CCM waanza kumgeuka Rais Magufuli

CCM waanza kumgeuka Rais Magufuli

MIE NADHANI WATU WASHAURI NINI KIFANYIKE AMBACHO NI PRACTICAL. MIMI KWA NIABA YA WANAUKAWA NINIAPENDEKA MH RAIS AFANYE KAMA KIKWETE YA KUWAACHIA WAFANYA BIASHARA WAPITISHE MIZIGO BANDALINI BILA KULPIA USHAURU..KWANI HILI LITASAIDIA MIZIGO MINGI KUPITA LAKINI WAKATU HUOHUO SISI WENYE BIAHSRA YA MALORI NA MENGINEO IPITE KILAHISI HIVYO KUCHANGAMSHA UCHUMI.NINAELEWA HATUA HII ITAPUNGUZA UWEZO WA SERIKALI KIFEDHA LAKINI AKINAFANYA HATA SISI UKAWA TUTAACHA KUMSHAMBULIA
Umetumwa?
 
Siwamini wana CCM wa aina yoyote ile waende huko wanafiki hao wanakula posho tu hawajui huku kitaa hawajui kukoje
 
HALI mbaya ya uchumi inaanza kuwaweka pamoja wabunge wa Tanzania, tayari wameanza kumshughulikia Rais John Magufuli, anaandika Faki Sosi.
Ilikuwa minong’ono kwa mbunge mmoja mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulalamikia namna uchumi wa nchi unavyoyumba miezi michache tangu Rais Magufuli kuingia madarakani, sasa wanaanza kujitokeza na kuungana na wabunge wa upinzani.

Goodluck Milingwa, Mbunge wa Ulanga Mashariki amevunja ukimwa ndani ya ukunbi wabunge jana na kuanza kunyooshea kidole utawala wa Rais Magufuli kwamba, wananchi wanatopea kwenye umasikini.
“Hali ya maisha ni ngumu sana, namuomba Muheshimiwa Rais hapo aliposhika kwa sababu si mahali pake, hali imekuwa ngumu sana,” amesema Milingwa akilalamikia umasikini unaokuwa kwa kasi chini ya utawala wa Rais Magufuli.

Alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia Muswada wa Sheria ya Taarifa ya Mwaka 2016. Muswada huo uliwasilishwa juzi na Dk. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Katiba na Sheria.
Kauli hizo zilikuwa zikitolewa na wabunge ama wadau wa vyama vya upinzani, taasisi na wasomi mbalimbali nchini.

Milingwa anaungana na mailioni ya Watanzania wanaolalamikia maisha kuwa magumu zaidi kuliko wakati wa Utawala wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Jakaya Kikwete. Ugumu wa maisha sasa unatambuliwa rasmi na Rais Magufuli ambapo hivi karibuni alidai kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara kuchangia hali hiyo kutokana na kutoa fedha zao benki na kukaa nazo majumbani wao.

Mtikisiko wa uchumi nchini upo dhahiri ambapo juzi Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo alinukuu taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikionesha namna wananchi wanavyotopea kwenye umasikini katika uongozi wa Rais Magufuli.

Kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya kiuchumi miezi michache Rais Magufuli kuingia madarakani, baadhi ya hoteli nchini zimefungwa.
Pia wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam wamehamisha mizigo yao na kutumia bandari zingine, madereva wa malori wakiachwa bila kazi huku kiasi kikubwa cha fedha zinazotokana na kodi zikipotea.

Katika taarifa ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini aliyoinukuu kutoka BoT na baadaye kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ameeleza;

a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba – Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari – Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%.

Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita.

Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakanic) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.d)

Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula
Wewe umesema wabunge wa ccm, sasa si ungesema mbunge wa ccm? Porojo tu unaleta hapa
 
Hivi Mbowe lile deni la Bilicanas ameshalilipa?
Alipe wap si mliona sifa kumtoa deni ndo lishapotea 1bilion na ushee. Tafuten pa kufidia, watu wanafikiri unapomharass mtu kwenye media ndo atalipa kodi. Au ndo atatetereka
 
Hali kama hii ni ya kawaida sana hasa ukiangalia ilikuwa tumekabiliwa na uchaguzi mkuu. Kushuka huku kwa muda inawza kuwa imetokana:-
1. Matumizi makubwa yaliotumika katika kipindi hicho kuyakabili "mashughuliko" ya uchaguzi
2. Hofu ya wafanya biasharana kuchukua tahadhari na hivyo shughuli kubwa za kibiashara husimama au kudorora.Hali hii itatengemaa siku chache zijazo.
Kwahiyo unasema ccm salichukua hela wakatumia kwenye uchaguzi mkuu maana walikuwa wamezidiwa?
 
