CCM ya Kinana inavyohangaika kukimbizana na CHADEMA ya Dkt. Slaa

Chief Isike

JF-Expert Member
Jan 17, 2010
445
462
Watu wengi hawajajua. Wanafikiri CCM ya Kinana inayofanya ziara sasa hivi, imeibuka from nowhere. Hapana wamelazimika kufanya hivyo baada ya kuzidiwa na mapigo ya CHADEMA ya Dkt. Slaa ambayo kama mnavyojua iliapa tangu baada ya uchaguzi kuwa itakuwa na kazi moja tu...kujenga chama. Kukipeleka CHADEMA kwa watu, kwa mikutano ya hadhara na vikao vya ndani, muda wote kikisikiliza na kuzungumza na wananchi hoja zinazohusu matatizo yao, maslahi na matakwa yao. Tunamwambia Kinana na CCM yake, ngoma ya CHADEMA kupitia kwa mtendaji wake mkuu na makini ni nzito. Kinana hana ubavu wa kufuta nyayo za Dk. Slaa ambazo hata mkuu wake Kikwete aliishindwa na ameendelea kusumbuliwa na kivuli cha Dokta wa ukweli. Hapa nitaonesha kwa uchache jinsi Kinana alivyolazimika kwenda Tabora kwa staili ile ile ya Dokta Slaa, kwa sababu Dokta alipiga vijiji mbalimbali vya majimbo yote ya Mkoa wa Tabora! Kote huko Dokta wa ukweli aliwakuna wananchi jinsi ambavyo alikuwa akiwaonesha wananchi kwa uwazi na facts namna ambavyo matatizo waliyonayo sasa yana uhusiano na utawala mbovu na kushindwa kwa sera za CCM.
 
Dr.Slaa ana ujuzi gani wa kisiasa? Mzee Slaa baada ya kutoka kwenye upadri aliangukia kwenye siasa za kitapeli za CHADEMA.
 
Uwezo wa KINANA kisiasa huwezi kuulinganisha na huu wa BABU SLAA.
msalani unachuma dhambi bure,yani unamfananisha gamba kinana na kamanda Dr.slaa!?wakati ukweli unaujua kwamba kinana kwa Dr.ni ushuz tu.
 
Anakulipa sh. ngapi mbona babu wa watu na chama chake wanajifia natural death let them rest in peace. Ni ubunifu wake tu, babu yenu si anatalii na UKAWA na wakimaliza mkutano wanasepa na choppa sasa wenzenu wanaweka kambi kwa muda kidogo. Hapa unalinganisha heavy weight na unyoya, na ndio kinachowacost siku zote. Nyie mnahitaji 10 more years ndio at least muwafikie nusu watu mnajilinganisha nao leo. Mkilitambua hili mtajipanga vizuri 2025 na sio 15 mnharibu resource tu.

Watu wengi hawajajua. Wanafikiri CCM ya Kinana inayofanya ziara sasa hivi, imeibuka from nowhere. Hapana wamelazimika kufanya hivyo baada ya kuzidiwa na mapigo ya CHADEMA ya Dkt. Slaa ambayo kama mnavyojua iliapa tangu baada ya uchaguzi kuwa itakuwa na kazi moja tu...kujenga chama. Kukipeleka CHADEMA kwa watu, kwa mikutano ya hadhara na vikao vya ndani, muda wote kikisikiliza na kuzungumza na wananchi hoja zinazohusu matatizo yao, maslahi na matakwa yao. Tunamwambia Kinana na CCM yake, ngoma ya CHADEMA kupitia kwa mtendaji wake mkuu na makini ni nzito. Kinana hana ubavu wa kufuta nyayo za Dk. Slaa ambazo hata mkuu wake Kikwete aliishindwa na ameendelea kusumbuliwa na kivuli cha Dokta wa ukweli. Hapa nitaonesha kwa uchache jinsi Kinana alivyolazimika kwenda Tabora kwa staili ile ile ya Dokta Slaa, kwa sababu Dokta alipiga vijiji mbalimbali vya majimbo yote ya Mkoa wa Tabora! Kote huko Dokta wa ukweli aliwakuna wananchi jinsi ambavyo alikuwa akiwaonesha wananchi kwa uwazi na facts namna ambavyo matatizo waliyonayo sasa yana uhusiano na utawala mbovu na kushindwa kwa sera za CCM.
 
asante kwa habari hii mkuu , ni hivi , UTAFITI HURU UNAONYESHA KWAMBA DR SLAA NDIYE mtu MAARUFU ZAIDI KISIASA KWENYE UKANDA HUU WA MAZIWA MAKUU , sasa mtu kama KINANA , AMBAYE VIJIJI VYOTE NCHI NZIMA VINAFAHAMU KWAMBA ANAMILIKI MELI INAYOSAFIRISHA MENO YA TEMBO , HAWEZI KUFUATA NYAYO ZAKE .
 
