CCM tuungane kupinga upuuzi wa UKAWA

CCM tuungane kupinga upuuzi wa UKAWA

Ni Wakati sasa kwa wana ccm kuungana na kuwaonyesha UKAWA kuwa si kila wanachofikiria wao nI sahihi LA hasha. Kama rais ameelezea vema suala LA Escrow kwamba zi pesa za Umma ni kwa nini wao walazimishie?

My take: Tuache utoto hata katika mambo yasiyohitaji elimu ya msingi kuyaelewa.
Kikwete mwenyewe alisema atamshhanga mwana ccm anayetetea uovu. zaidi buge zima lenye wabunge zaidi ya 70% waliungana juu ya suala hili. Elewa kuwa maazimio ya bunge si ya chama kimoja. Kikwete hakusema kuwa hakukuwa na pesa za umma. maana yake kulikuwa na esa za kodi. tena katika kuuza hisa serikali haikupewa kodi yake.
huoni maelezo yako ni ya uchochezi kwamba ccm kuungana dhidi ya ukawa maana yeke ni vita baridi ambavo mwisho wake vitazaa vurugu?
 
Bora yeye alizaliwa kwenye matope kuliko wewe uliyezaliwa kwenye zizi la ngo'mbe ndio mana una akili kama za ng'ombe mpaka fimbo ndio unasonga mbele.

Wewe mkuda kwelikweli. Hujui kwamba aliyezaliwa kwenye zizi la ng'ombe ndiye mwenye waumini wengi duniani na ndiye anayekufanya ushangilie christmas.

Cc: Simiyu Yetu
 
Ni Wakati sasa kwa wana ccm kuungana na kuwaonyesha UKAWA kuwa si kila wanachofikiria wao nI sahihi LA hasha. Kama rais ameelezea vema suala LA Escrow kwamba zi pesa za Umma ni kwa nini wao walazimishie?

My take: Tuache utoto hata katika mambo yasiyohitaji elimu ya msingi kuyaelewa.

kama siyo za umma kwanini maswi kasimamishwa ?
 
Wewe wenzako wameshaungana Na kugawana mabilioni ya iptl nyie masikini ndio mnadanganyana huku mwenye Mtandao.
 
Ni Wakati sasa kwa wana ccm kuungana na kuwaonyesha UKAWA kuwa si kila wanachofikiria wao nI sahihi LA hasha. Kama rais ameelezea vema suala LA Escrow kwamba zi pesa za Umma ni kwa nini wao walazimishie?

My take: Tuache utoto hata katika mambo yasiyohitaji elimu ya msingi kuyaelewa.

Funguka mwana
 
Rais kaelezea nini kuhusu watumishi wa umma kupewa zawadi zinazozidi shilingi 50,000 bila kuziripoti kama inavyotakiwa na sheria ya maadili ya uongozi Tanzania?

Ukiomgelea mambo yasiyohitaji elimu ya msingi, hilo mbona hujalitaja?
 
watanzañia mnaendeshwa kama maroboti mnaruka inayopigwa na upepo unakolalia ...mashirika ya umma ya TBC na ATC yanatumia pesa za umma vibaya huku kodi watu wakila na kusaza lakini ahaaa,wala huko hakuwahusu ...mngekuwa kweli mnajitambua msingeyaona haya yanatendeka kisha mkajifanya makatuni
 
Kama sio ya umma kwann CAG alikwenda kukagua na kwann mama Tibaijuka mmemuonea yy km sio ya umma amesema alipewa na kaka yake CCM mnakotupelika inatia huruma
 
Una saratani ya fikra, Tanzania ipo na itakuwepo hata bila ccm, ukawa na makundi mengne,, unapojaribu kuinangamiza Mama Tanzania kwa maslahi ya ccm hatutasita kukukemea kwa nguvu zote na tena ushindwe,, rushwa nyng zenye sura ya escrow zinataka kuiangamiza mama Tanzania hatutakubali kamwe, kamwambie aliyekutuma kwamba waTanzania wamekataa!!
 
Kuelezea vizuri kwenu msiofahamu suala zima la escrow na iptl hadi msubiri kuhadithiwa na mgonjwa aliyehadithiwa na vilaza walioamua kumpotosha kwa Makusudi!Rais ni wa kuwa empeached huyu,mara kadhaa amekuwa akivunja katiba aliyoapa kuitetea!Anaongea Uongo mchana Kweupe bila aibu,ni kwa kuwa anadhani watu wote ni Mburula km ulivyo wewe mtoa mada na wapuuzi wenzako.Sivyo ilivyo,Wazee wenyewe walimshtukia upuuzi wake, na wangepata nafasi ya kumuuliza maswali pangenuka, sasa poyoyo km wewe unakurupuka na kuja kuhara hapa kama fisi!Shame!

