TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
WanaCCM wanaounga mkono jitihada za kuijenga na kuiimarisha CCM wanatakiwa kujua na kutambua kuwa majimbo ya Kinondoni na Siha yalikuwa upinzani, siyo mara ya kwanza chama cha siasa kumsimamisha mgombea aliyetoka chama kingine cha siasa, Duni Haji, Lembeli, Ester Bulaya na wengineo wote walisimamishwa kugombea nafasi mbalimbali katika vyama vyao kwa mujibu wa katiba ya vyama vyao, sheria ya uchaguzi na kanuni zake, pamoja na kukidhi misingi ya kidemokrasi
Kuna mwingine mpaka alitaka kupewa urais wa nchi hii akiwa na siku moja tu ndani ya chama, halikuwa kosa hata kidogo maana katiba ya nchi, sheria ya uchaguzi, kanuni za uchaguzi na hata katiba za vyama husika ziliruhusu na zinaruhusu mpaka leo.
Majimbo yote mawili ya Kinondoni na Siha yalikuwa upinzani, kutokana na heshima kubwa ambayo chama cha mapinduzi kimejijengea baada ya jitihada zake za kujisahihisha na kujirekebisha kutokana na makosa ya nyuma, ni dhahiri kuwa CCM itashinda majimbo hayo maana wananchi wanaitambua kazi kubwa inayofanywa na Magufuli na serikali yake ya CCM ya awamu 5 ktk kuwaletea wananchi maendeleo na kupambana na ufisadi uliotapakaa kila kona