CCM ya Kinana inavyohangaika kukimbizana na CHADEMA ya Dkt. Slaa

CCM ya Kinana inavyohangaika kukimbizana na CHADEMA ya Dkt. Slaa

Kinana atahangaika mpaka suluari zake zitapopoka, chezea CHADEMA.

Kama alivyoanza hapa na kuja jukwaani na kandambili za kuogea.
ImageUploadedByJamiiForums1401984489.680994.jpg


Sent from my iPad using JamiiForums
 

KATIBU Mkuu Dk. Slaa aibua ufisadi mkubwa; ataka Ofisi ya Bunge ichunguzwe haraka


Katibu Mkuu Dk. Slaa ameendelea na ziara yake ya kuimarisha na kukagua uhai wa chama mkoani Tabora ambapo ametoa kauli juu ya masuala yanayoendelea bungeni akisema Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali anapaswa kufanya ukaguzi maalum haraka kwa Ofisi ya Bunge kutokana harufu ya ufisadi kwenye matumizi ya taasisi hiyo.

Amesema kuwa amenasa nyaraka za siri, zikiwemo barua za Katibu wa Bunge kwenda hazina zikiomba mabilioni ya fedha ambayo matumizi yake, hususan yale yaliyofichwa kwenye kichaka cha 'safari za ndani na nje' yananuka uvundo wa ufisadi unaofanywa na taasisi hiyo kisha kuuhalalisha kwa vitu visivyolingana na thamani ya rasilimali iliyotumika wala havina tija kwa wananchi.

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo mkoani Tabora, Wilaya ya Uyui, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika maeneo ya Tura na Kigwe, jimboni Igalula, akiendelea na ziara yake ya kutembelea mikoa minne, Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.


"Ndugu zangu wananchi wa Kigwe naomba kutumia nafasi hii kuzungumza masuala kadhaa ya kitaifa kabla sijazungumza masuala mahususi ya hapa kwenu kijijini, jimboni, wilayani na mkoani kwenu. Bila shaka mtakuwa mmesikia mambo yanayoendelea huko bungeni.


"Kwa muda sasa kumekuwepo na hoja inayohusu posho...posho za safari abazo wabunge wanatuhumiwa kuchukua kisha hawakwenda hizo safari. Imefikia mahali Spika Makinda ametoa maagizo...sasa mimi nasema hatuna tatizo kabisa na wabunge kuchunguzwa au kukaguliwa.

"Wakaguliwe wote kabisa...waliofanya safari za ndani na nje ya nchi. Wote...nasema hivyo kwa sababu ninawajua wabunge, wapo wanaoghushi hata risiti ili wapate malipo. Wapo wabunge badala ya kuwa watetezi wa mali za umma wamegeuka kuwa mstari wa mbele kuhujumu wananchi wao," amesema Dk. Slaa.

Amesema kuwa amenasa barua mbili za siri zilizoandikwa mwaka huu na Katibu wa Bunge kwenda hazina zikiomba jumla ya bilioni 52 ambazo zimetumika ndani ya miezi sita, huku matumizi yake yakiacha shaka kubwa hivyo akasema kama bunge linataka kuonekana 'relevant' kwa wananchi, ni lazima fedha hizo zikaguliwe.

"Barua ya kwanza inaomba jumla ya bilioni 23 kwa ajili ya matumizi ya Julai-Oktoba mwaka huu. Kwa wasiojua fedha hizi zinaweza kujenga takriban madarasa 300 yaliyokamilika yenye kila kitu bila kumchangisa mwananchi wangu hapa hata senti moja.


"Bunge limeomba fedha hizi kwa ajili ya posho ya jimbo, kwa ajili ya gharama za mkutano wa 14 gharama zenyewe hazijaoneshwa hapa, pia wameomba kwa ajili ya Kamati za Bunge, zingine ni kwa ajili ya kamati teule, kamati ya uchunguzi, pia wameomba bilioni 1 kwa ajili ya ziara za nje ya nchi za kamati.