Kama uchumi maana yake ni watu kuishi kama nyumbu mbugani au swala,basi Magu waachie watu waibe ili uchumi ukue. Ukizoea kuishi kijanja janja ujue ipo siku utaona cha moto...
 
Alipe wap si mliona sifa kumtoa deni ndo lishapotea 1bilion na ushee. Tafuten pa kufidia, watu wanafikiri unapomharass mtu kwenye media ndo atalipa kodi. Au ndo atatetereka
Kwa sababu ana daiwa kuna namna itafanyika ili alipe..
 
Bandarini mizigo imepungua na wafanyabiashara wamekimbia bandari yetu...sasa tushauri tufanye nini?

Naona ili madereva wa malori waendelee kupata kazi Serikali iwaachie wafanyabiashara wapite bila kulipa kodi bandarini...ili uchumi ukue na sie mama ntilie huku mitaani tuonje mema ya Serikali yetu...

Hii itafanya UKAWA wafurahi na kuipenda Serikali yetu. Pia Serikali iache kuwabana mafisadi ili hayo mafisadi yalete pesa mtaani yajenge majumba na sie mafundi ujenzi tupate kuonja mema ya duniani...kuyaacha mafisadi kutafanya UKAWA waiunge mkono Serikali...

Serikali iache kuwabana watumishi wake ili wafanye kazi wanavyotaka na kwa uhuru na wapeane maposho ambayo yatasaidia kukuza uchumi mitaani. Maana mitaani pesa imeadimika. Watumishi hao wazembe wakiachwa wataipenda Serikali na Rais wetu mpendwa..
Hivi ni nani ambaye ameshabikia ukwepaji kodi? Hili ndio tatizo letu siku hizi. Mtu akikosoa jinsi mambo yalivyo sasa anaitwa mkwepa kodi...au fisadi...au vyote viwili. Tunachosema ni hiki:

1. Ondoa vat kwenye mizigo ya transit. Hakuna bandari duniani (ninayojua) ambayo inafanya ujinga huo. Matokeo yake imekua ghali zaidi kwa wafanyabiashara kupitisha cargo yao dar. Kumbuka wafanyabiashara hao wanaenda kulipa kodi kwenye nchi zao. Sasa TRA wanasema eti hawatozi mizigo...wanatoza ancillary services...lakini hao wanaotoa hizo services wanachofanya ni kuongeza bei zao...so shida iko pale pale.

2. Ushuru wa forodha kwa mizigo ya ndani uangaliwe upya. Kwa mfano.. mimi gari yangu nilinunua kwa $8000 CIF. Ikafika hapa TRA wakanichapa kodi ya $10000. Yani kodi inazidi thamani ya gari. Ukowapi usawa hapa?

Tukisharekebisha hayo. Sasa tuhimize watu walipe hizo kodi...na watalipa tu!
 
uchumi tetele ndio habari ya mjini , kila siku afadhali ya jana., sasa hivi tulikuwa na mlo mmoja sasa nusu mlo.
 
Kama uchumi maana yake ni watu kuishi kama nyumbu mbugani au swala,basi Magu waachie watu waibe ili uchumi ukue. Ukizoea kuishi kijanja janja ujue ipo siku utaona cha moto...
Nakubaliana na yule aliyesema uvccm mkishindwa hoja pona yenu ni matusi
 
CCM WANAJUTA KWANINI WALIMPENDEKEZA KUWANIA URAISI
 
Huyu Mlinga ni moja kati ya walikokuwa na mazoea ya kupaya pesa kiujanja janja.... Tuendelea kufanya upembuzi yakinifu kuwafanya malaika waishi kama mashetani..
 
Back
Top Bottom