CCM Wasipogawanyika NCHI wataimaliza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Wasipogawanyika NCHI wataimaliza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ELNIN0, Dec 29, 2009.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  CCM wasipogawanyika ndani ya miaka 10 ijayo basi nchi yetu wataitafuna yote. Tumeshuhudia makundi mawili ndani ya chama hiki kikongwe kabisa lakini kadri siku zinavyozidi kusogea kwenye uchaguzi wanaweza kuwa kitu kimoja, wasiwasi wangu ni kwamba wakiungana tu (Mafisadi na Wasafi) sisi wananchi tumekwisha, watachukua kila kitu by the time tunashituka usingizini nchi nyeupee pee.

  Haya makundi pia yamesaidia changamoto hasa bungeni kusimamia utendaji wa serikali kwa ujumla ingawa baadhi ya wabunge wamepata kashi kashi kidogo in the process. ila wasiogope hakuna mapinduzi ya lelemama kokote duniani lazima upigane kufa na kupona na hawa mifisadi wana nguvu na mizizi ndani ya CCM usipime ndiyo maana baadhi ya wabunge wanatishiwa hata kun'golewa kwenye majimbo yao.

  Siku moja ningependa chama hiki kikongwe kimeguke ili kizaliwe kingine na hapo tutakuwa tumeingia kwenye stage nyingine ya demokrasia ya kweli, kwa sasa ni kama bado tuna chama kimoja tu.
   
 2. Nyuki

  Nyuki JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwahiyo ELNINO Vyama vyote vya upinzani hapa nchi kama CHADEMA,CUF n.k ni wasanii tu na hawana sera za maana za kuendesha Nchi bali ni CCM.BRAVO MKUU
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Nawatambua vizuri pamoja na michango yao na sera zao nzuri hasa CHADEMA, ila hawana nguvu ya kushika dola kwa sasa kwani wamebanwa kila kona Mkuu, niamini nisemayo hadi hapo kundi B toka CCM linakapomeguka ndipo demokrasia ya kweli itapepea tanzania.

  (Reference KANU - Kenya)
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,493
  Likes Received: 2,738
  Trophy Points: 280
  Elnino,

  Mfano wa Kenya does not hold water here. Watu wa Kenya hawakufuata mpasuko wa KANU ila baadhi ya viongozi wa KANU waliona alama za nyakati. Tatizo letu wananchi bado hawajaamuka na hawaamini nchi haiwezi kuongozwa na chama kingine zaidi ya CCM. Kwa taarifa yako wabunge wengi wa upinzani wana uelewa mkubwa kuliko wa wale wa CCM. Na vilevile upinzani inasimamisha watu bora kulinganisha na wale wa CCM. Sasa kama utawapa madaraka I am sure wanaweza kunda serikali bora kuliko ya CCM. Tatizo letu tunataka kusikia majina yale yale na ndiyo maana watoto wao wameanza kupokea vijiti.
   
Loading...