CCM ya Waswahili wa Pwani itadumu?

CCM ya Waswahili wa Pwani itadumu?

HAPA we are missing the point.
Kweli ukitaka kuiondoa ccm lazima uwe na uwezo wa kupambana na vikwazo vingi kuliko kawaida.

Kama ccm imeshakubalika kuwa ni mbovu basi ni bora tuangalie ni wapi tunaweza walau kupata unafuu , je? ni kweli kuwa Mbowe ni mkabila kama watu tunavyotaka kuaminishwa ama ni zilezile propaganda za enzi za akina kingunge?

Kwani hamjui kuwa nchi hii tayari inatawaliwa kimajimbo?

Angalia mfumo mzima wa mahakama wao wanasema ni kanda , tofauti ya lugha.
Angalia mfumo wa hospitali za rufaa wao wanasema ni kanda.
Angalia mfumo wa ukaguzi wa elimu wao wanasema ni kanda sio jimbo.
Angalia upande wa TRA wao wanasema ni kanda siop jimbo.
Angalia mfumo mzima wa uendeshaji wa TANROAD wao wanasema ni kanda sio jimbo .

unaweza kuorodhesha kadiri utakavyoweza, ila hili halionekani kama ni kuendesha nchi kikabila ila ukisema majimbo unaonekana wewe ni mkabila , Mbowe badilisha sema kanda labda wasnaweza kukuelewa kwani jimbo hawaelewi.
 
Hii ni makala nzuri sana ingawaje hilo la CCM ya Waswahili wa Pwani nafikiri angeweza kuiandika makala hii bila kutumia kichwa hicho.

Kitu kimoja ambacho kinaanza kujitokeza, kila mtu anajua sasa kwamba CCM bomu, boti inaanza kuzama, lakini kitu ambacho wengi wetu tunakikosa hapa JF ni je liko wapi boti la kutuokoa? Tuna uhakika gani na lenyewe halivuji? Tuna uhakika gani na lenyewe halina mafisadi? Tuna uhakika gani kwamba sio tu linavuja, lakini kuna mamba wamekaa tayari kuturarua kabla hata boti halijavuka?

Nafikiri akina Ngurumo wangetusaidia pia kwa kutuonyesha sera za
vyama vya ushindani ambazo zitaweza kumwokoa Mtanzania.

Kuichukia CCM peke yake hakuwezi kuwa sababu ya vyama vya ushindani kuingia madarakani. Inabidi waingia kwa sera, kwa visions zao.

Lakini kwa muda sasa sioni sera zikijadiliwa zaidi ya kutuonyesha ubaya wa CCM, kitu ambacho wengi wetu tayari tunajua.

Mimi nitafurahi kuona mada pia za je kwanini nichague au nijiunge na CHADEMA, TLP, CUF au NCCR?

Interesting kwa kweli. Hoja ya kuhusu sera za vyama vya upinzania sio ngeni. Labda nianze kwa kusema hivi kinachokosekana katika nchi yetu na pengine katika nchi zingine za Afrika sio sera, bali uwezo (capacity) wa viongozi. Sera za CCM zinajulikana, sera za wapinzani zinajulikana na kwa kiasi kikubwa hazina tofauti. Sababu ya kutotofautiana kwa sera za CCM na wapinzani ni rahisi nayo ni ukweli kwamba hao wote wakiwa madarakani itabdi washughulikie matatizo yaleyale. Itabidi wajenge barabara, waweke mambomba ya maji, wapambane na malaria na ukimwi, wapambane na umaskini. Kwa hiyo kupata sera katika nchi zetu sio tatizo hata kidogo, tatizo ni uwezo, nia na utashi. Kwa hiyo tatizo tulilonalo hapa ni kwamba CCM imepoteza uwezo wa kupambana na matatizo ya nchi yetu kwa sababu mbalimbali ikiwemo uchovu. Kwa hiyo ndio tunasema kwamba tuwape wengine, ambao ni wapinzani yaani CHADEMA wakishirikiana na wenzao wa CUF, TLP na NCCR. Hawa nao tutawapa 5 years baada ya hapo tutawapima, tukiona wamefanya vizuri, tunawapa tena, tukiona wamepwaya tunawatimua tunachagua wengine na nchi inakwenda. Kwa nini tunaogopa mabadiliko? Mbona wenzetu Kenya waliitoa Kanu, wakamweka Kibaki, na sasa wana mpango wa kumuweka Raila, huyu naye akipwaya wataweka mwingine after five years na nchi yao inakwenda. Kwani sisi ni akina nani hadi tuogope mabadiliko kiasi hicho? Wapinzani tunawaongolea hapa ni watanzania wenzetu hawahawa akina Mbowe, Zitto, Slaa, lwakatare, Lipumba, Bimani, Duni, Mnyika, n.k. Hatutakopa watu kutoka nchi zingine!

