Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
CCM ya Waswahili wa Pwani itadumu?Ansbert Ngurumo
SASA ni dhahiri kwamba tuna vyama vya mapinduzi vingi ndani ya CCM. Kipo kimoja cha Jakaya Kikwete na Yusuf Makamba; kingine cha Ali Hassan Mwinyi na Malecela; kingine cha Yusuf Makamba na Aggrey Mwanri, na kingine cha kina Joseph Butiku.
Cha Mwinyi kinasikiliza, kinajifunza na kinasema kukosoana ruksa. Cha Kikwete, Makamba na Mwanri kinachekacheka na kucheza dansi, huku kikiigiza sauti na tabia za wapinzani kwenye luninga, kupotosha umma na kukwepa hoja katika mjadala wa kitaifa. Nguvu yake inategemea takataka za kina Richard Tambwe Hiza na wachumia matumbo wengine!
Kile cha kina Butiku ni mithili ya mimba inayomlilia mama yake asiitoe; kinatamani kuishi katika tunu, misingi na fadhila zilizokiasisi, lakini wenye nguvu wa zama hizi wanasema: no way!
Mzee Butiku wiki hii amekuwa shujaa mwingine wa kitaifa, aliyerejea kauli iliyohitimisha uhai wa Horace Kolimba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, kwamba CCM imekosa dira na mwelekeo. Tunaamini kwamba Mzee Butiku ataachwa aitetee kauli yake.
Naamini watawala walijifunza kwa tukio la kifo cha Kolimba, kwani laiti wangemuacha Kolimba afafanue kauli yake, CCM ya leo ingekuwa tofauti kabisa. Ingekuwa moja, imara na yenye dira aliyokuwa akiizungumzia.
Uimara unaoonekana sasa kwa CCM unatokana na serikali. Chama kinategemea zaidi nguvu ya dola. Nadhani niliwahi kusema huko nyuma kwamba CCM ya sasa ni kama KANU ya Daniel arap Moi. Ilipoondoka Ikulu haikuwa KANU ile ile.
Kauli ya Butiku kwamba CCM inaelekea kwenye kifo chake, imenikumbusha kauli ya kigogo mwingine aliyewahi kuniambia kuwa CCM ya sasa ni kama tairi la gari ambalo limetumika kwa muda mrefu, limejaa pumzi na sasa linakaribia kupasuka.
Alikifananisha chama hicho na dola nzee inayoelekea kwenye anguko.
Aliongeza kuwa CCM haipo tena, bali kuna mkusanyiko wa watu wanaofahamiana ambao hushikamana tu wakati wa uchaguzi. Hugawanyika na kufa mara tu baada ya uchaguzi, kwa sababu misingi imeshabomolewa.
Kwa mujibu wake, utawala wa sasa wa CCM na serikali ndiyo utakuwa chanzo cha anguko la CCM, kwa sababu uwezo wake sasa unategemea usanii, ubabe wa dola, ujinga wa wapiga kura, woga wa wananchi na mambo mengine.
Alikifananisha chama hicho na Dola ya Kirumi ambayo ilivuma sana kwa karne kadhaa, lakini wakati ulipofika dola hiyo hiyo ikamongonyoka taratibu na kuanguka kwa kishindo kikuu. Viongozi walijisahau, wakakumbatia anasa. Na miongoni mwa walioangusha dola hiyo ni maswahiba wao!
Kama dola ya Kirumi ilianguka, ni kipi kitaizuia CCM hii ya Waswahili wa Pwani kuanguka? Mwingine alisema CCM ya sasa imejengwa juu ya mbinu zilizoiweka madarakani mwaka 2005; mbinu za uchonganishi, kupakana matope, migawanyiko na ubaguzi.
Na kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ubaguzi unapopewa nafasi hauishii pale ulipoanzia. Unakuwa kama moto wa kiangazi.
Hisia hizi hizi nimeziona katika kauli ya mzee Butiku. Nimeona hasira na kukata tamaa. Zaidi ya hayo ni hasira ya muda mrefu. Kwa sababu zozote zile, watu makini hawawezi kupuuza kauli ya mzee Butiku, kama wengine wanaojaribu kutoa kejli za kitoto dhidi yake. Hoja yake iko imara.
