CCM wajiandae kumlipa Tundu Lissu millioni 76

Chacha Willy

Senior Member
Joined
Mar 30, 2014
Posts
103
Reaction score
36
Kesi ya Lissu hukumu Septemba 30 Kesi ya madai ya gharama za uchaguzi anayodai Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu(chadema), inatarajiwa kutolewa hukumu Septemba 30 mwaka huu. Katika kesi hiyo namba 11 ya 2013, Lissu anadai gharama za uchaguzi za uendeshaji kesi katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani ambazo alishinda na kubaki na ubunge wake.

Lissu anadai Sh. milioni 79 ikiwa ni gharama za kesi ya uchaguzi aliyofunguliwa na Shaban Selema na Paschal Halu waliopinga ushindi wa ubunge wake. Baada ya kushinda kesi ya ubunge, Lissu aliiomba mahakama aweze kulipwa fedha hizo. Kesi hiyo ilisikilizwa Jana mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Dodoma, Rutatinisigwa, huku mdaiwa wa pili, Halu akiwakilishwa na wakili wa utetezi Geofrey Wasonga ambaye anapinga madai hayo na kusema njia iliyotumika si sahihi kulingana na viambatanisho vilivyowasilishwa mahakamani kughushiwa.

Hali hiyo ilimlazimu Lissu kumuomba Msajili kumueleza Wasonga kuongeza kitu kipya kutokana na hoja zake kujibishana kwa maandishi kama walivyoelekezwa na mahakama.
 
CCM italiangamiza taifa kwa uroho wa madaraka hata ilipowekewa HAPANA watalazimisha ili iwe NDIYO.
 
- Labda ailipe familia ya MWalimu kwa kumtukana Baba wa Taifa tena marehemu bila ya kosa, ok!!

Le Mutuz
 
Mpeleke mahakamani basi

- Si katangulia mwenyewe Sheria hajui Zitto kampiga mahakamani, Rais kamtwanga kama mtoto aibu tupu labda atulipe Taifa kwa kumtukana Baba wa Taifa tena maskini ya Mungu marehemu bila sababu ya msingi U know

Le Mutuz
 
Huyu mzee hajawahi kuwa na point hata siku moja. Wenzake wakizeeka huwa na Busara lakini kwa huyu mwenzetu ni kinyume chake.

- Busara ya kumtukana baba wa taifa sina upo sawa maana sijawahi kuona mtumzima na akili timamu anatukana Marehemu ambaye hawezi kujibu,

Le Mutuz
 
- Si katangulia mwenyewe Sheria hajui Zitto kampiga mahakamani, Rais kamtwanga kama mtoto aibu tupu labda atulipe Taifa kwa kumtukana Baba wa Taifa tena maskini ya Mungu marehemu bila sababu ya msingi U know Le Mutuz
Kazi kweli kweli! Hivi hii topic inamhusu Nyerere?
 
Back
Top Bottom