CCM yadai wafadhili wao wameisusa CHADEMA na Wafadhili hao ni Consevative Party | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yadai wafadhili wao wameisusa CHADEMA na Wafadhili hao ni Consevative Party

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 21, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  CHADEMA yapigwa kombora Arumeru

  CCM yadai wafadhili wao wameisusa

  Pamela Mollel, Arumeru

  C H A M A C h a M a p i n d u z i
  (CCM) kimesema siri ya Chama
  cha Demokrasia na Maendeleo
  (CHADEMA) kutembeza bakuli ya
  michango inatokana na wafadhili
  wake kukinyima fedha baada
  ya Serikali kukataa shinikizo
  lililotolewa na Waziri Mkuu wa
  Uingereza David Cameroon, la
  kutaka nchi zote rafiki na vyama
  vyote vya kisiasa kukubali ndoa ya
  jinsia moja.

  Hayo yalisemwa na mjini hapa
  jana na Mkuu wa Kampeni wa
  CCM Bw. Mwigulu Nchemba, kwa
  nyakati tofauti wakati akihutubia
  mikutano ya kampeni ya kumnadi
  mgombea wa chama hicho, Bw.
  Sioi Sumari.

  Bw. Nchemba aliipongeza
  Serikali ya Rais Jakaya Kikwete
  kwa msimamo wa kukataa shinikizo
  la Uingereza la kutaka ndoa za jinsia
  moja zisikubalike nchini.

  "CCM na Watanzania wote
  wanaunga mkono msimamo huo
  na hivyo tuko tayari kukosa misaada
  kuliko kukubali ndoa za jinsia
  moja," alisema.

  Aliwaambia wananchi kwamba
  siri ya CHADEMA kutembeza
  bakuli katika mikutano ya hadhara
  kwa wanachama wake ili wachangie
  kampeni ni kutokana na wafadhili
  wa chama chao Consevative cha
  Uingereza kinachoongozwa na
  Waziri Mkuu David Cameroon
  kukinyima fedha za misaada
  kutokana na Serikali ya Rais
  Kikwete kukataa kuunga mkono
  suala hilo.

  Alisema kuwa tangu chama
  hicho kianzishwe hakijawahi hata
  siku moja kutembeza bakuli na
  kuwakamua wanachama na wapenzi
  wake kwenye mikutano ya hadhara
  baada ya Serikali kukataa masharti
  ya ushoga na ndoa za jinsia moja
  kama ilivyokuwa imependekezwa
  na Uingereza sasa kimeibua mbinu
  hiyo ya kuwakamua wanachama na
  wafuasi wake.

  Aliongeza kuwa katika uchaguzi
  mdogo uliofanyika jimbo la Igunga,
  mkoani Tabora mwaka jana, chama
  hicho kilikuwa na fedha nyingi
  ambazo kilipewa msaada na ndio
  maana kiliweza kusumbua, lakini
  safari hii wamenyimwa ndio maana
  hata viongozi wao wa kitaifa
  ushiriki wao kwenye kampeni
  hizo za Arumeru Mashariki ni wa
  kusuasua.

  "Haiwezekani ghafla fedha
  w a l i z o k u w a w a k i z i f a n y i a
  mbwembwe kwenye uchaguzi
  wa Igunga zikawa hazipo na
  hapa wameshindwa kuonesha
  m b w e m b w e h i z o k u m b e
  wamenyimwa fedha kutoka kwa
  wafadhili sasa kazi waliyobakiza
  ni kuwakamua wanachama na
  wafuasi wao kwa kutembeza bakuli
  kwenye mikutano kama alivyofanya
  Mwenyekiti wa Taifa (Bw. Freeman
  Mbowe)," alisema Bw. Mwigulu.

  Aliwaambia wananchi kuwa
  wapinzani wameshindwa kueleza
  sera na matokeo yake wanaeneza
  propaganda za uongo, lugha za
  matusi na chuki.

  "Sisi tunaeleza ilani na sera za
  kumsaidia mwananchi kuboresha
  maisha sanjari na kutatua kero
  zilizopo hivyo mchagueni mgombea
  wa CCM ambaye sera za chama
  chake ndizo zinazotekelezwa na
  serikali iliyopo madarakani,"alisema


   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  So hiyo inamsaidia vipi mwananchi wa kawaida
  Ambaye hana maji au barabara au shule au madawati au ajira
  Wao wenye chama na sera nzuri mbona wameshindwa kuiendeleza arumeru miaka yote imebaki na hoi
   
 3. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  When brain's grey cells gets whiter this is the result...
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Unaposhindwa kujua wananchi wanataka kusikia nini unakuja na mambo kama haya
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwingulu just take the CCM tie from your Neck you will be able to think straight...
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Watanganyika amkeni muongo huyo! Hivi kwanini wanasiasa hawamwogopi mungu? Hapo wao walikuwa wanaomba DUDU au?
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]‘Mpeni Sioi ubunge mumfute machozi'
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 19 March 2012 09:23 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Sioi Sumari akiwa amebebwa na wafuasi wa chama chake CCM

  Mwandishi Wetu, Arumeru
  WANANCHI wa Jimbo la Arumeru Mashariki, wameombwa kumchagua mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia CCM, Sioi Sumari ili kumfuta machozi yaliyotokana na kifo cha baba yake mzazi, Jeremiah Sumari ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

  Mbali na hilo wananchi hao wameelezwa kuwa kwa kufanya hivyo, watakuwa wamejipatia baraka kwa Mungu kwani watamwezesha Sioi kupata mshahara utakaomwezesha kuendesha familia aliyoachiwa na baba yake.

