CCM wanafanya maandamano Mwanza

CCM wanafanya maandamano Mwanza

Huu ni uonevu!kwa vyama vya upinzani
Kwanini wao ndy wafanye maandamano na mikutano!lakini wakifanya wapinzani wanakamatwa????Wazee wa lumumba naombeni majibu

Ova
 
Mida hii nipo maeneo ya Aga khan naskia makelele road kuangalia ni CCM wana andamana kelele zinapigwa

Hivi maandamano si yalipigwa marufuku nchi au nyie CCM na mwenyekiti wenu mnaona hii nchi ni Mali yenu pekee yenu hadi mnaleta ubaguzi?

Haiwezekani wengine wajiachie wengine wabanwa sio haki

f8dbc62d81bdbbe6081c500d33a0694d.jpg
Wenye nchi hao, wengine ni wahamiaji, hata mkitaka huduma za jamii kama maji na barabara mpaka mkuu akipenda, au la mbunge wenu ndio awapatie japokuwa yeye sio mkusanya kodi zenu.
 
Hata chizi ataelewa ni nini kinaendelea awamu hii!!
Mkuu ninakuunga mkono.........Hii inaonyesha kuwa ccm walishindwa kwenye uchaguzi wa 2015,,So kwa kupiga marufuku mikutano ya kisiasa ya hadhara na maandamano ililenga ccm kujiimarisha na kufanya maandalizi ya uchaguzi wa 2020.
Hebu angalia ziara za "mzalendo",,,,kila anapofika ni lazima atoe shukrani kwa wananchi wa eneo husika kwa kumpigia kura lkn washindani wake ni marufuku mpaka 2020.Hii maana yake ni kwamba,Itakapofika 2020 mzalendo ataonekana kwa wapigakura kuwa anafaa kwa sababu alishukuru kwa kura alizopata ktk uchaguzi wa 2015 na washindani wake hawakushukuru hivyo hawafai kuchaguliwa........Ni mawazo yangu tu
 
Nimecheka kama vile ni mazuri!
Kwahiyo ni watu tu imetokea wakajikuta pamoja halafu wamevaa nguo za njano na kijani wanakimbia tu barabarani wakishangilia?
kwani maandamano ni nini?
Maandamano ni kuvaa sare za chadema na kuingia uwanjani kutumia uhuru wa kuongea kwa kumkosoa Rais ambaye ni Mtukufu na hakosei....
 
Lissu hajakosea.
It is there turn bwana
 
Hebu tusome Ibara ya 13 (4) na (5): "Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
Kwa madhumuni ya ufafanuzi wa masharti ya ibara hii neno "Kubagua" maana yake ni kutimiza haja, haki au mahitaji mengineyo kwa watu mbalimbali kwa kuzingatia utaifa wao, kabila, pahala walipotokea, maoni yao ya kisiasa, rangi, dini, jinsia au hali yao ya maisha kwa namna ambayo watu wa aina fulani wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, isipokuwa kwamba neno "Kubagua" halitafafanuliwa kwa namna ambayo itazuia Serikali kuchukua hatua za makusudi zenye lengo la kurekebisha matatizo mahususi katika jamii.
Hivi viongozi wa awamu hii wanajitia hamnazo au? Mbona Katiba iko wazi kabisa kuhusu haki za kiraia na za kidemokrasia! Sasa wanapoamua kuwatendea Wapinzani kwa ubaguzi, wanachotaka hawa watawala ni nini hasa. Mimi sijaelewa. CCM kama Chama kinachoongoza nacho kwa uzezeta wa viongozi wake wanaona ni sawa wao kuandama kifua mbele kama majuha bila kutafakari kuwa kwa kufanya hivyo wanaleta ubaguzi katika katika nchi.
 
Mida hii nipo maeneo ya Aga khan naskia makelele road kuangalia ni CCM wana andamana kelele zinapigwa

Hivi maandamano si yalipigwa marufuku nchi au nyie CCM na mwenyekiti wenu mnaona hii nchi ni Mali yenu pekee yenu hadi mnaleta ubaguzi?

Haiwezekani wengine wajiachie wengine wabanwa sio haki

f8dbc62d81bdbbe6081c500d33a0694d.jpg
Tutawaruhusu mkiacha Upumbavu na Urofa
 
JPM mwenyewe hawezi kusimamia maneno yake nani sasa anaweza kumwamini tena labda hao wazee wa ndio kukubali kila kitu bila kuhoji
 
Back
Top Bottom