Tuache visingizio, kama tunafikiri CCM wameshindwa, tunahaki na wajaibu wa kuwafukuza madarakani na kuwaweka wengine ambao wapo.
 
hii idea ya ubara na upwani na uzanzibari inapandikizwa kwenye akili za watu kwa kasi zote, ili ccm iwe rahisi kutawala.

na tuwe macho, hakuna kabila au mkoa bora kuliko mwengine, ni jinsi gani wewe utajiweka ndio cha umuhimu.

hizi propaganda za kikabila na zife, kabla amani haijavunjia

Gaijin,

Labda hatujaisoma vizuri makala ya Ngurumo. Naona baadhi ya watu hapa wanachangia si kutokana na makala bali kutokana na maoni ya wenzao. Kwa hiyo wanakuwa swayed katika judgements zao. Kwa mfano wewe hapa unasema ubara, upwani a uzanzibari unapandikizwa ... Mbona yenyewe ndiyo imeupandikiza? Tazama katiba ya CCM inavyogawa vyeo na nafasi kwa kuangalia ubara na uzanzibara. Tazama katiba ya taifa inayogawa madaraka kwa kutazama ubara na uzanzibara. Tazama sheria ya uchaguzi inavyozungumia ubara na uzanzibara wa wagombea urais. leo mnamlaumu Ngurumo kwa kuzungumzia 'CCM ya Waswahili wa Pwani?'

Kama nilivyoeleza hapo juu, nadhani wasomi wa fasihi hawapati shida kuelewa matumizi ya maneno hayo. Hata hivyo, tunaweza kuyatumia jinsi yalivyo, literally, na bado hoja ya Ngurumo ikabaki pale pale. Kwa mfano, Tazama viongozi na wapiga propaganda wakuu wa CCM ya sasa - kuanzia mwenyekiti Kikwete(Bagamoyo/Pwani); Makamba (Tanga/Pwani); Hiza Tambwe (Pwani); Salum Msabaha (Z'bar/Pwani?); Amani Karume (Z'bar/Pwani)...hawa wote wanapigapiga porojo za 'uswahilini' badala ya kujibu hoja. Kwa hiyo, tukimau kuwa literal, tunaweza bado kumuunga mkono mwandishi kuwa jamaa hawa wanataka kuendesha chama chao kiswahili swahili. Tukichunguza historia zao, hata kama baadhi yao hawaishi Pwani leo, hawa siyo waswahili wa Tabora ni wa Pwani.

Sasa kosa la Ngurumo ku-analyse hali hii ni lipi? Kama ni nchi kugawanyika, ilishagawanyika muda mrefu, iwe kwa majimbo, kanda, mikoa, wilya au kata. Mwandishi ameonyesha kilichopo, siyo yeye aliyekitengeneza, lakini kinaonekana kuwauma wale wasiotaka kuambiwa ukweli.

Kama ni kuvurugika kwa amani hakutatokana na makala kama hizi bali kutatokana na utawala mbovu unaowatenga watu katika makundi ya kimaslahi, na kukuza unyonyaji wa waziwazi.
 
na ccm ni nafasi hizo tu eeeh, makamo mwenyekiti bara pwani?, katibu mwenezi bara pwani? kurugenzi nyengine zote ndani ya ccm pwani? jumuiya za chama ya vijana wanawake na watu wazima ? pwani

huachi wewe?

suala la kuzungumzia katiba masuala ya zanzibar na bara vyama vyote viko hivyo kwa sababu hii ni jamhuri ya muungano wa bara na zanzibar, hata cCUF iko hivyo na nnategemea hivyo kote njoo na hoja nyengine
 
Mtu wa Pwani,

Samahani mkuu maana jina lako linafanana na usemi aliotumia mwandishi wa makala, lakini naamini alikusudia kuzungumzia dhana siyo jiografia. Hata mie nilipotoa hoja hapo juu nilisema tusilitazame suala hili literally, bali tulitazame kifasihi. Nikasisitiza kwamba kwa wale wanaotaka kulitazama kijiografia, nao wanaweza kupata maana fulani, hasa ikizingatiwa kwamba wapiga debe wakuu wa CCM sasa ndio hao akina Akwilombe, Hizza, na Makamba ambao kauli zao nyingi zimejaa 'uswahili.' Sasa wewe naona umechukulia serious kama vile mimi nasisitiza sualaa kijiografia. Ninachosema ni kwamba lazima tutafsiri hoja ya Ngurumo beyond jiografia ya 'Pwani' bali tutazame mantiki iliyokusudiwa. Au na sisi fasihi inatupiga chenga?
 
Back
Top Bottom