Kati ya Rais na PAC ni yupi alikuwa mwongo ? Rais alisema mpaka Escrow account inafungwa kwa mujibu wa ripoti ya CAG mlikuwa na pesa 202 Billions PAC wanasema mlikuwa na 306 Billions na ndio pesa zilizoibwa, Rais alisema kabla ya kufunguliwa kwa account ya Escrow IPTL walikuwa wanapeleka invoices zao Tanesco nao walikuwa wanalipa moja kwa moja kwa IPTL, baada ya Tanesco kuhisi wanalaliwa na IPTL ikabidi watoe notice kwa IPTL juu ya kutokubaliana na malipo hayo hivyo basi wakalazimika kufungua Escrow ili Tanesco badala ya kuzipeleka pesa zile IPTL waziweke kwenye account hiyo ya Escrow , lakini kwa mashart kwamba IPTL wataendelea kusubmit invoices zao kwa Tanesco za kiwango kilikile kilichokubaliwa na Tanesco kwa mujibu wa hukumu ya ICSID,si vinginevyo mpaka swala lao litakapopatiwa ufumbuzi.kwa muda wa miaka saba hapakuwa na ufumbuzi juu ya swala lile kwa uelewa wangu mdogo IPTL haikuwa na wajibu wa kukokotoa viwango vipya vya capacity charges kwa sababu hawakuwa na madai, bali Tanesco ndio walipaswa kufanya kazi hiyo na kuwapa IPTL ambao nao wangeipitia na kuikubali ama kuikataa, lakini hata wangekubali bado wangelazimika kukubaliana ni lini viwango hivyo vipya vianzie(Mwaka). sasa kwa miaka saba hapakuwa na viwango vipya na kwa nini IPTL asisema kwamba pesa zile ni zake kama ilivyokuwa awali kabla ya kufunguliwa account hiyo ya Escrow? jiweke wewe katika nafasi hiyo ya IPTL, hivi ungesema pesa ile iendelee kubaki kwenye account ya Escrow wakati huo pia unaendelea kutoa huduma?.

Kwa mtazamo wangu kosa kubwa limefanyika kwa Tanesco kushindwa kukokotoa viwango vipya, hata PAC nao walishindwa kuwashauri Tanesco ama kuwasaidia kukokotoa viwango hivyo vipya maana mpaka wanatoa ripoti yao hawakuonyesha endapo viwango vipya vingekokotolewa Tanesco ingeweza kuokoa kiasi gani,alafu katika ulimwengu huu wa utandawazi sio jambo jema kushawishi wengine wakubaliane na mawazo yako kwa matusi , kejeli, na hata vijembe bali hoja pekee ndio zitafanya watu wakubaliane na wewe, hivi leo ukisema Rais ni mbumbumbu kwa sababu tu alichosema wewe haukkubaliani nacho, una hakika gani kwamba yale unayoyaamini wewe wote wanakubaliana nayo? mizani gani ambayo wewe umeitumia kupima uzito wa hoja zako na kuona kwamba zina unzito kuliko za Rais?.
 
kwa hiyo unataka kuaminisha umma kwamba kakosea kumwondoa prof na maswi?
 
Nashkuru kwa kuwa muwazi kuwa unauelewa mdogo, sasa nakushauri usipende kurukia mambo complex kama haya yanayohitaji integrated knowledge and analytical minds ili kubaini ubabaishaji upo wap. Kimsingi Rais kaungana na mijizi aliyohitaja Lissu pale bungeni kwenye huu ukwapuaji wa fedha katika account ya escrow.
 
Kama sio ya umma kwann CAG alikwenda kukagua na kwann mama Tibaijuka mmemuonea yy km sio ya umma amesema alipewa na kaka yake CCM mnakotupelika inatia huruma

Sababu kubwa iliyomfanya CAG aende kukagua ni kwamba hilo lilikluwa ni moja ya hadidu za rejea alizopewa na Waziri mkuu, na Waziri mkuu alifanya hivyo baada ya wabunge kudai kwamba pesa za umaa sh 306 billions zimeibiwa kwenye account ya Escrow, hilo ni jambo zito sana, watu wengi nikiwamo mimi niliamini kwamba pesa za uma sh 306 billions zimeibwa, najua hata wewe pia, sasa moja ya kazi ambayo CAG alipaswa kuifanya ni hiyo kujibu swali la kwamba je pesa zile zilizokuwa kwenye account ya Escrow nui za umma ama ni IPTL?.

