CCM yaanika vyanzo vya bajeti ya uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yaanika vyanzo vya bajeti ya uchaguzi 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 29, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,735
  Trophy Points: 280
  CCM yaanika vyanzo vya bajeti ya uchaguzi 2010

  Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th November 2009 @ 23:59
  Habari Leo

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeweka hadharani mkakati wake wa kupata fedha za kugharamia Uchaguzi Mkuu ujao ambapo kuna uwezekano Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Rais Jakaya Kikwete akahusika kutembelea mikoa kuhamasisha harambee ya kukichangia chama hicho.

  Aidha, chama hicho pia kinapanga kutumia hazina ya wanachama wake karibu milioni nne, kujipatia karibu Sh bilioni 40 kupitia mchango wa Sh 10,000 kwa kila mwanachama. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) Uchumi na Fedha, Amos Makalla, alitoa mkakati huo mwishoni mwa wiki na kuwataka wana CCM nchini kote kujiandaa kujitolea kukichangia chama fedha ili kifanikishe uchaguzi huo.

  Akielezea mikakati hiyo mjini Songea mwishoni mwa wiki, Makalla ambaye alipokea maandamano yaliyoandaliwa kusherehekea ushindi wa chama hicho kilichojinyakulia asilimia 97 ya viti vya vitongoji na vijiji katika Mkoa wa Ruvuma, kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika hivi karibuni, pia alitamba kuwa CCM itaendeleza ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mkuu 2010.

  Katika hotuba yake hiyo, Katibu huyo alieleza kwa undani mikakati mitatu ya idara yake itakayopendekezwa katika vikao vya chama hicho hivi karibuni kama njia ya kukipatia chama fedha kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi huo.

  Mikakati hiyo inahusisha kuchangisha michango hiyo ya Sh 10,000 ambayo ni ya hiari kwa wanachama, kufanya harambee za mikoa na kuhamasisha michango mingine kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi.

  "Hapa nina maanisha kama mwanachama mmoja mmoja wa CCM akichangia elfu kumi tena alipe kidogo kidogo kwa miezi sita, chama kina uhakika wa kupata Sh bilioni 40," alisema Makalla.

  Amewata viongozi wa mikoa na wilaya kuimarisha kamati zao za uchumi na kuandaa harambee za mikoa na ikibidi katika harambee hizo, mgeni rasmi awe Mwenyekiti wa Taifa na kuhimiza maandalizi hayo yaanze sasa.

  Kuhusu njia ya kutuma ujumbe kwa njia ya simu, Makalla alisema si muda mrefu chama kitazindua utaratibu utakaotumika mara baada ya kufanyika vikao hivyo.

  Amewataka Watanzania wenye mapenzi na CCM kujitokeza kwa wingi kutuma ujumbe mara baada ya uzinduzi huo kwani kufanya hivyo ni kukijenga chama chao.

  Amewahakikishia wanachama kuwa CCM itashinda uchaguzi ujao kwa kishindo kwa sababu ya mikakati kabambe ambayo wameanza kujiandaa nayo.

  Ameipongeza serikali kupeleka muswaada bungeni wa uwazi wa mapato na matumizi wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi na kuongeza kwamba muswaada huo umekuja muda muafaka sana na utasaidia vyama kuwa wazi katika mapato na matumizi.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nashauri Tanzania iwe na sheria ya kulimit na kuregulate kiwango cha pesa zinazo tumika kwenye uchaguzi. Hiyo itasaidia vyama vya upinzani viwe competative zaidi na pia ita saidia kupunguza kiwango cha pesa zisizo halali. Maana vyama vikiruhusiwa kutumia as much as they can ndiyo ina changia wizi wa pesa haswa za umma. Na kwa chaguzi za kwetu sh bilioni 40 naona kama ni nyingi mno. Anyway ni mtazamo wangu tu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,735
  Trophy Points: 280
  Hao watakaochanga hizo 10,000 natumai watajiuliza kwanza CCM imetufanyia nini katika kipindi cha miaka 5 iliyopita? Kama watakuwa wakweli wa nafsi zao basi wengi wao hawatachanga hata shilingi 10 badala yake hao omba omba wa CCM wataishia kuzomewa katika sehemu nyingi watakazopita.
   
 4. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kwavile mafisadi wengi wapo ndani ya chama hiki cha siku nyingi kama wanavyosema kuwa wote au karibu wote ni mafisadi huenda ndo watakao beba huo mzigo wa kuchangia ila sina uhakika kama mkulima wa kijiji mwana ccm anaweza changia kiwango hicho wakati hata chakula hana.
  Nadhani wangetumia mda vema kwa kuweka mipango ya kuwawezesha watu wapate maisha bora kama ilivyokuwa kaulimbiu yako kuliko kuweka ulafi wa madara mbele.
   
 5. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  nashangaa kwanini hawazungumzii kuhusu njii kuu ya kuwapatia michango.wana timu ya mafisadi kama kina rostam na wenzake ambao ndio watakao wapatia hayo mabilioni.yale mabilioni ya EPA,DOWANS,KAGODA,RADA na mengineyo mengi bado yapo kwenye account zao hivyo kutoa vijisenti kwaajili ya uchaguzi ujao hakutawasumbua,wanajua kwamba pesa zao zitarudi tu.wasitudanganye kwamba watapitisha harambee za elfu 10 kwa wanachama wao wakati tunajua halihalisi ya wananchi wa tanzania.na hata kama kuna watu wenye uwezo wa kuchangia hizo elfu 10 watakua wajinga wa kutupwa kama watazitoa kwa ajiliya ccm.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,549
  Trophy Points: 280
  Mwana FA1, Bilioni 40 sio nyingi, wanaweka makisio kama yale ya 2005 ambapo ni bilioni 40 za Kagoda, zilimaliza kila kitu!.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  But the question is mkuu did they really have to use that much money? Ndiyo maana nasema ina encourage wizi tu. That's why I suggest we set rules regarding campaign expenditures.
   
 8. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wanataka kutumia 40 bn kwenye uchaguzi ili waingie kwenye madaraka,so what? Nafikiri ilikuwa wawatumikie wananchi kwa uadilifu na maendeleo/maisha bora kwa kila mtanzani yangeonekana wala wasingehitaji hata 10bn za kampeni.
  Watanzania tusidanganyike tena,utatoa elfu 10 halafu unakuja kupewa rushwa ya sh elfu moja.UTAKUWA UMEPOTEZA PESA ZAKO NA HAKI YAKO.
   
Loading...