CCM wafarijiana kwa kushindwa na CHADEMA

CCM wafarijiana kwa kushindwa na CHADEMA

Waziri wa maendeleo, jinsia na watoto bi Sofia Simba leo akiwa ziarani wilaya ya Mwanga amekiri kuwa mtiti wa CHADEMA hata wao kama wajumbe wa kamati kuu unawatia wehu.

amesema hata hii mwanga mnayosema ipo salama kwa ccm sio kweli kwani haipo kwani siasa za wanaccm wa mwanga za makundi wanataarifa nazo na pia ziara za kimya kimya za viongozi wa CHADEMA na damage ambayo wameshafanya hasa kwa wazee na vijana wanaijua.

Amesema kuwa CHADEMA wameanza kuukwepa mtego wa polisi na wanafanikiwa akifananisha na matukio ya kupigwa wanaCHADEMA kwenye uchaguzi wa Udiwani Arusha na wao kukaa kimya! " hii ni dhahiri kabisa kuwa mchezo kidogo tu wa kuzembea ni mauti kwetu kama hapa tulivyokuwa tunapategemea pameharibiwa kiasi hiki hamdhani kuwa 2015 mkoa wote tutakuwa wapinzani? alisema Same mashariki CCM hoi, Magharibi CCM hoi Mwanga nayo ndo hivyo tena mtakuwa wageni wa nani? Mwenyekiti ?" alihoji Waziri Simba wakati akiongea na kamati ya Utekelezaji na Baraza la UWT leo ndani ya Ukumbi CCM !

Hii ni kazi njema ya kamanda Anorld Kileo aliofanya kipindi cha mwezi April na May mwaka huu iliyosababisha kungoa mwenyekiti mmoja wa UWT kata.

Hivi huyu Mama alishamaliza Bifu lake na Anne Kilango?
Manake hata yeye ni miongoni mwa Nguli waanzilishi wa siasa za Makundi ndani ya CCM..
 
we hujaelewa tu. sophia simba amezungumza kutokana na uzoefu wa wizara yake. kuna malalamiko mengi ya viongozi na wabunge wa chadema kupora wake za watu. pia chadema wanasababisha mimba nyingi za uchochoroni na watoto wa mitaani kutokana na kuzalisha mimba nyingi zisizotarajiwa
mkuu kuna mimba zisizotarajiwa, kivip?
 
wapare na wachaga ni dugu moja. hivyo usijivunie sana. nenda kwa wamakonde kama we unajifanya unaweza kushawishi sana
mkuu wamekonda tayari ni cdm, si unaona wanavyokamaa na gesi yao? Maccm wasubiri kichapo mwaka 2015 maeneo ya kusini...
 
Kuwa punguani ni majaliwa ya mwenyezi mungu, lakini kuiunga mkono ccm ni upunguani binafsi.
 
Ni hatari kama hiyo mikutano iliyopigwa weekend iliyopita lazima uchanganyikiwe....hawajuai hata wajmjibu nanai....huku lema ..huku mbowe...huku lisu....huku mnyika...huku mawazo...huku ..kila maahali watu wanapachimba...ni bala kwa CCM sasa hivi....polisi inabidi waandae makontena ya kuweka barua za kuomba vibali vya mikutano...haina jinsi tena...
 
CCM imeshazikwa tayari
kilichobaki ni matanga yake 2015
hata wafanyaje kuiba kura 2015 wajisahau
na kuhonga kama jadi yao wananchi wanasubiri hela za bure
lakini kura kwa chadema..
wapare msidangayike na CCM iliowanyima maendeleo
 
ccm isiyohofia upinzani ni ccm iliyobweteka,lazima kama chama tawala kikubaliane na mazingira ya sasa ili kupata mwarubaini
 
we hujaelewa tu. sophia simba amezungumza kutokana na uzoefu wa wizara yake. kuna malalamiko mengi ya viongozi na wabunge wa chadema kupora wake za watu. pia chadema wanasababisha mimba nyingi za uchochoroni na watoto wa mitaani kutokana na kuzalisha mimba nyingi zisizotarajiwa

