nitonye
JF-Expert Member
- Dec 18, 2011
- 7,349
- 3,908
Kipindi kirefu serikali ya CCM imekuwa ikituhumiwa kulinda mafisadi pamoja na kelele zote kutoka kwa wapinzani. Sasa mwaka huu umekuwa wimbo wao hadi kuahidi kuwaundia mahakama ya mafisadi kana kwamba mahakama zetu hazina ubavu wa kuwahukumu wala rushwa. Napata mashaka wanaposema mafisadi wameanza kukimbia ccm najiuliza wameenda wapi na ni akina nani? Ufisadi wao ni upi kwa hao waliokimbia wamekwapua kiasi gani serikalini, na imekuwaje wanawaacha mafisadi wanakimbia bila kukamatwa na vyombo vya dola je wamekimbia nchi au bado wapo?