"Kwa ajili ya ziara za kikazi ndani na nje ya nchi wameomba milioni 300 ambazo ni sawa na kituo kimoja cha afya kilichokamilika bila kuwachangisha wananchi. Pia wameomba kwa ajili ya matibabu ndani na nje ya nchi jumla ya shilingi milioni 130, ambazo wangeweza kuzitumia kujenga hospitali nzuri hapa nchini kila mtu anaweza kutibiwa, kwa ajili ya uendeshaji ofisi na mikataba gani sijui wameomba bilioni 1," amesema Dk. Slaa akinukuu barua hiyo.

Katika barua ya pili, Dk. Slaa amedai kuwa bunge limeomba jumla ya bilioni 29 kwa ajili ya Oktoba hadi Desemba, huku akisema fedha fedha hizo zingeweza kutumika vizuri kwa manufaa na maslahi ya Watanzania ambao bado wanahangaika kupata huduma za msingi ndani ya nchi yao.

"Hivi hizi fedha zingeweza kulipa madeni na mishahara ya walimu wangapi, zingejenga barabara za vijijini ngapi, zingehudumia wananchi kiasi gani katika elimu, afya au maji bila kuwachangisha michango ya ajabu ajabu. Hivi kuna mtu anaweza kuniambia thamani ya fedha za posho ya jimbo endapo hata wabunge hawaji majimboni kama huyu wa kwenu.

"Nani anaweza kuniambia hapa tija aliyopata au kama amesikia Kamati ya Bunge imemsemea mkulima wa tumbaku wa Tabora au hapa Igalula, nani anaweza kusema amepata tija kwa safari hizi za ndani au nje ya nchi za kamati za bunge au za ofisi. Ndiyo maana nasema, naunga mkono kabisa wabunge wakaguliwe, lakini tunataka ukaguzi maalum...performance audit ya ofisi ya bunge," amesema Dk. Slaa huku akishangiliwa na wananchi hao.

Amesema kuwa chombo hicho muhimu kwa ajili ya kuwasemea na kuwawakilisha wananchi kimeanza kupoteza maana kwa wabunge wakisaidiwa na kiti, kuanza kujikita katika masuala yasiyokuwa na umuhimu wowote kwa Watanzania wanaotaka kuwasikia wakijadili maslahi ya watu waliowatuma bungeni.

"Bunge limeacha kazi ya kutetea, kusemea na kuwakilisha wananchi, badala yake, wanageuza bunge sehemu ya majungu, vijembe, umbea wakisaidiwa na spika au naibu spika kulinda mambo hayo ya ajabu. Tunataka bunge lifanye kazi yake. Nimenyamza kwa muda mrefu. Nimekaa kimya muda mrefu juu ya bunge...


"CAG afanye huo ukaguzi maalum, tunataka kujua thamani ya fedha za walipa kodi Watanzania hawa. Wanapanga ufisadi mkubwa kama huu kisha wanatafuta namna ya kuuhalalisha kwa kupanga safari zinazoitwa za kazi au mafunzo...wakati hazina mpango wowote wala manufaa kwa Mtanzania," amesema Dk. Slaa.

Kesho Dk. Slaa ataendelea na ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ya majimbo ya Mkoa wa Tabora, akiwa amebakiza majimbo ya Bukene, Nzega na Igunga, kisha ataingia Mkoa wa Singida


 

Hapa alisema tatizo si mizigo, tatizo ni ufisadi na mafisadi! Nani anayewateua?


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willibroad Slaa amesema kuwa CCM kisiwahangaishe Watanzania kuwatajia majina ya mawaziri mizigo pekee, kwani suala la msingi ni namna ‘mizigo' hiyo inavyopatikana hadi kufikia nafasi hizo nyeti za utumishi.

Amesema kuwa kwa muda mrefu sasa chini ya utawala wa chama hicho katika serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete, kumekuwa na hoja ya uteuzi wa mawaziri, ambapo Dk. Slaa amesema haufanyiki kwa umakini na hauzingatii vigezo, bali uswahiba.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Uyui, mjini Tabora juzi jioni, Dk. Slaa alisema kuwa kinachoendelea ndani ya serikali hivi sasa sababu si mawaziri mizigo moja kwa moja, bali hao ni dalili ya tatizo kubwa hususan katika mamlaka ya uteuzi, akisema uongozi makini unapaswa kushughulikia kiini au chanzo cha tatizo.

