Kipindi kilichopita Chadema iliungwa mkono huko na Mashati ilikua ngome ya Mramba iliyogawanyika.Mashati ni tarafa yenye wapiga kura wengi zaidi hasa ukanda wa juu ikifuatiwa na Tarakea hasa tarakea mjini na nilichoona Selasini ameachia ngome yake hasa Tarakea mjini na Mashati anakotokea Ben.uchaguzi uliopita wagombea wote Selasini na Mramba walitokea mkuu.Frate anatokea Useri
Mkuu kama una nakala ya matokeo kata kwa kata hapo naomba uangalie tena...
1. Mashati haina wapiga kura wengi zaidi ya Tarakea. Tarakea ilikuwa na karibia nusu ya wapiga kura. Ukijumlisha na Usseri, especially Urauri, Ngaseni, Marongota, Kahe na Leto; tayari una zaidi ya 60 ya wapiga kura. Uchaguzi wa mwaka 1995 ulitoa picha halisi, kwani Tarakea na Usseri walibase kwa Salakana. Mashati wakabase kwa Ngalai na Mkuu na Mengwe wakabase kwa Mramba. Salakana alishinda kirahisi...
2. Hadi sasa Selasini ana strong hold Tarakea yote, mashima, Ngaseni, na Kahe, kuliko sehemu yeyote Rombo.
3. Mashati haitabiriki, na mara nyingi wanaangalia haiba ya mtu kuliko chama ama origin, hasa inapokuwa sio mtu wao. Lakini inapokuwa mtu wao. huwaambii kitu. Nadhani unakumbuka Ngalai alivyokuwa anatisha Mashati, pamoja na kwamba Mramba alikuwa favourite candidate...
4. Frate sio wa Usseri. Frate ni wa Tarakea, Nayeme. Kwa Tarakea Frate anaonekana kama "the best alternative" kama mgombea hatakuwa Selasini.
5. Usseri, hususani ukanda wa chini wenye wapiga kura wengi ni rahisi sana kushabihiana na maamuzi ya Tarakea. Refer uchaguzi wa 1995 utaona jinsi Salakana alivyobebwa na Usseri na Tarakea...
Comparison kati ya Ben na Frate...
Frate namfahamu "in and out", Ben namfahamu kupitia mitandao. In general, Ben will make a better MP than Frate... sio kwa maendeleo ya Rombo, bali kwa ujumla wa uhai na mchango wake kwa chama na taifa. Hata hivyo, kama tunataka kuangali mtu anayekubalika na atakayeweza kupambana na CCM ili jimbo libaki, Frate is far better than Ben. Frate amekulia Tarakea na anajulikana. Ukiuliza mtu yeyote Tarakea au Usseri atakwambia, yes, Frate anafaa, but asubiri kwanza Selasini aende kipindi kingine. Ukiwauliza kuhusu Ben, zaidi ya viongozi wa chama, kiukweli hawamjui.
Jipangeni...