w
Embu weka hapa ushaidi kama kweli wewe ni mwana ccm . Hizi ni propaganda za kitoto . Hata mimi naweza kujisemea ni mwana TADEA kwa manufaa fulani wakati sio kweli mwana TADEA.
Hii ndiyo shida ya kilichokuwa chama changu toka TANU.
Wengi tumejiengua kutokana na kushindwa kwa juhudi zetu za kukikosoa chama tukiwa ndani kwani kila tulipofanya hivyo tuliishia kuitwa "Wasaliti" au "Wamenunuliwa".
Pole pole chama kinawapoteza wanachama wenye moyo wa dhati na kujaza mamluki toka upinzani.
Binafsi nilihamia upinzani baada ya kuchukizwa na tabia mbovu za viongozi walioonekana dhahiri kuzidiwa hoja na wapinzani haswa CHADEMA.
Kwa hakika watanzania tumechoka na muda unaopotezwa na wabunge na mawaziri akiwemo Waziri Mkuu kuhangaika na kupeleka mashambulizi kambi ya upinzani na kwa njia hiyo kuupaisha umaarufu wao!
Najua wapo watakaobeza hoja hii lakini mambo yakiendelea hivi nina mashaka kama chama changu cha kale kitamudu hata kuunda kambi ya upinzani.
Mi natabiri mambo yakiendelea hivi itakuwa vigumu kupata hata wabunge 20 katika bunge lijalo.
Hivi ni kipi mtakachowadanganya wananchi mkafanikiwa? Matumizi ya Polisi kukisaidia chama kila mmoja anayaona, hongo za kununua mashabiki wa kuhudhuria mikutano yenu zinapokelewa hadi na wapinzani, utekaji nyara na kuteswa kwa walio kinyume chenu kuko wazi mno na karibu kila mtanzania wakiwemo makada wanafahamu ni nani anayehusika! Wakati nyinyi mnahangaika kuudanganya umma eti ni CHADEMA mitaani kote watu wanawasema ni Usalama wa
Taifa kwa maelekezo ya CCM!
Sijui kama yupo hata kingozi mmoja wa CCM anayesoma kijitabu cha Hayati Baba wa Taifa - mwasisi wa chama chenu cha "Tujisaihishe".
Muda ukifika ugonjwa utajitokeza hadharani na kuwaumbua kweupee!