwa kuhusiana na mgombea wa CCM, Ridhiwani Kikwete.

Kuna baadhi walikuwa wanaingojea na wanaendelea kuingojea siku hiyo bila kufahamu kuwa, fikra zao zilikuwa zimenunuliwa na viongozi walaghai wa kisiasa kwa sababu chama chao kimejengwa katika misingi ya kilaghai.

Viongozi wa CHADEMA Makao Makuu wamekimbia vivuli vyao vya kilaghai na kuwaacha wale waliokuwa wamejazwa fikra za kilaghai wakisubiri kusikia huo uchafu wa Ridhiwani Kikwete ukiainishwa katika mikutano ya CHADEMA. Where are they?. This was the best opportunity!!.

Huu ndiyo ulikuwa muda mwafaka wa kuueleza ulimwengu kuhusiana na uchafu wa kisiasa wa mgombea wa CCM kwenye majukwaa ya kisiasa na siyo chini ya uvungu wa meza za kisiasa.

Mwenyezi Mungu ana njia zake katika kuonyesha ukweli. Ukweli unatamalaki kila siku.

Kila siku tunasema, ulaghai wa kisiasa humea katika jamii kwa sababu hutumia lifti kuwafikia walengwa lakini pindi ukweli unapofika, ulaghai hujitenga huku walaghai wakijificha kama ilivyotokea kwa Viongozi wakuu wa CHADEMA katika Jimbo la Chalinze.

Hatutashangaa kuwasikia viongozi wakuu wa CHADEMA wakianza kupiga kelele za kilaghai kuhusu mgombea wa CCM katika Jimbo la Chalinze baada ya uchaguzi kumalizika. Hii ndiyo kasumba na mwonekano wa viongozi wa kisiasa walaghai.

CHADEMA lazima wajiandae na tsunami ya kisiasa inayowanyemelea Jumapili, Tarehe 6/04/2014.

Tunachoomba ni CHADEMA walete tena vijana kutoka Arusha na helikopta ili kulinda kura zao kama walivyofanya katika jimbo la Kalenga.

Karibuni sana katika Jimbo la Chalinze.
 
watawala wa ccm wametengeneza mazingira ya utawala wa kisultani akitoka baba anafuata mtoto, hivyo sisi wengine tutaishia kuwa walimu na police. watanzania tufanye mabadiliko. ccm wataimaliza nchi.
 
Sijakuelewa?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
watawala wa ccm wametengeneza mazingira ya utawala wa kisultani akitoka baba anafuata mtoto, hivyo sisi wengine tutaishia kuwa walimu na police. watanzania tufanye mabadiliko. ccm wataimaliza nchi.
Kama hufahamu hata maana ya neno UTAWALA, utaweza kufahamu maana ya kutengeneza mazingira ya utawala?.

He who knows not and knows not he knows not: he is a fool.
 
chama cha wauza madawa ya kulevya, majangili...
Mnaongoza kwa kuongea na kutukana huku mmejificha chini ya meza lakini uwanja wa wazi unapopatikana kama ilivyokuwa kwenye Kampeni za ubunge Jimbo la Chalinze, hamuonekani zaidi ya kuendelea kupiga kelele tupu.

Kama mama wa vifaranga amekimbia , ninyi vifaranga mtaweza?.

Waambie wanasiasa wako (Viongozi wakuu wa CHADEMA) wakayaseme mbele ya jukwaa la wazi haya unayoyasema huku umejificha chini ya meza.

Huoni viongozi wakuu wa CHADEMA wameamua mpaka kumkimbia mgombea wao kwa kuogopa kivuli cha ulaghai wao.

Ukweli umewakumba viongozi wakuu wa CHADEMA kama maporomoko ya Mto Nile. Hawaonekani mchana kwenye Jimbo la Chalinze. Wanakuja kwa kuvidhia kama wezi wa kisiasa.

Karibuni sana kwenye Jimbo la Chalinze siku ya Jumapili ili mzilinde kura za Mathayo Torongey kama mlivyolinda za Grace Tendega katika Jimbo la Kalenga.
 
watawala wa ccm wametengeneza mazingira ya utawala wa kisultani akitoka baba anafuata mtoto, hivyo sisi wengine tutaishia kuwa walimu na police. watanzania tufanye mabadiliko. ccm wataimaliza nchi.

