Ccm wapokea wanachama wanafunzi wa central sekondari

kibunda

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
403
52
Ndugu wadau, gazeti la mwananchi la jana, 16/4/2011 lilikuwa na habari kuwa, yale majigambo ya ccm (nape) kuwa wamepokea wanachama 670 pale nyerere square dodoma kumbe walikuwa ni wanafunzi wa shule ya mbunge wa jimbo la dodoma inayoitwa central secondary school. Wanafunzi hao walipelewa ama bila kujua leo au kwa kulazimishwa. Ndiyo maana katika wale waliopokea kadi walikuwa ni watoto tu na mkubwa mmoja. Huenda ndiyo dalili za kuishiwa kwa chama hiki
 
soma gazeti la mwananchi la jana huu siyo unafiki. WALA SINA SABABU YA KUANDIKA UNAFIKI.
 
Acha unafiki kijana, weka ushahid hapa sio unakurupuka tu.......NON SENSE

ushahidi gani wakati ni kweli na vijana 800 waliokwenda kutafutwa wakaletwa na posho wakapewa unakubaliana nalo mimi sinilikuwepo unabisha nin?? Ccm aipendwi hilo hata wao wanalijua
 
Taarifa wana Jf.
Mbunge wa Dodoma ni mmiliki wa CITY SEC cyo CENTRAL SEC. Hata hvyo ndo tabia yake huyo mbunge nimesoma pale namjua.
 
Wanafunzi wote 800 watakuwa na umri zaidi ya miaka 18 kweli??? Au ndo richipukizi ra thithiem
 
Yale yale ya Tambwe, kukusanya watoto wa shule hadi karimjee, kuzomea wapinzani wa mswada wa katiba. new gamba, the same strategies!! CDM songa mbele vijijini kuimarisha umoja na ukombozi wa taifa, naona ccm imeshindwa kutawala.
 
Wanafunzi wote 800 watakuwa na umri zaidi ya miaka 18 kweli??? Au ndo richipukizi ra thithiem
Kama vyuoni wanazuia siasa iweje kwenye shule za sekondari wao wanafanya....na kwa hali ya siku hizi wanafunzi wengi wa sekondari wako chini ya miaka 18...
 
achana na siasa wewe, hamna kijana anayeweza kujiunga CCM labda hao wa vijijini
 
Pia kuna habari ambazo tunahitaji kuzifuatilia kuwa mbunge wa dodoma mjini aliwaahidi wanafunzi wa shule yake mwaka jana wakati wa uchaguzi wampigie kampeni ili akipata ubunge awapunguzie ada. Ni kweli wanafunzi wa shule husika walishiriki kampeni kwa kiasi kikubwa. Kitu ambacho si uhakika nacho kama amepunguza ada ama hakufanya hivyo. Kama itatokea ametekeleza ahadi yake basi atakuwa amekiuka sheria ya gharama za uchaguzi na atakuwa ametoa rushwa.
 
...........Jamaa washenzi kweli,yaani walikataa siasa vyuoni wameenda mpaka sekondari...............................
 
Bado najiuliza wanamdanganya nani na ili iweje sasa??
Ninachofurahia hawa jamaa ni sikio la kufa, hawasomi alama za nyakati pia zaidi hawajifunzi kwa makosa yao wenyewe..... hawa si ndio walipewa faida ya kubeba watu kwenye malori wakati wa kampeni na kwenye uchaguzi ule "wakapiga mti" i mean wakaangukia pua kwa staili hiyohiyo ambayo walikuwa wanafanya kumfurahisha ndugu mgombea/mwenyekiti aonekane bado anapendwa!!
Waendelee tu, maana pia tumeaswa kutokuhangaika na sikio la kufa, pia tusimwamshe mlalaji!
Hii ni vita ya kukomboa nchi, ujinga wao faida kwetu.
 
waacheni hata mie mwaka 2005 nilikuwa advance pale Jamhuri wakaja kutulaghai tukapewa kadi za chama baada ya kufika UD tukapigishwa kunji la kwanza na ndo ikawa mwanzo na mwisho wa uteja wetu ...tukapata akili ya kukua, tukaanza harakati,mwaka wa kwanza nikachukua kadi ya Chama changu cha ukombozi CDM

namaanisha hao wanafunzi wanapelekwa tu ,pindi wakija mtaani na kuona life watakuja kuipigania nchi yao ndani ya chama cha ukombozi CDM
 
Jamani CHadema ijipange upya CCM imeanza vizuri kujipenyeza kwa jamii! Tusikae wa kuwa beza! Angalie mkutano wa Dr Slaa jana hata watu mia 400 hawafiki!
 
Ndugu wadau, gazeti la mwananchi la jana, 16/4/2011 lilikuwa na habari kuwa, yale majigambo ya ccm (nape) kuwa wamepokea wanachama 670 pale nyerere square dodoma kumbe walikuwa ni wanafunzi wa shule ya mbunge wa jimbo la dodoma inayoitwa central secondary school. Wanafunzi hao walipelewa ama bila kujua leo au kwa kulazimishwa. Ndiyo maana katika wale waliopokea kadi walikuwa ni watoto tu na mkubwa mmoja. Huenda ndiyo dalili za kuishiwa kwa chama hiki
CENTRAL SECONDARY haimilikiwi na Mh. Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini.Yeye anamiliki CITY SECONDARY.Kama ni Central basi itakuwa ni RA kawaleta kupunguza kasi ya wana CHE CHE MEA kumtimua
 
Ndugu wadau, gazeti la mwananchi la jana, 16/4/2011 lilikuwa na habari kuwa, yale majigambo ya ccm (nape) kuwa wamepokea wanachama 670 pale nyerere square dodoma kumbe walikuwa ni wanafunzi wa shule ya mbunge wa jimbo la dodoma inayoitwa central secondary school. Wanafunzi hao walipelewa ama bila kujua leo au kwa kulazimishwa. Ndiyo maana katika wale waliopokea kadi walikuwa ni watoto tu na mkubwa mmoja. Huenda ndiyo dalili za kuishiwa kwa chama hiki
Mallole mp wa dom shule anayomiliki inaitwa city na sio central. Hata kura za maoni ccm aliwatumia hao wanafunzi kupata nafasi ya kugombea ubunge.
 
hii nayo inaonyesha kuwa mambo yanazidi kuwakaba shingoni. ila kali niliyoiona ni ile ya mjadala wa katiba pale Karimjee ati saa 11 alfajiri viti vimeshajaa watoto tena wa chini ya miaka kumi alafu wakati mjadala unataka kuanza, watoto wote wakawa wamelala, ile kitu ilinipa picha ya ajabu kabisa, na sijui kama aliyepanga ule mpango atakuwa na akili za kibinadamu
 
Back
Top Bottom