CCM waingia mitini, kesi ya Lissu yasimama

Kila Mtanzania mwenye akili timamu kwa sasa anajua kabisa nini kinachoendelea KUHUSU KESI BANDIA ZILIZOFUNGULIWA NA WANA-CCM dhidi ya Wabunge wa Upinzani hususani wa CHADEMA. Tumeona kilichotokea Arusha juzi baada ya Jaji kutoa hukumu yenye kuacha shaka kubwa na kudhihirika kuwa HUKUMU HIYO ILIKUWA NA MAELEKEZO TOKA JUU!!

Mpaka sasa kesi za Wabunge wa CHADEMA zilizoko Mahakamani ni:

  1. Jimbo la Arusha Mjini kwa Mhe. G.Lema ambaye tayari amevuliwa Ubunge.
  2. Jimbo la Singida Mash kwa Mhe.Tundu Lissu bado iko Mahakamani.
  3. Jimbo la Ubungo kwa Mhe.J.Mnyika bado iko Mahakamani.
  4. Jimbo la Meatu kwa Mhe. Opulukwa, Meshack Jeremiah bado iko Mahakamani.

Kuna habari za kuaminika kuwa kuna kesi nyingi zitafunguliwa dhidi ya Wabunge wa CHADEMA ili tu kuwafanya wawe busy all the time na wa sipate muda wa kuwatumikia Watanzania na wasiweze kupanga mikakati ya kuibana Serikali ya Majambazi Bungeni na nje ya bunge. Huo ndo mpango uliopo. Bado kuna kesi hii ya Arusha dhidi ya Viongozi wa CDM kwa tuhuma za Maandamano bila kibali. Wamo Dr. Slaa,Mhe. Mbowe,Mhe.Ndesamburo na wengineo.

CHADEMA kaeni macho na hao wahuni wa CCM wanaotaka kuwapotezea muda wenu Mahakamani na mwisho wa sikuu muonekana kuwa mlishindwa kuwahudumia Watanzania.


Tunaweza kuchambua pumba na mchele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom