CCM ya sasa ni ya kupambana na marehemu

CCM ya sasa ni ya kupambana na marehemu

Mama Samia anaupiga Mwingi sana.
Hilo halina ubishi.
Mama Samia ni Kiongozi.
Atuletee TU katiba mpya Kisha atawale milele kama Malkia wa Uingereza

Tanganyika iwe na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa JMT.
Zanziba iwe na Rais na Makamu wa pili wa Rais wa JMT na JM wa Tanzania iwe na Rais Wa Maisha ambaye ni Mama Samia.

Mambo ya Marehemu Magufuli na Sumaku gang sijui CCM na chawa zake ni mambo ya watafuta madaraka TU hayana tija Kwa Taifa
Ili hii nchi ipone ni lazima CCM ife chini ya Katiba yake iliyoiumba.
Hakuna mbegu inayoota bila kufukiwa ardhini na kufa na kuoza.
CCM ikiwa hai milele Taifa hili litakufa milele. CCM ikifa italihuisha Taifa hili. Tena CCM ikijiua yenyewe inaeweza ikafufuka lakini ikisubiri ikauawa na wananchi itakufa na kuzikwa milele.

Rais Samia weka katiba mpya yenye miiko ya uongozi.
Mifumo Bora ya Dola itakufanya uongozi nchi hii bila stress. Nchi hii Rais Hana Raha mpaka mana anafanya Yale yanayowafurahisha wezi na wapigaji huku yeye akiwa kama chambo Cha kuwanufaisha makada ambao wengi walitafuta Taifa hili mpaka wanavimbiwa na kula majivu ya maiti za wanyonge.

Haiwezekani Mtumishi wa umma Kwa miaka mitatu au mitano awe Bilionea kushindana na Wafanyabiashara walioanza biashara miaka ya 1980 huku ofisi yake ikinyooshewa vidole Kwa ufisadi lakini tume ya maadili inakosa nguvu ya Kikatiba kumwajibisha Kwa sababu Tume na Wanayetamani kumchunguza wote ni wateuliwa wa Rais. Kama Jambazi aliyevamia Clauds na Waziri wa Habari wakati ule. Waziri alipepwrushwa na hakuna kufungu Cha katiba kilichomsimamia.

Unakuta Wilaya maskini inabeba wateuliwa wa Rais watatu wa kula tu Kodi za wananchi wakati mipango yote Iko Dodoma.
Mama Samia alete katiba mpya basi, tulifikishwa mahala pabaya kwamba sanduku la kura likawa haliheshimiwi, TISS na Polisi ndo walikuwa sanduku la kura la CCM utake usitake. Magufuli kawatisha Wakurugenzi kuwa nakulipa vizuri halafu eneo lako ashinde mpinzani, sijui utanieleza nini? Uchaguzi ukawa unatoa watu anaotaka Magufuli, ona bunge lilivyo kibogoyo, hata wakiweka LIVE halinogi. CAG anatoa wizi wa kutisha kwa serikali iliyojidai inasimamia wizi. We're, Mwenyezi Mungu, tunusuru utuondolee chama hiki chakavu.
 
Huwezi kuumiza watu hi alafu ukawa Bora, huwezi kuamua uchaguzi unavyotaka wewe halafu ukawa Bora, huwezi kuulizwa na CAG tri. 1.5 ziko wapi halafu ukamfukuza ukawa Bora, huwezi kujenga uwanja wa ndege wa Kimataifa kwenu bila idhini ya bunge halafu cc ukawa bora. Hebu amkeni.
Mnachekesha!!!
 
RAISI WETU SAMIA SULUHU HASSAN dira na mwelekeo katika kutatua kero za watu na kufanya maendeleo ya wananchi yapo kwenye ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 cha ajabu kwa sasa wewe na team yako unayoiamini kuwa itakurudisha madarakani 2025 mmebaki kumchafua marehemu ambaye kwa sasa hawezi amka na kujitetea!

Angalia mwenyewe tangu umerithi kijiti hicho zaidi ya madarasa yaliyojengwa kwa tsh trion1.3 umefanya nini, miradi mingi inasuasua huku wananchi wakikamuliwa fedha za tozo tumeona mikopo mingi umekopa lakini hatujaona chochote ulichofanya!

Vijana wako wanakudanganya unaupiga mwingi huku wengine wakijiita nyuki wa mama hao vijana wameshakuingiza chaka na unahofia kivuli chao ukiamini uliokuwa nao 2015 hadi march 17/2021 hawafai na hawezi kukusaidia chochote.

Mfumuko wa bei wa vitu ni mkubwa na wewe kama raisi ulisema vitu vitapanda na kweli vimeshapanda kabla ya vita vya UKRAINE ulivyohadaa wananchi.! Miradi inasuasua mingi huku watu wakijipigia kodi za wananchi hutaki kusikia kelele za wananchi kwani hufanyi ziara yoyote kuwasikiliza na kujuwa kero zao huku ukiamini kwamba viongozi uliowateua wanakufanyia kazi ipasavyo!

Shindaneni na marehemu kwa maneno bila kufanya kazi mkiamini kwamba ushindi mtapata kwa njia yoyote ile lakini sasa hivi wanauelewa utaona mwenyewe 2025.

Nawatakia pasaka njema wazalendo wa taifa hili.
Dogo umesoma rporti ya CAG??
 
Kwa viwango na maono ya Magufuli hawa wanaomchafua wanaonekana makumbikumbi tu. Kama ni kufa kila mtu atakufa hata hao waliomuua Magufuli. Suala la msingi ni legacy ya maisha yake na katika hili mwamba atabaki katika kumbukumbu za marais wawili bora kabisa wa taifa hili vizazi hadi vizazi.
Ubora gani?
 
Wanahaha na hayati Magufuli sababu kawaachia viatu vikubwa mno wao kuvivaa. Too huge in size, unfit for the so called alive.
 
Back
Top Bottom