Kama hoja yako inachagizwa na hisia zako, basi huo ndiyo ukweli wako katika mtazamo wako.

Siasa haziendeshwi kwa hisia bali kwa ukweli kama unavyowadia kila siku. Chaguzi mbali mbali zinatoa akisi la kisiasa kwa sasa.

Ni CHADEMA hiyo hiyo ya Dkt. Slaa haikutaka nguvu nyingine katika uwepo wake kisiasa baada ya kudhani kuwa kura walizozipata wakati wa General Election 2010 zingetosha kuwafanya wasimame katika ulingo wa kisiasa bila political external power.

Ni CHADEMA hiyo hiyo ya Dkt. Slaa leo hii inatafuta uwezekano wa kushirikiana na vyama vingine na kuna sauti tunazisikia eti wanasema watashirikiana kuweka mgombea mmoja kwa kila chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais. Hii ina maana kuwa, mapigo ya CCM wameshindwa kuyamudu na kwa sasa wanatafuta msaada.
Mr Kinana says the main secret of CCM's survival for over 50 years is that it has a genuine internal mechanism to assess itself. "What has been helping us is a mechanism to assess ourselves from time to time, which we have cherished for decades," says Mr Kinana. "If you don't have a genuine self assessment mechanism, you are definitely going to collapse like Chadema today."

Chadema changes tack amid CCM onslaught - National - thecitizen.co.tz
 
Nafikiri thread ya mtu mzima Chief Isike inapaswa kuongezewa some facts kama hizi...

Dkt. Slaa aliingia Mkoa wa Tabora kwa kupitia Wilaya ya Kaliua, kisha Urambo, Sikonge, Igalula, Tabora mjini, Nzega kisha Igunga... Katika wilaya hizo, alifanya mikutano miwili hadi mitatu kwa kila jimbo. Maeneo mengi yakiwa ni vijijini. Tutaweka some facts kwa mkoa huo tu, eneo kwa eneo....

Kaliua...

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimetoa kauli kuhusu mabishano kati ya serikali na Tume ya Uchaguzi juu ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya katiba mpya, kikizitaka pande zote mbili kusema ukweli, badala ya kusema sababu ambazo hazipo. Kimesema kuwa kinaelewa kiini cha mabishano hayo, hivyo hakitakubali kura ya maoni ifanyike bila daftari kuboreshwa kama sheria ya uchaguzi inavyoagiza.

Katika kauli hiyo chama hicho kimetoa madai mazito kuwa kinazo taarifa kwamba hakuna maelewano kati ya Serikali na NEC, kwa sababu tume inataka uandikishaji mpya wa daftari zima badala ya kufanya maboresho ambayo serikali inataka kuyatumia kulinda maslahi Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye mchakato wa katiba mpya.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara jana katika Kijiji cha Mwendakulima, wilayani Kaliua, ikiwa ni siku yake ya kwanza akiwa mkoani Tabora akitokea Mkoa wa Kigoma, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibroad Slaa alisema kuwa katiba ni suala nyeti ambalo mchakato wake unapaswa kuwa jumuishi kwa gharama yoyote. Aliongeza kusema kuwa suala la uboreshaji wa daftari la wapiga kura ni takwa la kisheria wala halitegemei hisani ya mtu kwa kisingizo chochote kile ikiwemo gharama au ukubwa wan chi.

"Tumepata taarifa kwamba serikali na NEC yaani Tume ya Uchaguzi wanabishana…wanavutana kuhusu kuboreshwa kwa daftari la wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni ya katiba mpya. Wakati serikali wanasema wameshatoa fedha, tume inasema haiwezekani kwa sababu muda ni mdogo kulingana na ukubwa wa nchi na gharama ni kubwa. "Tunataka kuwaambia kwamba kwanza suala la uboreshaji wa daftari hilo si suala la hisani ni takwa la kisheria.

Kama nchi imeamua kuwa ya demokrasia haiwezi kutoa visingizio vya muda, ukubwa wa nchi na gharama kwa sababu demokrasia yenyewe ni gharama. Lakini pili, ambalo ndilo kubwa zaidi, hawasemi ukweli.

