CCM v/s CHADEMA against ACT Wazalendo

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
747
1,000
Kinachoonekana sasa ni kwa CCM kuitumia nafasi ya ACT Wazalendo kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa huko nchini Zanzibar ,CCM kwa kutumia sura mbalimbali inazojivalisha inaonekana inatumia wanachama wake na wa ndani wa vyama husika kutaka kujenga hoja na kuleta fitina ndani ya vyama vya ACT na CHADEMA.

Hizi fitina tuwatake viongozi wetu wasizipe nafasi kupenya na kuingia waanze kuzivunja na mapema kabla hazijaota mizizi ili zisifanikiwe kuuvuruga upinzani unaoonekana kuwa na nguvu zinazoimarika kila siku zinaposonga mbele.

Covid 19 vile vimelea kumi na tisa visivyo na haya na kujipelekesha kiajabu ajabu halafu vikaapishwa kimazingara ,CHADEMA wameshafanya lockdown na kufanya sanitization na sasa CHADEMA ipo salama na vimelea vile,kwa maana wameshafukuzwa uwanachama hili ni suala la kichama na zaid kwamba chama hakihusika na kuwateuwa ,hio ni tofauti kubwa sana ambayo haihusiani kwa aina yeyote ile na ile ya ACT Wazalendo wala hapana ufananisho wala kigezo. Na kubwa ACT wamekiri mchana kweupe kuwa msimamo au msimamo yao kuhusiana na uchaguzi ipo palepale.

CCM wabaya sana.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
27,053
2,000
Huwezi kusema nguruwe haramu lakini mchuzi wake hauna shida. ACT wamekosea kuungana na wale wadhalimu
 
MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,759
2,000
CHADEMA wanadai hawautambui Uchaguzi Mkuu 2020 lakini wanachukua ruzuku za serikali zinazotokana na Uchaguzi Mkuu 2020!

Baada ya muda hata wabunge wa viti maalum watapeleka bungeni hata kama sio kina Halima Mdee na kundi lake!

CHADEMA wananikumbusha ule mwaka ambao Mbowe alikataa kupewa gari la KUB eti halina manufaa lakini baada ya wiki akaenda kuchukua kimya kimya!

Kama umewekeza ''mayai yako yote'' kwa wanasiasa wa CHADEMA kwa kuamini maneno yao, anza kujiandaa kupata mshituko!
 
herman joshua

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
1,124
2,000
N kama cjaelewa pahali.
N kwamba ACT hawakumteua Maalim katika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa...?🚮
🚶🚶🚶🚶
 
Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
747
1,000
Miccm mtakuwa mbioni sana kutaka kuingiza fitina ndani ya vyama hivi, hoja mnazojenga ni muflisi na hazina mashiko ,mnapokuwa kwenye mechi probabilty ya kuumizwa ipo,ya kuvujika ipo ya kufa ipo na hata ya refa kupendelea nayo ipo na timu ya mpira hio inayopata masaibu hayo haivunjwi,haivurugiki na inaendelea kuwepo.

Tume kama refa na mlolongo mzima wa wasimamizi wa uchaguzi labda tuwaite malinesman,makamisaa wamechezesha au waliochezesha uchaguzi huu wamesababisha watu,kuumizwa,kuvunjika miguu na kuuwawa kama haitoshi na upendeleo .

sasa mnapozuka wazushi kutaka kuingiza fitna eti wale wameumizwa,wengine wamekufa na waliobaki ambao walikuwa mstari wa mbele wameingia kwenye timu ya Taifa na sasa wanakula raha ,mtakuwa hamjielewi au mnajua kila kitu kitu ila lengo lenu ni kuingiza fitina ili vyama visifahamiane na nyinyi kujitengenezea mazingira mazuri zaidi,

Mlifanikiwa kuia TLP,CUF na sasa mnaiandama CHADEMA ,eneo mlilopo CCM kwa sasa ni kujaribu kutenganisha vyama hivi viwili vya ACT na CHADEMA,ili uzidi urahisi wa kuteketeza upinzani.

