CCM waanza kumgeuka Rais Magufuli

CCM waanza kumgeuka Rais Magufuli

HALI mbaya ya uchumi inaanza kuwaweka pamoja wabunge wa Tanzania, tayari wameanza kumshughulikia Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.
Ilikuwa minong’ono kwa mbunge mmoja mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulalamikia namna uchumi wa nchi unavyoyumba miezi michache tangu Rais Magufuli kuingia madarakani, sasa wanaanza kujitokeza na kuungana na wabunge wa upinzani.

Goodluck Milingwa, Mbunge wa Ulanga Mashariki amevunja ukimwa ndani ya ukunbi wabunge jana na kuanza kunyooshea kidole utawala wa Rais Magufuli kwamba, wananchi wanatopea kwenye umasikini.
“Hali ya maisha ni ngumu sana, namuomba Muheshimiwa Rais hapo aliposhika kwa sababu si mahali pake, hali imekuwa ngumu sana,” amesema Milingwa akilalamikia umasikini unaokuwa kwa kasi chini ya utawala wa Rais Magufuli.

Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Taarifa ya Mwaka 2016. Muswada huo uliwasilishwa juzi na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria.
Kauli hizo zilikuwa zikitolewa na wabunge ama wadau wa vyama vya upinzani, taasisi na wasomi mbalimbali nchini.

Milingwa anaungana na mailioni ya Watanzania wanaolalamikia maisha kuwa magumu zaidi kuliko wakati wa Utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Jakaya Kikwete. Ugumu wa maisha sasa unatambuliwa rasmi na Rais Magufuli ambapo hivi karibuni alidai kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuchangia hali hiyo kutokana na kutoa fedha zao benki na kukaa nazo majumbani wao.

Mtikisiko wa uchumi nchini upo dhahiri ambapo juzi Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo alinukuu taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikionesha namna wananchi wanavyotopea kwenye umasikini katika uongozi wa Rais Magufuli.

Kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya kiuchumi miezi michache Rais Magufuli kuingia madarakani, baadhi ya hoteli nchini zimefungwa.
Pia wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam wamehamisha mizigo yao na kutumia bandari zingine, madereva wa malori wakiachwa bila kazi huku kiasi kikubwa cha fedha zinazotokana na kodi zikipotea.

Katika taarifa ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyoinukuu kutoka BoT na baadaye kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ameeleza;

a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba – Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari – Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%.

Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita.

Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakanic) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.d)

Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula
Sasa wewe kinakuuma nini? We shughulika na chama chako cha mafisadi.
 
cha kufanya ni kukaa na wadau na serikali yani wafanyabiashara, wizara ya fedha na mipango, BOT, ili zile Treasury bills zirudishwe kwenye mabenki binafsi ili zirudi kwenye mzunguko kama zamana ya serikali kwa wananchi wake uku serikali ikiweka mipango mizuri ya ulipaji kodi. pia ongezeko la VAT liangaliwe kwa kina. bandari hii ni rasilimali hisiyoisha yani renewable property. na hapa unaweza kupata faida kwa kupunguza kodi ukaongeza mizigo ya kutosha ukapata hela zaidi ya sales maximuzation by increasing volume of cargo.
 
Mahali tulipofikia sasa sio pazuri kiuchumi sasa sijua maskini ananufaika vp yeye anawabana matajili na matajili wanatubana sisi apa Kama Wana komaana ila tunaumia sisi
 
He! Leo hii mmeanza kumkubali huyo Mlinga? Kwa nini sasa hamkumuelewa wakati ule?
Nani amemkubali Mlinga, au tunatofautiana kuelewa kilichoandikwa? Nani alikwambia mtu mwongo huwa hawezi kusema ukweli hata mara moja? Je, inamaanisha muongo akisema ukweli sifa yake ya kuwa muongo inaondoka?
 
Ila ccm hawaamiki wakipata posho siku mbili to wanasahau yote ya mtaan inakua ndiyoooooooo!!!!!!!!
 
MIE NADHANI WATU WASHAURI NINI KIFANYIKE AMBACHO NI PRACTICAL. MIMI KWA NIABA YA WANAUKAWA NINIAPENDEKA MH RAIS AFANYE KAMA KIKWETE YA KUWAACHIA WAFANYA BIASHARA WAPITISHE MIZIGO BANDALINI BILA KULPIA USHAURU..KWANI HILI LITASAIDIA MIZIGO MINGI KUPITA LAKINI WAKATU HUOHUO SISI WENYE BIAHSRA YA MALORI NA MENGINEO IPITE KILAHISI HIVYO KUCHANGAMSHA UCHUMI.NINAELEWA HATUA HII ITAPUNGUZA UWEZO WA SERIKALI KIFEDHA LAKINI AKINAFANYA HATA SISI UKAWA TUTAACHA KUMSHAMBULIA
Sasa ni wazi wewe wala si muwakilishi wa ukawa ila ni MCHOCHEZI.
 
Ukitaka kutawala vizuri tz ruka angani nchi nzima uone ... Tembelea watu na taasisi... Sikiliza watu.... Sasa rudi ofisini chukua katiba uisome vizuri. Soma yaliyofanywa na wenzako. Angalia kwigineko duniani. Tafakakari na chukua hatua. Utagundua kuwa unamhitaji kila MTU kila MTU kila MTU! Ili utawale vema!
 
Nikisoma comment zako huwa nacheeka! JF imeingiliwa miaka hii! Hivi unakua uko serious? Umevaa nguo zako afu unaandika vitu unavyofikili ni point kuiwasilisha kwenye jamii?

Ulisomaga kweli mkuu? Hapa JF nadhani hoja ndio bora kuliko vioja! Sijui kama utaelewa!
elimu....elimu.....elimuu
 
Back
Top Bottom