"Tunazo taarifa kwamba wanachobishania ni kuboreshwa au kuandikwa upya. Tume ya Uchaguzi wanajua daftari hilo la sasa limechakachuliwa sana sana kwa maslahi ya CCM, halifai tena. Hivyo kitu pekee kinachoweza kufanyika ili kunusuru mchakato huu kufanyika vizuri ni kuandikwa upya. Serikali haitaki hivyo. Tunajua hawataki kwa sababu wanataka kulinda CCM," alisema Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa ambaye jana ameingia mkoa wa tatu akiwa katika ziara ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama hicho katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida, alisema kuwa serikali isifanye mchezo na mchakato wa katiba mpya kwani endapo daftari hilo halitafanyiwa kazi, kuna hatari wananchi wengi wakakosa haki yao ya kikatiba.

"Mchakato wa katiba mpya unapaswa kuwa jumuishi kwa gharama yoyote ile. Hatuwezi kukubali wananchi wengi ambao ni vijana wenye sifa za kupiga kura kuamua hatima ya nchi yao kwa kupiga kura ya hapana au ndiyo kwenye katiba mpya, wasipate haki yao eti kwa sababu yeyote ile," alisema Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa jana alikuwa na mikuano miwili Mwendakulima na Kaliua mjini, ambapo leo ataendelea na ziara yake kwa wilaya ya Urambo, ambapo atafanya mikutano katika Jimbo la Urambo Kaskazini, ambalo linaongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.
 
Dr.Slaa ana ujuzi gani wa kisiasa? Mzee Slaa baada ya kutoka kwenye upadri aliangukia kwenye siasa za kitapeli za CHADEMA.

Kubali tu ukweli kaka! Nini kimewakurupusha CCM kila kukicha muko barabarani mnawapigia watu magoti na kujifanya kulilia shida zao? Sio spidi ya chadema imewatisha kweli? Kwa nini kinana imebidi atoke kustaafu siasa aje kuhangahika mikonai kuitetea CCM? Tatizo ni chadema inatishia ulaji wa maCCM. Hata kam kuna jambo dogo leo CCM inafanya ni kwa sababu ya kuwaogopa chadema. Mikopo inayokopwa mpaka deni la taifa limefikia trilioni 29 ni kujaribu kujitutumua na vimiradi kutimiza ahadi kwa sababu chadema ipo inafuatilia mlichokiahidi na utekelezaji wake. Kwa maneno mengine lolote mnalofanya ni plus kwa chadema. Mkifanya vizuri sifa inaenda kwa chadema mkifanya vibaya mnajiweka katika hali mbaya uchaguzi unaofuata.

Tunamshukuru mungu kwa kutuletea chadema walau CCM imeamka kidogo. Tunaomba nguvu ya chadema iongezeke mara dufu labda hii nchi inaweza kubadilika! By the way ndio maana CCM wanapambana na chadema kwa kila hali kuhakikisha wanawamaliza ili wao ccm wapumue kidogo na waondokane na mateso haya ya kuzunguka mikoani muda wote kujaribu kulaghai wananchi kwamba wananwajali!
 
Kama hoja yako inachagizwa na hisia zako, basi huo ndiyo ukweli wako katika mtazamo wako.

Ni CHADEMA hiyo hiyo ya Dkt. Slaa haikutaka nguvu nyingine katika uwepo wake kisiasa baada ya kudhani kuwa kura walizozipata wakati wa General Election 2010 zingetosha kuwafanya wasimame katika ulingo wa kisiasa bila political external power.

Ni CHADEMA hiyo hiyo ya Dkt. Slaa leo hii inatafuta uwezekano wa kushirikiana na vyama vingine na kuna sauti tunazisikia eti wanasema watashirikiana kuweka mgombea mmoja kwa kila chaguzi za Madiwani, Wabunge na Rais. Hii ina maana kuwa, mapigo ya CCM wameshindwa kuyamudu na kwa sasa wanatafuta msaada.

Siasa haziendeshwi kwa hisia bali kwa ukweli kama unavyowadia kila siku. Chaguzi mbali mbali zinatoa akisi la kisiasa kwa sasa.

Kwa hiyo hungependa kabisa chadema ishirikiane na vyama vingine vya upinzani? Mbona upinzani kushirikiana ni jambo la kawaida dunia nzima? Cha ajabu n nini?
 
Siasa haziendeshwi kwa hisia bali kwa ukweli kama unavyowadia kila siku. Chaguzi mbali mbali zinatoa akisi la kisiasa kwa sasa.

Kwa hiyo hungependa kabisa chadema ishirikiane na vyama vingine vya upinzani?
Mbona upinzani kushirikiana ni jambo la kawaida dunia nzima? Cha ajabu n nini?

Swali zuri sana hili hapo kwenye bluu.

Tukilirejesha nyuma tutauliza, ...ni sahihi kwa CCM kushirikiana na CUF kuunda serikali Zanzibar miaka michache iliyopita, lakini sio sahihi kwa CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kuungana ili kuing'oa CCM kwa wakati huu?...

c.c. Mwanadiwani
 
Back
Top Bottom