  Mwito huo ulitolewa juzi katika Kijiji cha Migadini, Kata ya Mororoni na Mbunge wa Mtera(CCM), Livingstone Lusinde alipokuwa akimnadi mgombea huyo katika kampeni za uchaguzi mdogo zinazoendelea jimboni humo.

  Lusinde alisema wananchi hao wanastahili kuwa na moyo wa huruma kwa kumchagua kwa kura nyingi ili ajipatie mshahara wa kumwezesha kumudu familia aliyoachiwa na marehemu baba yake, ikiwa ni moja ya njia ya kumfuta machozi.

  "Mkimchagua Sioi mtapata baraka za Mungu kwa vile mtakuwa mmewezesha kutokea kwa mambo matatu… kwanza kura zenu zitamfuta machozi ya kufiwa na baba yake, pili mtamwezesha kupata mshahara utakaomwezesha kulea familia yake ambayo sasa haina baba," alisema Lusinde.

  Pia aliwaambia wananchi hao kwamba kumchagua Sioi kuwa mbunge wa jimbo hilo ni kumfurahisha Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa huyo ndiye chaguo lake na ndiye aliyeongoza vikao vya Kamati Kuu iliyokutana mara mbili kupitisha jina lake kuwa mgombea wakati wa mchakato wa kura za maoni.

  Alisema katika kura hizo za maoni zilizofanyika mara mbili, zote Sioi alionekana kushinda na kuibuka kidedea.

  "Njia pekee ya kumfurahisha Rais ni kumchagua Sioi kwa kuwa ni chaguo lake, hakika mtamfurahisha na Sioi ataweza kutekeleza vyema ilani ya chama," alisema Lusinde.

  Kwa upande wake, Sioi alisema anayaelewa vyema matatizo yanayoikabili Kata ya Maroroni ikiwemo ukosefu wa mashamba ya uhakika, maji, barabara na zahanati hivyo akichaguliwa, atayatatua matatizo hayo mara moja.

  "Nawaombeni sana mnichague kuwa mbunge wenu ili kwa pamoja tuweze kushirikiana kutatua kero hizi ambazo kimsingi zote nazifahamu vyema na nafahamu pia hatua za kuchukua ili kuhakikisha tunaondokana nazo," alisema Sioi.

  Shabiki wa Chadema
  Katika tukio jingine hekima na busara za Mratibu Mkuu wa kampeni za CCM, Mwigulu Nchemba zilitumika kuepusha maafa kwa mwanachama mmoja wa Chadema, aliyevalia sare za chama hicho baada ya kufika kwenye mkutano wa CCM katika Kata ya Kikatiti.

  Wakati Mwigulu akihutubia mkutano huo, mwanachama huyo wa Chadema, ghafla alivamia mkutano huo na kuanza kupiga mayowe huku akitamka maneno ya "Peoples Power" (Nguvu ya umma).

  Hatua hiyo iliwakera wafuasi wa CCM ambao waliamua kumtia adabu kabla ya Mwigulu kuingilia kati kuwazuia akiwataka wamwache kwani alikuwa anapaswa kufundishwa sera za CCM.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. E

  Elizabeth Dominic Platinum Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 4,547
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Duuh! Yaani nimesoma huku nimeshika kichwa mbona hawakufunga mahusiano ya kibalozi, mbona our dear leader ametoka UK juzi juzi....
   
 9. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,182
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Dah mambo mengine haya sio hata ya kuongea jukwaani
  ni ya kwenye vijiwe vya kahawa na maeneo ambako wamekaa wanywa kahawa
  Watu wamekuja kukusikiliza sera zako na unawaambia nini wajikomboe na umaskini wanaelezwa mambo kama haya
   
 10. MANI

  MANI Platinum Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280

  Dalili ya mfa maji hiyo haachi kutapatapa.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huyu Mwigulu anaumwa? Siamini kama mtu mwenye akili timamu anaweza kusema wa level ya juu kiasi hicho. Uingereza ndio wanaongoza kwa kuchangia bajeti ya serikali (General Budget Support). Approx. theluthi moja ya National budget ya Tanzania inatoka kwa Cameroon. Infact, Uingereza inazidi (kwa misaada hapa TZ) World Bank, IMF! Leo hii Cameroon akikataa kuandika cheque, serikali ya CCM itachemsha vibaya sana. Maajabu haya!
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Cameron akutana na JK, aisifu Tanzania

  28 January 2012 09:12
  Fredy Azzah
  RAIS Jakaya Kikwete amekutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na kufanya mazungumzo, huku kiongozi huyo wa Uingereza akisifia Tanzania kwa kupiga hatua katika sekta ya elimu na kilimo.


