Tundu Lissu tayari ameshaonyesha wazi kuwa ni mwiba mchungu kwa CCM kuelekea kwenye kampeni, kwa muda mfupi aliopanda kwenye majukwaa yasio rasmi kwa ajili ya kampeni ameoneka kuwa Ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja zitakazo wabadilisha wengi mawazo hata kwa WanaCCM wenyewe.
Huyu Tundu ana uwezo mkubwa sana wa kujieleza, kujenga , na kutetea hoja kuliko watu wanavyo fikiria.
Na kwa vile Watanzania wa leo wengi hawana tena ushabiki wa vyama kama zamani, ni rahisi sana kuoambanua kile anacho kusema Lissu na yale yaliyotokea miaka mitano iliyo pita Kisha wakachukua hatua ambazo zitaweza kuishangaza hata CCM ambao wanadhani wanaweza kuhodhi utawala milele.
Ni ukweli ulio wazi tu kwamba kwa vyama vyote vya siasa watu wao watakaopanda kwenye majukwaa ya kampeni wasipojipanga vizuri Tundu atawagaragaza vibaya sana kwa hoja.
Kuna hoja dhaifu inayotolewa na makada wengi wa CCM kwamba urais hauwezi kutolewa kwa mtu kama huruma kwa sababu tu eti alipata shambulio la kupigwa risasi; huo ni udhaifu wa kujenga hoja na hilo litweza kuamsha hisia na kuwakumbusha wengi juu ya kipindi kigumu walichopitia Watanzania hapo nyuma.
La msingi kwa CCM msimbeze Lissu na kujaribu kupambana naye, bali mjipange kupambana na hoja zake ambazo kwa hakika zitakuwa kama msumari wa moto kwenye kidonda kibichi.