katika ripoti yake CAG alijibu kwamba ndani ya pesa zile mnawezakuwa na pesa za uma ama zisiwemo! Rais kwa mujibu wa maelezo yake alitaka ufafanunzi wa statement hii maana haikuwa conclusive, akajibiwa kwamba palikuwa na namna mbili (2) za kuwemo kwa pesa za uma kwenye account ile ya Escrow namna ya kwanza, ni kwamba Tanesco walikuwa wanalalamikia tozo kubwa ya capacity charges ambayo IPTL walikuwa wanaitoza, hivyo kama wangeweza kuestablish viwango vipya kwa IPTL kujustfy madai yao, na IPTL kuridhia, tena wakakubaliana madai hayo yaanzie mwaka gani, basi ina maana katika zile pesa Tanesco wangeweza kuokoa kiasi flani, lakini kwa muda wa miaka sabab Tanesco hawakuwahi peleka viwango vipya kutibitisha madai yao,namna ya pili ambayo inaifanya Escrow account kuwa na pesa za uma ni kwa njia ya kodi kwa sababu IPTL baada ya kuchukua pesa zile hakuwa amelipa kodi, sasa ebu mimi na wewe tujiulize jambo moja ikiwa mimi na wewe tunafanya biashara na mimi nikalalamika kwamba wewe unanilalia katika malipo, tukamtafuta mtu wa tatu asaidie kushikilia pesa ambazo mimi nilipaswa kukulipa wewe direct, ikisubiliwa mpaka mimi nikupatie viwango halali kwa mujibu wa madai yangu, lakini miaka inapita mimi naendelea kulipa kwa viwango vilvile vya zamani wala nisikupe viwango vipya nani mwenye kosa hapo wewe ama mimi?.

Mama Anna Tibaijuka hakuwaachishwa kazi kwa sababu tu ile pesa ni ya umma hapa bali kwa sababu ya kukiuka miiko ya maadili ya utumishi wa umma, alipaswa ku-declare kwamba amepokea pesa kiasi flani kwa kwajili gani that all !
 
Mimi ni mwanaccm lakini siwezi kuungana na mafisadi kisa nipo ccm. Mpuuzi mkubwa wewe labda uungane na dada ELizaboni na mama mwa 4 (Mwajuma)

Yes unajielewa kuwa ccm au chadema then kujifanya uoni uovu kisa unamaslai tu ni ujinga pleas elimisha ccm wenzio ambao wanajitoa akili sure ukiwa hivyo kwenye siasa utafika mbali komaa
 
Nashkuru kwa kuwa muwazi kuwa unauelewa mdogo, sasa nakushauri usipende kurukia mambo complex kama haya yanayohitaji integrated knowledge and analytical minds ili kubaini ubabaishaji upo wap. Kimsingi Rais kaungana na mijizi aliyohitaja Lissu pale bungeni kwenye huu ukwapuaji wa fedha katika account ya escrow.

Kwa wewe mwenye uwezo mkubwa basi tusaidie wewe kujua kwamba ni wajibu wa IPTL ama Tanesco kukokotoa viwango vipya vya tozo? hata kama kuna harufu ya udanganyifu juu ya viwango vile vya IPTL kwa uelewa wako wewe mwenye akili kubwa ilikuwa ni wajibu wa nani kutibitisha udanganyifu huo IPTL ama Tanesco?.wewe unakubali kwamba sh 306 billions fedha za uma zimeibwa ama sh 202 billions zimelipwa na IPTL kutoka Escrow account?
 
Hiyo kikwete mwenyewe kila siku hakosi msemo wake za kuambiwa changanya na zako kwa hiyo ulivyomsikiliza hiyo kikwete ndio umemwamini kwa akiri zako kuwa zile pesa si za umma
 
Kweli nisikufiche, uwezo wako wa kijenga hoja ni mdogo sana sana, na Bahati mbaya hata hujijui, hizi pointi haziwezi kufanya pesa iwe ya umma, tusimuonee muwekezaji Haki yake apewe tuwaumu walotuingiza kwenye mkataba hata tukawa overcharged

Sidhani kama utakuwa unajitambua vizuri yaani kifikra na kimtazamo swali la msingi lililopo hapo Kikwete katamka wazi kuwa fedha ni za IPTL je inakuwaje mawaziri, watumishi wa umma na viongozi wa kamati za Bunge waliopokea fedha hizo kuwajibishwa kwa suala hilo? jitahidi kuuweka vizuri ubongo wako ufikirie mbele zaidi sio kujikita kwenye ushabiki pasipo kuwa na fikra pana.
 
Uungane labda na wanaojipambanua kuwa ni wasomi wa udom ndio watakaokusapoti
 
Mama Anna Tibaijuka hakuwaachishwa kazi kwa sababu tu ile pesa ni ya umma hapa bali kwa sababu ya kukiuka miiko ya maadili ya utumishi wa umma, alipaswa ku-declare kwamba amepokea pesa kiasi flani kwa kwajili gani that all !

Mbona ali-declare akasema ni za kuendeshea shule?
 
Back
Top Bottom