Alisisitiza kuwa mamlaka ya uteuzi ikiwa makini inapaswa kuchukua maamuzi sahihi ya wakati kwa wateuliwa iwapo wameonekana wamekosea au hawawajibiki ipasavyo badala ya kuwazunguka na kuishia kuwataja majukwaani ikiwa ni njia ya kusukuma agenda ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.

Akifafanua zaidi, Dkt. Slaa alisema kuwa serikali ya Rais Kikwete iache ubutu linapofika suala la kuwachukulia hatua watendaji au viongozi wabovu, kwani suala la uwajibikaji likipuuzwa au kutiliwa mkazo ni moja ya masuala ambayo ama yamefanya nchi nyingi duniani zishindwe au zifaulu kuwapatia wananchi wake fursa za ustawi wa maendeleo.

Dk. Slaa ambaye anaendelea na ziara ya kuimarisha na kukagua uhai wa chama hicho mkoani Tabora ambapo juzi alikuwa maeneo ya Ugoweko, Kakola na Tabora mjini, alisema kuwa hata mabadiliko ya mara kwa mara ya Baraza la Mawaziri katika Serikali ya Rais Kikwete akidai yamekuwa hayana tija kwa Watanzania, ni dalili za tatizo kubwa la ukosefu wa uwajibikaji.

"Tuna tatizo kubwa la serikali butu. Serikali butu haiwezi kufanya maamuzi sahihi, muhimu kwa wakati. Haiwezi hata kuchukulia hatua mawaziri wabovu, wazembe au wasiowajibika kwa wananchi ipasavyo. Badala yake chama ambacho kimeunda serikali kinakwenda kutangaza majukwaani, wakati mamlaka ya uteuzi ipo kimya.

"Tunataka kuwaambia CCM, kama wanaendelea kudanganya wananchi, wananchi hawa wanajua mamlaka iliyowateua inaweza kuwa mzigo pia. Kwa nini inakaa kimya, wakati Rais ndiye anakaa na hiyo mizigo kwenye Baraza la Mawaziri. Sasa kama Rais anaongoza mawaziri mizigo na yuko kimya, wananchi wamweleweje.

"Hii ni dalili ya wazi kabisa kuwa tuna rais dhaifu. Sasa ni mara ya pili Rais Kikwete anashindwa kufanya mabadiliko ya mawaziri wake wabovu, badala yake anaanza kwa kuzunguka zunguka. Mawaziri mizigo hao ni dalili ya tatizo katika uteuzi unaofanyika bila kufuata vigezo, badala yake unaangaliwa uswahiba, ujomba," alisema Dk. Slaa.

Aliongeza kusema kwamba CCM wanapaswa kuwaambia wananchi ukweli juu ya chanzo cha ubovu wa serikali yao kwamba unatokana na kukosekana kwa uwajibikaji kuanzia ngazi ya juu hadi chini, ambao hatimaye umesababisha ufisadi unaoangamiza maisha ya Watanzania na kuongeza umaskini, ujinga na maradhi.

"Tatizo lililopo ni kwamba wote wameoza kwa ufisadi. Hakuna anayeweza kumwajibisha mwenzake moja kwa moja kwa sababu kila mmoja anamfahamu mwenzake. Hivyo dawa ukitaka kufanya maamuzi unazunguka zunguka ili wanaotakiwa kuondoka waone aliyewateua si yeye aliyewaondoa. Huu ni udhaifu," alisema Dk. Slaa.

CCM inatekeleza sera za CHADEMA kwa vitendo


Dk. Slaa ambaye jana aliendelea na ziara yake katika maeneo ya Mtakuja, Kaloleni, Lembeli na Sikonge mjini, wilayani Sikonge, alisema kuwa katika suala hilo la mawaziri mizigo, CCM wanalazimika kuzungumza sera cha chama hicho cha upinzani kwa vitendo.
Alisema kuwa amewasikia CCM wakilalamika kuwa kwa nini mawaziri hawafiki katika maeneo ya pembezoni mwa nchi wakati wananchi wanahitaji huduma za muhimu kutoka katika wizara husika.

