Kama kuna mwaka ambao CCM walidhamiria kwa hali na mali kutaka kulichukua jimbo la Moshi mjini basi ilikuwa 2010 lakini ndio mwaka ambao CCM ilishindwa vibaya sana pale kuanzia kura za Urais, Ubunge mpaka udiwani.
Yusuph Makamba, Steven Wassira na Kikwete wanaijua vizuri sana Moshi mjini, kilichowakuta 2010 pale Moshi mjini nina uhakika hawatakisahau maisha yao yote. Maana wa waliwekeza zaidi ya bilioni tatu za kampeni pale Moshi mjini, waliweka kambi rasmi ya kampeni ikiongozwa na katibu mkuu wa CCM wa wakati huo Yusuph Makamba, na kumtumia Steven Wassira kwa wiki tatu mfululizo katika jimbo moja tu la Moshi mjini, wakipita kila kata na kila mtaa, walitumia kila bar kuhonga watu bia, lakini wapi, hiyo kitu akawageukia wenyewe. Kura zikapungua kabisa badala ya kuongezeka.