Naamini mzee Butiku asingeibuka leo kusema aliyoyasema, wala asingefika mahali pa kuonyesha nakala ya waraka wake kwa mwenyekiti wa CCM, ulioandikwa miaka miwili iliyopita.
Chama chake kimempuuza na kimeshindwa kujirudi. Uvumilivu na ukimya wake vimefikia kikomo. Akaamua kuwajulisha Watanzania jinsi alivyopuuzwa na wale wale wanaojidai kumuenzi Mwalimu Nyerere.
Taifa litaendelea kumshangaa Katibu Mwenezi wa CCM, Mwanri anayemkejeli mzee Butiku na kumkemea akisema angepeleka maoni yake kwenye chama badala ya kuyaweka mbele ya waandishi. Mwanri anajifanya kichekesho kwa wanaojua kwamba naye ana waraka huo mezani kwake kwani mzee Butiku aliusambaza kwa wajumbe wote wa NEC tangu miaka miwili iliyopita.
Mwanri amezama katika siasa za usanii. Amesahau kumbukumbu zilizo kwenye mafaili yake.
Hakumbuki hata kanuni za chama, hadi mzee Malecela na Mwinyi wamkumbushe kuwa Butiku ana ruksa na haki, kwani aliapa: Nitasema ukweli daima, fitina kwangu mwiko.
Sisi tunabaki kujiuliza. Mwanri si Katibu Mwenezi wa CCM? Mwinyi si Mwenyekiti Mstaafu wa CCM? Malecela si Makamu Mwenyekiti wa CCM? Mwanri na Malecela wanaongoza chama kimoja? Sasa Mwanri anaeneza nini? Wote bado wanaiamini misingi, kanuni na imani za CCM?
Mambo haya yanatukumbusha simulizi la kauli mbili tofauti za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu mstaafu, Rashid Kawawa.
Ni kwamba, siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (alipostaafu rasmi siasa za majukwaani), katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM.
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM? Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi, nami naachana nayo, kwa sababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine...
Ndiyo maana aliwahi pia kusema kuwa maendeleo ya nchi yanategemea CCM madhubuti. Hii tuliyo nayo sasa ni goigoi! Ni huyo huyo pia aliyetamani CCM ikatike vipande viwili ili kuleta upinzani makini.
Je, yawezekana zama za upinzani makini ndo zinaanza kujiunda? Lakini je, upinzani makini utaletwa na watu waoga? Wako wapi wana CCM wengine, wenye uchungu na chama chao, wanaomuunga mkono mzee Butiku hadharani liwalo na liwe?
Kama wangejitokeza, hatua hii ingesaidia mambo kadhaa. Kwanza, ingewashtua watawala kubadilika na kurejea katika misingi wanayoitupilia mbali. Wangejenga na kusimamia upya misingi ya uongozi na utumishi bora kama ilivyoasisiwa na CCM.
Na kama wangeshindwa kubadilika, ingekuwa fursa ya hawa wasiokubaliana nao kujitoa kabisa ili wasiwe sehemu ya ubovu wanaoukemea.
Ni wazi kwamba wengi sasa wanakubali kwamba ni vigumu kukirekebisha chama wakiwa ndani. Bora watoke walisaide taifa wakiwa nje.
Kadiri wanavyoendelea kubaki ndani, huku wakijua kabisa kwamba chama kinaendelea kuzama, wajue kuwa wakati utafika nao watazama pamoja nacho, na hawatapata faida ya malalamiko yao.
Nashawishika kuamini kwamba kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai leo, asingekuwa ndani ya CCM hii. Yawezekana pia kuwa kama angekuwa hai, hata CCM hii isingekuwapo, maana asingewaruhusu waifikishe huko; au wao kwa kujua uwezo wake na adhabu ambayo ingeweza kuwapata, wasingejiruhusu kufika hapo walipo leo.
