CCM tusiende tena kwenye Midahalo

CCM tusiende tena kwenye Midahalo

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Leo nilikuwepo Serena Hotel kuhudhuria Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi moja binafsi nchini (jina limenitoka). Nimesahau hadi jina la Taasisi kwa yaliyotokea pale. Mdahalo huo ulikuwa ukiongozwa na Bi.Rosemary Mwakitwange na kurushwa moja kwa moja na ITV na Radio One. Pamoja na washiriki wengine,meza kuu iliwajumuisha watu 'wazito'.

Mdahalo ulijikita katika Mada: Tanzania Tuitakayo.Lakini hasa ilizungumzwa sana Rasimu ya Katiba mpya.Meza kuu ilikuwa na Wageni kama Ndugu Juma Duni Haji (Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF),Ndugu Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar) na Humprey Polepole (Mjumbe wa zamani wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba).

Kiufupi,CCM tumedhalilishwa,tumezomewa,tumejichanganya,tumepoteana,tumejiharibia na kukosea kuhudhhuria pale. Vuai hakutusaidia. Alibaki kutetema kwa hasira na kushikwa na tashwishwi zisizo na maana. Eti alidai watu 9000 ni asilimia 5 ya watu wote wa Zanzibar.Kweli?! Hivi hata kama Zanzibar ina watu milioni moja kamili,asilimia 5 ni watu 9000?

Duni na Polepole walitamba walivyoweza.Walishangiliwa.Walifunika.Walimpotezea mbali Vuai. Walishinda kirahisi kutokana na mwakilishi wa CCM kukosa hoja za haja na kubaki kubwabwaja. Sikuamini macho yangu.Watanzania watatuonaje kiuongozi kama watu waliopo ni watu aina ya Vuai? Tusiende tena kwenye Midahalo

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Tehe tehe tehe! Hata mi niliona kwa kupitia ITV ilikuwa ni aibu sana.
 
TIDO ndio kiboko yao aliweka hadharani maradhi ya ccm kuhusu midahalo
Hawatamsahau tido maisha yao makamba baba alichanganyikiwa
 
Leo nilikuwepo Serena Hotel kuhudhuria Mdahalo ulioandaliwa na Taasisi moja binafsi nchini (jina limenitoka). Nimesahau hadi jina la Taasisi kwa yaliyotokea pale. Mdahalo huo ulikuwa ukiongozwa na Bi.Rosemary Mwakitwange na kurushwa moja kwa moja na ITV na Radio One. Pamoja na washiriki wengine,meza kuu iliwajumuisha watu 'wazito'.

Mdahalo ulijikita katika Mada: Tanzania Tuitakayo.Lakini hasa ilizungumzwa sana Rasimu ya Katiba mpya.Meza kuu ilikuwa na Wageni kama Ndugu Juma Duni Haji (Waziri wa Afya wa Zanzibar-CUF),Ndugu Vuai Ali Vuai (Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar) na Humprey Polepole (Mjumbe wa zamani wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba).

Kiufupi,CCM tumedhalilishwa,tumezomewa,tumejichanganya,tumepoteana,tumejiharibia na kukosea kuhudhhuria pale. Vuai hakutusaidia. Alibaki kutetema kwa hasira na kushikwa na tashwishwi zisizo na maana. Eti alidai watu 9000 ni asilimia 5 ya watu wote wa Zanzibar.Kweli?! Hivi hata kama Zanzibar ina watu milioni moja kamili,asilimia 5 ni watu 9000?

Duni na Polepole walitamba walivyoweza.Walishangiliwa.Walifunika.Walimpotezea mbali Vuai. Walishinda kirahisi kutokana na mwakilishi wa CCM kukosa hoja za haja na kubaki kubwabwaja. Sikuamini macho yangu.Watanzania watatuonaje kiuongozi kama watu waliopo ni watu aina ya Vuai? Tusiende tena kwenye Midahalo

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Ukiwaona walikuwa Bungeni wenyewe lakini bado wakawa wanarusha matusi juu ya UKAWA basi ujue hao watu ni wepesi.Niamini ikifika kwakati wa kampeni wategemee wizi wa kura na kwa kuwa tume ni yao ili kulazimisha maoni ila kusema ukweli CCM bila vyombo vya dola haipo .
 
Kwa hiyo ule ulikuwa uchaguzi? Pole pole amepata kura ngapi?
 
Nape alitegemewa awepo mdaharoni akamtuma vuai a vuai ambae amekaririshwa majibu na kuyatoa bila kuya chambua;anafanya paper ya math ameingia na majibu ya bios
 
Si kweli, tupatupa unasema uongo. Vuai ali vuai ni kati ya waliozungumza vizuri tena kwa kujiamini pamoja na yule Awadh ....wa tume za haki za binadamu zanzibar. Polepole aikuwa anatumia madesa na gugo kuleta "fact" za kujitutumua.
 
Ishu ya katiba ni nzito kwa mwana CCM yeyote. Hata angekuja Wassira angechemka tu
 
Twende na mada acha porojo zisizo na mashiko, hujui hata majimbo yaliyoko upinzani yalikuwa ya CCM? Nani anapoteza nani anaongeza utajua mwenyewe. Leo ilikuwa aibu na ukweli utajulikana tu mnafikiri zile taarabu zenu za wingi wenu mjengoni watu tunafurahi? Poleni sana kwa aibu mnayopata
,come back TANGANYIKA:israel:
 
Si kweli, tupatupa unasema uongo. Vuai ali vuai ni kati ya waliozungumza vizuri tena kwa kujiamini pamoja na yule Awadh ....wa tume za haki za binadamu zanzibar. Polepole aikuwa anatumia madesa na gugo kuleta "fact" za kujitutumua.

Duh!!CCM wajinga sana
 
Back
Top Bottom