ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
Mimi ni mteja wa Vodacom (T)LTD. Mara kwa mara napokea matangazo ya promosheni ambayo yanatumwa na Voda au kupitia mifumo ya taarifa nilizojisajili rasmi kama "Clouds Kwanza" nk.
Imeniaribia mudi yangu saaana, nimesikitika sana, nimehuzunika sana na nimekereka sanaaaa kupokea ujumbe huu wa "Kutoa ni moyo unaweza! kuchangia CCM kwa kutuma neno CC Kwenda namba 15377........!. Nichangie CCM, eti CCM ambayo haikuwahi hata siku moja kutumia utaratibu huo kuhamasisha kuchangia maendeleo ya wananchi masikini huko vijijini, leo inataka tena kura!.
Cha ajabu huu ujumbe umetumwa na kampuni ya "PUSH MOBILE" ambayo hata sijawahi kuisikia masikioni mwangu kabisa na sijui ipo wapi na imepataje namba yangu ya simu na inanufaikaje na zoezi hili.
Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa, achia mbali CCM ambayo ni Serikali na nilidhani ndio ilipaswa ihakikishe taarifa zangu binafsi kama namba ya simu zinatumika kwa ridhaa yangu lakini inaonekana imehusika kukihuka hilo kwa lengo la kujinufahisha.
Kama utaratibu wa makampuni ya simu sasa upo hivi wa kutoa taarifa za wateja pasipo ridhaa ya mteja husika, kwa nini tusiamini kuwa haya makampuni ya simu yanatumia kinyume cha taratibu taarifa zetu binafsi?. Na kama ndio voda imetoa namba yangu kwa huyo mdudu "PUSH MOBILE" or CCM, je hakuna uwezekano wa kunikata fedha juu kwa juu hata nisipochangia kama sms inavyotaka??..
Nimekereka sana na jambo hili la kutuanika wateja.