Wachumi wa Tanzania,mamlaka ya TRA,wanashindwa kufahamu umuhimu wa uzukaji wa Pesa wao wanachokifiria ni kupandisha kodi ndio ukuwaji wa uchumi na mapato,kila siku tunasikia kodi za maajabu zinawekwa sehemu tafauti kuanzia bandarini,Utalii nk
Kupandishwa huko kwa kodi za maajabu zimefanya biashara nyingi kufungwa, watalii wamepungua kuja Tanzania ,haya yote wanaifanya Tanzania kukosa mamilioni ya mapato.
Mambo yote hayo bado utasikia wachumi wetu bado wakiema "kama watu hawawezi kulipa wafungiwe au waondoke tu au hatuwezi kukosa watalii watakuja tu,tunataka watalii wenye hadhi...bla bla bla"
Ushauri wangu serikali ipunguze kodi zinazowaumiza wananchi,kufanya hivo itawasaidia watanzania kuweza kunufaika katika biashara zao,kwani watanzania wakizidi kufungua biashara serikali itazidi kukusanya kodi,mizigo itazidi kumiminika bandarini...
Kinachoendelea hivi sasa hakuna mzunguko kila kitu kimekwama.,muuza vitumbua hawezi kuuza vitumbua hakuna mnunuzi,Nyumba za wageni hakuna wa kulala,Baa zimefungwa hakuna mywaji kwa sheria za kipuuzi...nk
Sasa serikali ifikirie kama sekta zote hizo zitafungwa ua wataamua kupunguza wafanyakazi,mtanzania wa maisha ya chini atafanya nini,vipi watanzania watalisha familia zao...
kama hali itaendelea hivi tusubiri makubwa,,, "This is the begining of the end".....
Serikali ifikirie kuwawezesha raia wake sio kuwaadhibu kwa visasi nakejeli,ikifanya hivyo tutafika tunapotaka kwenda....