Punguani we! Msxxcc mazako anaongea majanga yanayowakumba...unatema pumba. Kama ana kesi za ivo chama lenu ndo linaongozo. Ovyo kabisa...mbuzi we
 
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sophia Simba, amewataka wanachama wa chama hicho wasivunjike moyo kwa kupoteza viti vya udiwani katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni.Simba ambaye pia Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto, aliyasema hayo juzi katika ziara yake wilayani Babati ambapo ameambatana na Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Amina Makilag.

Katika uchaguzi huo, ambapo aliongea na viongozi wa ngazi ya mkoa na wilaya katika ofisi ya Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara na baadaye aliongea na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Old-Majengo mjini Babati.Katika uchaguzi huo CCM ilishindwa katika kata mbili za Bashnet iliyopo Babati Vijijini na Dongobeshi Wilaya Mbulu, ambapo CHADEMA iliibuka mshindi.

"Poleni kwa kushindwa kwani ilituuma sana, kwa kushindwa kule tunapigiwa kengele tusicheze kabisa ingawa sote tunajua chaguzi ndogo watu hawaendi kupiga kura sisi hilo linaweza likatuathiri pia na hali iliyotokea mkoani Arusha," alisema na kuongeza;"Ndugu zangu tusifanye mambo yetu gizani tutakuwa hatukitetei chama chetu, tutakwenda na maji."

Alisema pamoja na kujitahidi kufanya kampeni nyingi lakini walishindwa katika uchaguzi huo mdogo na badala yake kata kuangukia CHADEMA.Alisema hiyo ni dalili mbaya, hivyo wana-CCM wanatakiwa kujipanga upya ili kuondoa hali hiyo.

"Lazima tuwe na watu wetu ndani mwao ikiwezekana tuwalipe kwani wao wana watu wao ndio maana wanajua mbinu zetu,"alisemaAliwataka viongozi kuhakikisha wanakuwa karibu na wanachama ili ule unyonge uliosababishwa na vuguvugu la chaguzi ndogo uondoke, kwani wana-CCM hawajui kujibu mapigo bali hujipanga kuhakikisha pale walipokosea wanajirekebisha.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UWT Taifa, Makilagi, alisema mara nyingi wanawake wamekuwa wakishindwa kujiamani na uwoga unachangia kushindwa kutekeleza wajibu wao katika nafasi zao za uongozi.

Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Manyara, Salome Luhinguranya, alisema ziara ya waziri inawezekana ikaleta mabadiliko na chachu katika mkoa huo ambao unaendelea kutekwa na wimbi la upinzani. Alisema ni wazi wapinzani wame j i a n d a a k u h a k i k i s h a wanashinda kwa nguvu


Source: NIPASHE -21 Jul 2013 | Na Jamillah Daffo, babati
 
Mbona babu kijana W. Malecela anasema amezunguka Kilimanjaro nzima na kuona ccm bado imara?

Ndio kusema ccm hawajui wako wapi kichama na wanaelekea wapi?
Habari inayoendelea mujini wanayo sana tu...wanajifanya jeuri in public view but am telling you currently they do experience the so called sleepless nights...chezea cdm
 
524363_10151402560413581_400931884_n.jpg

hii inaitwa bila kuremba. Natamani tungekuwa tunatawaliwa kijeshi tungeishi katika true colors
 
Walisema chadema ni chama cha msimu haya sasa mziki wake wanaushindwa.
 
Hoja zingine ni kama maji machafu tungeni uongo wote mwisho wa siku mtasema tu ukweli.
 
Kwa hiyo amegundua kuwa nguvu ya Taarabu mwisho wake Chalinze siyo !
 
Back
Top Bottom