"CCM wanalalamika eti kwa nini waziri hajafika mahali fulani sijui Namtumbo huko. Sisi tumewaambia siku zote, majibu yake ni kuwa na serikali za majimbo. Huwezi kutegemea katika nchi kubwa kama Tanzania Waziri wa Kilimo aliyeko Dar es Salaam ndiye anaamua kila kitu hata kwa mwananchi aliyeko mbali huko.

"Waziri wa Elimu au ajira ndiye anayetegemewa kuamua kila kitu cha kisera ndani ya nchi, yeye yuko Dar es Salaam anatakiwa kuwaamulia watu wa Namtumbo, watu wa Tunduru, watu wote wanasubiri Dar es Salaam inasemaje, CCM wanalalamika nini," alisema Dk. Slaa.


 

Aangua kilio taarifa ya Operesheni Tokomeza Ujangili na mateso ya wachimbaji wadogo


Wakati huo huo, Dk. Slaa alishindwa kujizuia kudondosha machozi baada ya kupewa taarifa za matukio mawili, yote yakihusisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola kwa usimamizi wa baadhi ya watendaji wa serikali.

Akizungumza na wananchi wa Kata ya Lusu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ng'wa…..juzi asubuhi Dk. Slaa alipewa malalamiko ya wakazi wa maeneo hayo wakiwemo wachimbaji wadogo namna ambavyo hawajanufaika na uliokuwa mgodi wa dhahabu uliokuwa ukimilikiwa na Kampuni ya Resolute Nzega.

Alishindwa kujizuia kutoa machozi, pale aliposimuliwa na kuoneshwa majeraha ya mateso aliyopata mmoja wa vijana ambaye familia yake iligundua dhahabu katika shamba lao pembeni mwa eneo la mgodi, lakini viongozi wakuu wa serikali kutoka wilayani wameamua ‘kuliteka' eneo hilo na kutumia askari polisi kuwashushia kipigo raia wanaofika hapo na kuwataka waondoke mara moja.

Akizungumzia suala hilo akiwa mjini Nzega, Dk. Slaa alisema kwa mambo yanayowatokea wananchi walioko karibu na rasilimali za nchi hii kama madini, yanatia huruma na kama serikali haiwezi kuchukua hatua kuwa upande wa wananchi wake, haitaweza kusafishika kwa mawaziri kujiuzulu.

"Nimeshuhudia kwa macho yangu kijana majeraha ya vipigo ambayo wananchi wale wamesema ni kutoka kwa askari polisi waliowekwa kulinda eneo hilo la mgodi ambao ulikuwa unawanufaisha wachimbaji wadogo wadogo. Yaani tumefikia mahali polisi wanatumika kiasi hiki…

"Sasa mgodi ule umegeuka kuwa wa wakubwa wenu wilayani (anawataja kwa vyeo, DC na OCD) ambao wanawatumia askari polisi kulinda pale, kisha askari hao wanafanya biashara ya kuruhusu watu wenye fedha wanaotoa shilingi milioni 2 hadi 3, wanapewa muda wanaingia kwenye mashimo hayo kuchimba dhahabu.

"Wananchi walioko katika maeneo hayo wanaambulia vipigo. Akina mama wanapigwa, biashara zao za mamantilie zimevurugwa, nchi hii inaelekea wapi wananchi wangu. Hata makaburu wa Afrika Kusini hawakufanya unyama kama huu. Jana tunatajiwa ya bungeni, kumbe huku pia mnayo ya kwenu," alisema Dk. Slaa.

Aliwaambia wananchi walioko karibu na uliokuwa mgodi wa Resolute kuwa chama hicho kitasimama kidete kuwatetea kwa sababu kimepata taarifa kuwa waliokuwa wawekezaji katika eneo hilo wanataka kumwaga maji kwenye mashimo ya machimbo hayo, hali ambayo inatasababisha madhara makubwa kwa binadamu kuokana na kemikali kusambaa.