Ninachokifurahia ni kauli za viongozi wa upinzani kukoromea kuwa mbali ya yote ya kuingia kwenye timu ya Taifa bado hawautambui uchaguzi uliopita.
Weka mbali probability za wanajeshi kwenda vitani seuze chama cha siasa kupambana na chama fisadi.

CCM wabaya sana,waharibifu.
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,154
2,000
Huwezi kusema nguruwe haramu lakini mchuzi wake hauna shida. ACT wamekosea kuungana na wale wadhalimu
Mbona 2015 waliunywa mchuzi wa Lowassa bila shida ambaye nae hapo kabla walimtambua kama nguruwe? Kuna wakati unaangali faida na hasara za kuamua kufanya jambo au kuacha kufanya.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,532
2,000
CHADEMA wanadai hawautambui Uchaguzi Mkuu 2020 lakini wanachukua ruzuku za serikali zinazotokana na Uchaguzi Mkuu 2020!

Baada ya muda hata wabunge wa viti maalum watapeleka bungeni hata kama sio kina Halima Mdee na kundi lake!

CHADEMA wananikumbusha ule mwaka ambao Mbowe alikataa kupewa gari la KUB eti halina manufaa lakini baada ya wiki akaenda kuchukua kimya kimya!

Kama umewekeza ''mayai yako yote'' kwa wanasiasa wa CHADEMA kwa kuamini maneno yao, anza kujiandaa kupata mshituko!
Kila wakati ume-stuck mind yako kwa kukumbatia hoja ya ruzuku ili kuhalalisha Chadema wanakosea, kwani Chadema kuchukua hiyo ruzuku siyo haki yao? na Chadema wakiamua kutopeleka wabunge bungeni sio haki yao?

Nakuona kila mara unahangaika kuwapangia Chadema nini wafanye, wao kama chama ndio wanaamua wafanye nini, wakati gani, na kwa madhumuni gani, sio wewe kibaraka mlamba visigino wa jiwe.

Tena ukumbuke pesa ya ruzuku siyo ya CCM au ya jiwe kama unavyodhani, ni pesa za walipa kodi wa Tanzania, hivyo nikushauri utafute propaganda nyingine ya kitoto uje nayo hapa, sio kila siku unarudia hii moja tu.

Hapa najua utajaribu kujenga hoja nyingine dhaifu kuwa Chadema wana hali ngumu kiuchumi, ukweli uchumi wa nchi hii kwa sasa umeyumba kwa kila mtu, kila taasisi, sio Chadema peke yao, na hilo zigo nalo anabebeshwa bosi wako asiyejua namna bora ya kutawala nchi, badala yake anakazania kila siku kununua Bombardier.
 
Kwetuntwara

Senior Member
Jun 13, 2020
143
225
CHADEMA wanadai hawautambui Uchaguzi Mkuu 2020 lakini wanachukua ruzuku za serikali zinazotokana na Uchaguzi Mkuu 2020!

Baada ya muda hata wabunge wa viti maalum watapeleka bungeni hata kama sio kina Halima Mdee na kundi lake!

CHADEMA wananikumbusha ule mwaka ambao Mbowe alikataa kupewa gari la KUB eti halina manufaa lakini baada ya wiki akaenda kuchukua kimya kimya!

Kama umewekeza ''mayai yako yote'' kwa wanasiasa wa CHADEMA kwa kuamini maneno yao, anza kujiandaa kupata mshituko!
Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu....mpooo?
 
Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,299
2,000
Nimesoma hapo mwisho tu,nikajua pumba bado zimejaa miongoni mwa watanzania, naishauri serikali kurudisha elim ya UPE
 
X-bar

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
839
1,000
Mtoa mada hivi ushirikiano wa CHADEMA na ACT kupambana na CCM na vyama vingine bado uko palepale au?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom