CCM yaamua kumng`oa Selasini jimbo la Rombo

CCM yaamua kumng`oa Selasini jimbo la Rombo

harakat

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
2,887
Reaction score
1,361
Imedhibitika kwamba CCM imedhamiria kuhakikisha mbunge wa Rombo Mh.Selasini harudi baada ya uchaguzi ujao. Hii ni kutokana na mkakati waliouweka baada ya kufanya tathmini ya uchaguzi mdogo uliopita.

Pamoja na hayo jimbo la Rombo linaonekana lina changamoto nyingi hivyo kuhitaji Mbunge kijana na makini ili kumudu mikiki ya eneo husika.

Katika kuchunguza ukweli wa hili mchunguzi wetu alipita maeneo ya kata ya mahango na nguduni na kujaribu kuzungumza na baadhi wa kazi ambao walilaumu kwamba kuna tatizo sugu la maji ambalo halijashughulikiwa kwa kipindi kirefu.

Hii inaonyesha kwamba Mbunge aliyepo ameshindwa achilia mbali changamoto ya maji bado kuna tatizo la uhaba wa madawati na matatizo mengine ya kielimu yanayoonyesha kwamba ameshindwa kuchapa kazi ipasavyo.

Nawasilisha
 
CCM haiwezi kuchomoza ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro.. labda Upareni ....
Imedhibitika kwamba CCM imedhamiria kuhakikisha mbunge wa Rombo Mh.Selasini harudi baada ya uchaguzi ujao. Hii ni kutokana na mkakati waliouweka baada ya kufanya tathmini ya uchaguzi mdogo uliopita.
Pamoja na hayo jimbo la Rombo linaonekana lina changamoto nyingi hivyo kuhitaji Mbunge kijana na makini ili kumudu mikiki ya eneo husika.
Katika kuchunguza ukweli wa hili mchunguzi wetu alipita maeneo ya kata ya mahango na nguduni na kujaribu kuzungumza na baadhi wa kazi ambao walilaumu kwamba kuna tatizo sugu la maji ambalo halijashughulikiwa kwa kipindi kirefu. Hii inaonyesha kwamba Mbunge aliyepo ameshindwa achilia mbali changamoto ya maji bado kuna tatizo la uhaba wa madawati na matatizo mengine ya kielimu yanayoonyesha kwamba ameshindwa kuchapa kazi ipasavyo.
Nawasilisha
 
Hivi ccm wanaviti vingapi hapo Rombo (Wenyeviti wa vijiji) labda tuanzie hapo kwanza..!!!

Halafu mwenye hilo jimbo katulia kimya hana papala wala nini, Uliza kazi yake aliyoifanya kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Ni kijana makini mjenzi wa hoja bobovu kwenye halaiki mpaka Mitandaoni, We subiri tu muda ufike achukue form. Ninaamini wana Rombo wanaimani naye na imani hiyo kwake wameionyesha kwenye uchaguzi Serikali za mitaa uliopita..

Wait an See.

BACK TANGANYIKA
 
Huelewi what you are posting to us,,,,,

Ccm has been in rombo for decades haijawahi kuwapa wananchi elimu, haijawapa maji wala haijui how those people are struggling to earn aliving!!!

Then keo chadema within have a decade unailaum haijafanya hayo ambayo ccm imeshindwa within 50years of rulling??????
Go a start a fresh,,, you are outdated!
 
Kwani Selasini anakusanya kodi?Au Selasini ni serikali inayotakiwa kuhudumia WANANCHI wake?

Hivi kazi ya MBUNGE ni kupeleka maji na kuahakisha madawati yanakuwepo kwenye shule za serikali?

Ni miaka mingapi upinzani wamekaa kwenye jimbo hilo VS CCM?

Sasa kama hii ni kazi ya MBUNGE kazi za serikali ni zipi.Mleta mada ukitufahamisha labda tutakuelewa.
 
Ni kweli pale kuna eneo toka huku mwika madukani ukifika kirimeni shuka mpaka huko mahida, mteri huko maji ni ya shida sana ila kuna miundombinu ya siku nyingi tu sema uvivu wa viongozi wameshindwa kufuatilia ili maji yatoke.
Pale pia kuna diwani wa eneo hilo Sijui wanafanya nn hawa watu Ni bora wananchi wafanye maamuzi magumu kama walivyomkataa Mramba
 
huyu chizi nae...amesambaza propaganda FB tumemshinda kwa hoja imebidi ahamie huku
 
Jimbo hilo linge mfaa sana KAMANDA Ben Saanane!!!!...
 
ccm kutawala rombo ni sawa na ndoto za kichaa kujenga ghorofa angani
 
Ni kweli pale kuna eneo toka huku mwika madukani ukifika kirimeni shuka mpaka huko mahida, mteri huko maji ni ya shida sana ila kuna miundombinu ya siku nyingi tu sema uvivu wa viongozi wameshindwa kufuatilia ili maji yatoke.
Pale pia kuna diwani wa eneo hilo Sijui wanafanya nn hawa watu Ni bora wananchi wafanye maamuzi magumu kama walivyomkataa Mramba
Hizo ni fitna tuu rombo ni jimbo la CHADEMA litaendelea kuwa CHADEMA ccm msahau kabisa kutawala rombo tena
 
Watanzania kwa kufikiri kwa ufupi na haraka mnapata 100%, kweli tokea Selasini awe mbunge hapo Rombo ndo ameng'oa mabomba yote yaliyokua yanatoa maji? na pia avunja madawati zote shuleni?

Hii kali!
 
Watu wanaangalia Mtu sio chama jamani.
Hawa wawakilishi wanaotaka huruma za wananchi bila utendaji unaonekana watapigwa chini 2015. Jimbo la Rombo linahitaji kijana na tayari CCM wameshamwandaa kijana mwenye shule ya kutosha tayari kwa kupeperudha bendera
 
Rock Spider,wapare tumeshituka,magamba hawafurukuti tena,enzi yao upareni imekwashaa waulize Anne Kilango Malecela na Matayo David Matayo wakueleze vipigo walivyovipata toka kwa wapare kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Ben saanane anaendeleza fitina zake kwa Selasini. Adui mkuu wa Selasini ni Ben Saanane sio CCM
 
Ben saanane anaendeleza fitina zake kwa Selasini. Adui mkuu wa Selasini ni Ben Saanane sio CCM

Hii haihusiani na kijana Ben wa saanane jamani hii ni CCM imejipanga vyema kumleta kijana wa Rombo atakae watumikia wanarombo
 
Back
Top Bottom