Akiwa katika Kijiji cha Nanga jana, Dk. Slaa pia alishindwa kujizuia kudondosha machozi baada ya wabunge wake wawili, Conchesta Rwamlaza na Dk. Gervas Mbasa kuelezea kwa kina na mifano hai, juu ya ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili wakionesha namna ambavyo wananchi wasiokuw ana hatia wamefanyiwa unyama wa kutisha.

Wabunge hao walilazimika kusimama na kuhutubia mahali hapo, baada ya kumkuta Katibu Mkuu wao wakiwa njiani kwenda majimboni wakitokea mjini Dodoma kwenye mkutano wa bunge lililoahirishwa Ijumaa iliyopita.

JK kashauriwa vibaya bunge la katiba, asogeze muda mbele


Akiwa mjini Igunga mjini jana baada ya mkutano wa Nanga, Dk. Slaa mbali ya kufanya majumuisho ya ziara yake katika mikoa ya Kigoma Tabora, alizungumzia suala la kujiuzulu na kuwajibishwa kwa mawaziri hivi karibuni bungeni, akisema kuwa walioondoka ni dagaa, mkubwa wao aliyesimamia na kutoa kauli bungeni kwamba wananchi wapigwe ambaye ni Waziri Mkuu Pinda bado yuko madarakani, endapo hataondoka wananchi wang'ang'anie shingo ya rais wao Kikwete.

Akinukuu ripoti ya Kamati ya Bunge juu ya Operesheni Tokomeza Ujangili, Dk. Slaa alihoji inakuwaje Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi na Usalama wa Taifa wanahusishwa katika unyama waliofanyiwa wananchi, halafu wakuu wa taasisi hizo wakaendelea na kazi kama kawaida.

Alisema kuwa ikilazimika vyombo hivyo vya dola kusukwa upya ili viwe vyombo vyenye maadili vinavyotumikia wananchi, Rais Kikwete hana budi kufanya hivyo kwa maslahi na matakwa ya Watanzania.

Wakati huo huo, Dk. Slaa ametoa rai kwa Rais Kikwete kusogeza mbele muda wa makundi mbalimbali ya kijamii na asasi za kiraia kutuma majina kwa ajili ya Bunge la Katiba, kwa sababu aliotoa hautoshi kwa wananchi kushiriki kikamilifu kutumia fursa hiyo kutuma maombi yao.

"Katika jambo hili ama hakushauriwa au alishauriwa vibaya. Muda alioutoa wa hadi Januari 2, mwaka kesho ni muda mfupi
kutoka sasa. Hautoshi kwa wananchi walioko kila pembe ya nchi ambao wana sifa za kuwa wabunge wa Bunge la Katiba kuweza kutuma maombi yao kwa taasisi, asasi au makundi husika ili wapate nafasi hizo.

"Ni vyema akasogeza hadi Januari 15, ili kila Mtanzania kokote huko aliko mwenye sifa ya kutuma maombi na kuwa mbunge wa bunge hilo muhimu atume maombi ndani ya muda unaotosha. Vinginevyo asasi hizo au makundi hayo yatafanya kazi ya kuteua watu wanaotaka wenyewe waende kuchukua nafasi hiyo, CHADEMA tusingependa kufanya hivyo labda tulazimishwe na huu muda mfupi wa Kikwete," alisema Dk. Slaa.

Alisema kuwa hadi jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ofisi yake ilikuwa haijapata barua kutoka ikulu kuhusu suala hilo hivyo naye amesikia kwenye vyombo vya habari kama wengine, kwa hiyo muda utakaokuwa umebaki hadi mwisho wa kutuma maombi ni siku 7.

Alisema katika ndani ya siku 7 hizo kuna siku za siku kuu hivyo Rais Kikwete anapaswa kuzingatia mambo mengi ili wananchi wanaostahili wapate fursa hiyo.

Alisema kwa upande wa chama chake, kama hali itabaki hivyo hivyo, ofisi yake itatoa taarifa kwa wabunge na viongozi wote wa ngazi za chini kuwahamasisha wanachama wa chama hicho wenye sifa kwenye maeneo yao watume maombi yao ndani ya muda huo mfupi utakaokuwa umebaki.
 
