CCM Yafanya Vurugu Hospitalini Sinza!

CCM Yafanya Vurugu Hospitalini Sinza!

MgungaMiba

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2011
Posts
999
Reaction score
816
Hospitali, kwa mujibu wa Sheria za nchi ni mahali pa wagonjwa wa aina mbalimbali, kwa hiyo haparuhusiwi makelele ya aina yoyote ya kuwabughudhi wagonjwa, labda kelele za wagonjwa waliozidiwa maumivu, ambazo madaktari hufanya kazi ya ziada kuzituliza. Madereva wa magari pia wanajua kuwa sheria hairuhusu hata kupiga honi eneo la Hospitali, akipiga honi anaweza kushtakiwa. Itakumbukwa pia pale madaktari wa Muhimbili walipogoma walileta vyombo vya mziki, wakafungulia kwa sauti kubwa, walilaaniwa na serkali kuwa wamekiuka maadili kwa kupiga makelele eneo la hospitali kwenye wagonjwa.
Sasa cha kusikitisha na kuhuzunisha, leo mida hii, CCM wanapiga bendi ya muziki kwa sauti kubwa huku mashabiki wake wakipiga makelele ya kushangilia kwa sauti kubwa na ya kuudhi ndani ya Hospitali ya Sinza, Dsm, tangu asubuhi, hali ya wagonjwa hospitalini hapo imekuwa mbaya, wagonjwa wengine. hasa wa Presha (HBP) ilibidi waondoke wakatafute matibabu kwengine, hapavumiliki. Tukaambiwa anakuja Kikwete, barabara kuelekea Hospitalini hapo zikafungwa, tukaondoka na mgonjwa wetu kwa miguu hadi Sinza Makaburini, tukakuta mzazi kwenye Kibajaji analia kwa uchungu, matrafiki walikuwa wanawake, wakavunja sheria kwa uchungu waliouona kwa mwanamke mwenzao, wakamruhusu apite, tulipowauliza wenzetu waliobakia, wakatuambia mzazi huyo alipofika getini hospitalini hapo alikumbana na vishindo vya muziki na makelele na kizaazaa, hali yake ikazidi kumuharibikia, alianza kujifungulia kwenye Kibajaji, manesi walipata wakati mgumu kumsitiri!
Kwanini CCM imefanya hivi?
Sherehe hizo wanamfurahisha nani? Mpaka kiasi cha kukera wagonjwa kiasi hiki?
 
Ccm wanadhani nchi ni yao kama Deo Filikunjombe alivyosema. Ndiyo maana wanavunja sheria ovyo wkijua kuwa mkuu wa nchi atawatetea, jeshi la polisi ni lao, mahakama nk vyote ni vyao.Lakini sisi tunajua mteteszi wetu yu hai, na siku si nying tutapata haki yetu. Poleni sana wagonjwa kwa maumivu mliyoyapata.
 
Mbwembwe za kupewa mkate mmoja . kweli ezezeta kitu kibaya sana
 
Ingekuwa vyama vya upinzan au wanaharakat,ungesikia saut ya KOVA
 
yani hao jamaa niwandewazimu sijapata ona,leo asubuhi nimefiwa na shemejiangu dadaake wakufatana na wife pale hospitali,chakushangaza wamenigomea kuingiza gari kuweza kupakia wafiwa waliokuwa hawajiwezi kwa uchungu wa msiba kisa wamepamba kwa ajiri ya sherehe.yani hawa jamaa niwa puuuuuz* mpaka nakosa jina la kuwaita
 
yani hao jamaa niwandewazimu sijapata ona,leo asubuhi nimefiwa na shemejiangu dadaake wakufatana na wife pale hospitali,chakushangaza wamenigomea kuingiza gari kuweza kupakia wafiwa waliokuwa hawajiwezi kwa uchungu wa msiba kisa wamepamba kwa ajiri ya sherehe.yani hawa jamaa niwa puuuuuz* mpaka nakosa jina la kuwaita

Watukane lile tusi baya ntakutetea kwa mods!!ni rafiki zangu sana.
Ccm zao ni vurugu tuu na baada ya hapo hujituliza kwa ngono zembe.
 
Kuna usemi usemao,mvunja nchi ni mwananchi mwenyewe na hii si hapa kwetu pekeee ila ni hata nchi nyingine
 
Hawa ni waswahili wa ghahawa na kashata na pia wahitimu wa shule zinazobaka waalimu. Hapo unatarajia nini cha maana kutoka kwao?
 
yani hao jamaa niwandewazimu sijapata ona,leo asubuhi nimefiwa na shemejiangu dadaake wakufatana na wife pale hospitali,chakushangaza wamenigomea kuingiza gari kuweza kupakia wafiwa waliokuwa hawajiwezi kwa uchungu wa msiba kisa wamepamba kwa ajiri ya sherehe.yani hawa jamaa niwa puuuuuz* mpaka nakosa jina la kuwaita

kumbe kweli duh basi hawa jamaa wanajali matumbo yao tu
 
kwa kweli kwa kitendo hicho sihamini kama kweli chama cha mapinduzi (CCM)kina washauri juu ya mambo ya kijamii. na tena sifikilii kama wanaelewa maana ya hospitali na wagonjwa. wametenda kitendo cha ajabu sana, pengine ni wenye vyombo vya muziki ndio ambao hawakuelewa kuwa mahali pale ni hospitali? lakini hata hivyo, kwani hawakuona majengo yale ya hospitali kuwa hayafanani na majengo ya chama chao wakauliza? mbona kule mori pana uwanja mkubwa tu wangekwenda wakapiga muziki na kucheza hadi asubuhi? kuliko kubughudhi ndugu na jamaa zetu waliotoka nyumbani kwa maumivu kwenda pale kupata tiba? imeniuma sana kwa kitendo hicho.
 
Back
Top Bottom