  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na kusainiwa na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Premiere Kibanga, Cameron alimweleza Rais Kikwete kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa kwa kuleta mabadiliko chanya kwenye sekta za kilimo na elimu barani Afrika.


  "Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ametoa pongezi hizo kwa Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yao jana (juzi) jioni hapa Davos, ambapo wote wawili wanahudhuria mkutano wa uchumi duniani wa kila mwaka, World Economic Forum (WEF)," inaeleza taarifa hiyo. Inasema katika mkutano huo masuala ya uchumi, ikiwamo athari zinazokabili uchumi duniani kwa sasa na jitihada mbalimbali zinazofanywa kuunusuru vitajadiliwa.


  "Afrika inapitia kipindi cha mabadiliko ambayo ni chanya, Tanzania ni mfano bora wa kuigwa katika hili," taarifa hiyo ilimnukuu Cameron akimweleza Rais Kikwete walipokutana juzi jioni. Inasema katika mazungumzo yao, Rais Kikwete amemweleza Cameron kuwa kilimo ni sekta kubwa na inayotegemewa na Watanzania wengi na kwamba, Serikali inalenga kujitosheleza kwa chakula ndani na nje ya nchi.


  Inasema Rais Kikwete na Cameron pia walizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu siasa na usalama barani Afrika. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awali juzi asubuhi, Rais Kikwete alijumuika na viongozi wengine kutoka Ethiopia, Guinea-Conackry, Kenya na Afrika Kusini kuzungumzia mabadiliko mbalimbali ya uchumi na maendeleo barani Afrika.


  Taarifa hiyo inaeleza kuwa, mjadala huo uliongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Gordon Brown, ambapo Rais Kikwete alisema bara la Afrika limepata athari mbalimbali zinazotokana na mabadiliko ya uchumi duniani. "Afrika ina mahitaji zaidi katika kutekeleza sera zinazolenga uchumi imara na kuwekeza katika sekta za elimu, utafiti, kilimo, viwanda na miundombinu," taarifa inamkariri Rais Kikwete.
   
 13. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Mkiambiwa hawa jamaa wameishiwa sera mnakataa, hapa wao walikuwa anataka kuchangiwa nywele wapeleke kwa mganga au fedha??? Mwigulu gonjwa ya akili, inaropoka tu hovyo kama mtu anayeharisha!!!! Hovyooooooooo!!
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mwigulu kapime akili...hivi kuomba watu wakuchangie ni kwasababu ya wafadhili? Kwanini Mwigulu anakuwa na mawazo ya kimaskini hivi? Mawazo yake yamekaa kitegemezi kama mtumwa vile,hii dhana ya misaada imewaathiri sana CCM.Mimi nasema,hata kama ni kweli misaada imekoma,hii dhana ya CDM kuwataka wananchi,wapenzi na wanachama wake kuchangia ni dhana inayofaa kuigwa na hata watawala wetu.Nguvu ya wananchi maskini ikiwekwa pamoja ina uwezo wa kuangusha utawala dhalimu wa CCM.
   
 15. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  mbona chadema mara nyingi tu inaendesha harambee kwenye mikutano yake?. hili halijaanzia arumeru. Mwigulu ni hopless sana.
   
 16. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ammh.......I cant see Mbowe here

  [​IMG]
   
 18. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  View attachment 49837

  Nadhani kuchangia fedha kwa mtandao si hoja, hoja ni kutembeza bakuli!!!!!! Akili nyingine bana yaani kweli Mwigulu anatumia masaburi kufikiri katika hoja ndogo kama hizi, je kubwa si ndiyo ataingia chaka kabisa!!!!
   
 19. w

  wikolo JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  "Sisi tunaeleza ilani na sera za
  kumsaidia mwananchi kuboresha
  maisha sanjari na kutatua kero
  zilizopo hivyo mchagueni mgombea
  wa CCM ambaye sera za chama
  chake ndizo zinazotekelezwa na
  serikali iliyopo madarakani,"alisema


  Kwa hiyo kuelezea CDM wanakotoa hela za kampeni ndo ilani na sera za kumsaidia mwananchi? Watu wengine bwana sijui wanawachukulia vipi hao wananchi wanaokuwa wanawasikiliza mikutanoni!!
   
 20. Kibwagizo

  Kibwagizo Senior Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 132
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kumbe Chadema ndio wakombozi wa Watanzania kama Mwigulu anajuwa kuwa wako tayari kumpoteza mfadhili kwa mambo yasiyo na tija.Viva CDM.
   
Loading...