Kiukwel tuseme ukwel
Mwisho wa CCM umefika. Mwananchi katawaliwa na CCM miaka 50 lakin hana hata maendeleo. Mwananchi anakuwa masikin lakin chama na viongizi wanakuwa matajiri. Sasa chaguo la Mungu linakuja kuikomboa kwa mara ya pili nchi ya Tanzania.
 
Dr.Slaa ana ujuzi gani wa kisiasa? Mzee Slaa baada ya kutoka kwenye upadri aliangukia kwenye siasa za kitapeli za CHADEMA.

Enock je Kinana baada ya kuzamia nchini akitokea somalia je ?
 
Naonea huruma kodi yangu tu hapo

Sent from my Nokia Lumia using Tapatalk
 
Swali zuri sana hili hapo kwenye bluu.

Tukilirejesha nyuma tutauliza, ...ni sahihi kwa CCM kushirikiana na CUF kuunda serikali Zanzibar miaka michache iliyopita, lakini sio sahihi kwa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kuungana ili kuing'oa CCM kwa wakati huu?...

c.c. Mwanadiwani

Naam ni kosa kubwa kwa upinzani kushirikaina na chama tawala> Tatizo linalotokea hapa ni kwamba wananchi wanakosa mtu wa kuwasemea na pia serikali inastarehe sana kwa sababu inakosa ile misukosuko ya upinzani! Upinzani kuungana na chama tawala sio sawa bali upinzani kuungana wao kwa wao ndio sahihi. Ndio maana kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa ni kitu cha mpito tu kwa sababu hiki kitu kinavisha demokrasia. Kwa akili yako wewe upinzani ukiungana na chama tawala ni nanai atamtetea mwananchi?
 
Naam ni kosa kubwa kwa upinzani kushirikaina na chama tawala> Tatizo linalotokea hapa ni kwamba wananchi wanakosa mtu wa kuwasemea na pia serikali inastarehe sana kwa sababu inakosa ile misukosuko ya upinzani! Upinzani kuungana na chama tawala sio sawa bali upinzani kuungana wao kwa wao ndio sahihi. Ndio maana kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa ni kitu cha mpito tu kwa sababu hiki kitu kinavisha demokrasia. Kwa akili yako wewe upinzani ukiungana na chama tawala ni nanai atamtetea mwananchi?

Mkuu mcfm400

Hapo kwenye bluu akili yangu haihusiki, maana tumeona hapa Zanzibar CCM na CUF zimeshirikiana kuunda serikali. Swali ndio hilo hilo nililouliza ambalo nawe umelijenga upya ati 'upinzani ukiungana na chama tawala nanai atamtetea mwananchi?'

Kwa mwelekeo wa siasa za Tanzania bila shaka swali hili likirejewa mara nyingi kadri iwezekanavyo inawezekana tukajua nani ni nani kwenye siasa, na kwa manufaa ya nani.
 
Chezea CHADEMA wewe wameshinda Chalinze , Kalenga , na Zenji yote kwa sababu ya Dr. Slaa
 
Naam ni kosa kubwa kwa upinzani kushirikaina na chama tawala> Tatizo linalotokea hapa ni kwamba wananchi wanakosa mtu wa kuwasemea na pia serikali inastarehe sana kwa sababu inakosa ile misukosuko ya upinzani! Upinzani kuungana na chama tawala sio sawa bali upinzani kuungana wao kwa wao ndio sahihi. Ndio maana kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa ni kitu cha mpito tu kwa sababu hiki kitu kinavisha demokrasia. Kwa akili yako wewe upinzani ukiungana na chama tawala ni nanai atamtetea mwananchi?

HUYU UNAYEHANGAIKA naye , MAISHA YAKE YOTE YANATEGEMEA CCM ! MKIONDOA CCM TU MMEMUUA KWA NJAA !
 
Kama alivyoanza hapa na kuja jukwaani na kandambili za kuogea. View attachment 162885 Sent from my iPad using JamiiForums
Alikuwa anatawadha.....akasikia kitu km peoples power kichwani akatoka ndugu akijidai kuwa ni msanii anaweza geuza kuwa upande wak ..ikabidi atoke nduki kuwahi jukwaa.
 
Back
Top Bottom