Hekaheka hatuzioni jukwaani tulishazoe kusikia mipango chopa itapeleka Ugali na Ndondo kwa mawakala. Wabunge watakuja kusimama ktk kata kumsaidia yule mkwavi na kuna vijana wanakuja toka Arusha na Moshi kuja kulinda kura lakini hadi Sasa karibu tunaenda kulala kimya! Nilidhani hii ilikua fursa wahishimiwa wangetoka Dom jana leo wangekua wapo ktk mapambano lkn wapi bana ni dhahiri mmejielekeza kibla mnasubiri mchinjaji Riz One ajichinjie mpo lainiiii kama sufi!
 
Wenzenu CCM wamehitimisha kampeni za kishindo maskini CHADEMA mnafanya kampeni za vijipicha mlivyopiga huko karatu hahahaha
 
Sikipendi chama tawala but nadiriki kusema kuna aibu kubwa inayokingojea chama kikuu cha upinzani kwenye uchaguzi huu mdogo. Aibu.
 
Harufu ya aibu inanukia lakini anaelalamika ukoo ukoo, je chademachaga si ndiyo wanaongoza kubebana kama crdb
 
Mnaongoza kwa kuongea na kutukana huku mmejificha chini ya meza lakini uwanja wa wazi unapopatikana kama ilivyokuwa kwenye Kampeni za ubunge Jimbo la Chalinze, hamuonekani zaidi ya kuendelea kupiga kelele tupu.

Kama mama wa bifaranga amevikimbia vifaranga, ninyi vifaranga mtaweza?.

Waambie wanasiasa wako (Viongozi wakuu wa CHADEMA) wakayaseme mbele ya jukwaa la wazi haya unayoyasema umejificha chini ya meza.

Huoni wameamua mpaka kumkimbia mgombea wao kwa kuogopa kivuli cha ulaghai wao.

Ukweli umewakumba kama maporomoko ya Mto Nile. Hawaonekani mchana kwenye Jimbo la Chalinze. Wanakuja kwa kuvidhia kama wezi wa kisiasa.

Karibuni sana kwenye Jimbo la Chalinze siku ya Jumapili ili mzilinde kura za Mathayo Torongey kama mlivyolinda za Grace Tendega katika Jimbo la Kalenga.

Nimeambiwa kirefu cha CHADEMA ni Chaga Development Mission Agency hiki chama ni kama wakala wa kuendeleza missions 'mipango' ya maendeleo kwa wachaga tu... wengine ni kama hadaa tu!
 
Natabiri chadema kuanza kutuhumiana kwa wizi baada ya uchaguzi wa Chalinze.
 
Kila mtanzania anayelipenda taifa letu hawezi kuunga mkono huu urithi wa ubunge kwa mtindo huu hata kidogo! Je chalinze anayeweza kuongoza ni riz 1 tu?
 
Kila mtanzania anayelipenda taifa letu hawezi kuunga mkono huu urithi wa ubunge kwa mtindo huu hata kidogo! Je chalinze anayeweza kuongoza ni riz 1 tu?

Nashangaa hata hizo kampeni za nini wakati matokeo yako predetermined kuwa Riz 0 atashinda maana ni mwana wa sultani kwenye nchi ya kisultani. Demokrasia ya kisultani inanikumbusha Sam Kutesa wa Uganda alipogombea ubunge na Museven na Museven kupigwa mbali sana maana Sam Kutesa alikuwa na ujamaa na Paul Muwanga kiongozi wa muda wa Uganda baada ya Museven kwenda msituni baada ya kuona hakuna haki basi jimbo la Kutesa lilipigwa kikumbo na mfuasi wa Museven kabla Museven hajamrehabilitate Kutesa kuwa mwana NRA na sasa ni moja ya mawaziri mashuhuri Uganda na cha kushangaza hata ngazi ya Urais Museven anapeta kama analia wakati zamani hata ubunge alishindwa kuupata. Afrika hakuna demokrasia ya kweli ni wizi wa walio madarakani
 
Back
Top Bottom