Watawala wetu wanajisahau. Mwalimu Nyerere bado ana nguvu leo katika mioyo ya Watanzania. Ni vema wajue kuwa misukosuko inayowapata leo inatokana na ukweli kwamba wananchi wamegundua kuwa watawala wetu wamempuuza Mwalimu Nyerere, na wanashindana na wananchi wake.
Wakubali, wakatae; vigezo vilivyowekwa na Mwalimu Nyerere ndivyo vitakavyoendelea kuwapima viongozi wetu wa sasa na wa baadaye.
Mwanzoni mwa utawala wa Rais Kikwete, baadhi ya mashabiki wake walianza kupenyeza hisia kwamba sasa amepatikana Nyerere mpya. Du! Hili nalo lilikuwa tusi kwa Mwalimu Nyerere, maana naamini hata Kikwete mwenyewe hawezi kudiriki kujifananisha naye.
Mwalimu Nyerere alikuwa mtu mwenye dhamira safi. Nguvu yake ilitokana zaidi na uadilifu wake binafsi. Alikuwa na uwezo wa kuwaambia ndugu zake na rafiki zake kile alichokuwa anawaambia Watanzania wengine wote. Hakuwa mpenda anasa. Hakutumia siasa kujitajirisha.
Ndiyo maana hata akiwa mstaafu, Mwalimu Nyerere alikuwa na nguvu kuliko hata dola yenyewe.
Wanaokumbuka jinsi alivyosambaratisha uamuzi wa Bunge lililoridhia Muungano wa serikali tatu, watakubaliana na nguvu ya Nyerere, ambayo pia ilichangiwa sana na uwezo wake wa kujenga hoja na kushawishi kwa kutazama pande zote za hoja.
Aliposhindwa kuwashawishi kwa hoja za kihistoria, akawarejesha kwenye sera za CCM, na kuwauliza: Serikali tatu ni sera yenu? Wakaitupa, hata bila kukubaliana naye, huku wakiogopa pia kuondoka kwenye chama.
Ushawishi wa Mwalimu Nyerere ulidhihirika pia katika mchakato wa kumpata mgombea urais kupitia CCM mwaka 1995, alipomwengua Kikwete na kumpitisha Mkapa. Hakuwa na dola. Alikuwa na karama ya ziada ambayo viongozi wetu wa leo hawana.
Mwinyi na Mkapa leo wana nguvu gani na ushawishi gani? Hata Kikwete hana ushawishi tena. Amebaki na nguvu ya dola, mabavu yanayotokana na uhalali wa urais wake. Akiondoka madarakani leo atakuwa kama Mkapa anayekimbia maswali ya wanahabari.
Ushawishi, uwezo na uadilifu wa Nyerere ndivyo viliifanya CCM yake iwe moja; iwe na nguvu. Naamini mambo haya haya ndiyo yaliwafanya wanaCCM waimbe zidumu fikra za mwenyekiti. Wao hawakuwa nazo; na hili limethibitika baada ya Mwalimu Nyerere kuondoka. Leo wanashindwa kujaza ombwe la uongozi linalojitokeza.
Wakati wanaomba kura wanatuletea fikra za Nyerere katika maandishi. Hazimo mioyoni mwao. Wakishapata madaraka wanatekeleza miradi yao na ndugu zao.
Ndiyo maana sasa wananchi wamegundua kwamba dawa ni kuwazomea. Kama watawala hawajifunzi kutokana na zomeazomea hii; wananchi wakimaliza kuwazomea watachukua hatua nyingine, labda kali zaidi. Wamechoka kudanganywa na kutumiwa.
Ndiyo maana habari za kusikitisha za wakulima wa Tandahimba kuchoma moto nyumba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Njwayo, zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari kubwa kwani sasa Watanzania wameanza kujipigania, kujikomboa.
Ni tukio ambalo mabavu hayataweza kulikabili, kwani linatoka mioyoni mwa wananchi. Ajabu ni kwamba mambo haya haya yanajitokeza wakati kina mzee Malecela wanajitapa (mbele ya wananchi wale wale) kwamba CCM inatekeleza sera zake. CCM ipi?
http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/10/21/makala2.php