CCM tupo katika mwanguko mkubwa

CCM tupo katika mwanguko mkubwa

Wewe bungeni wewe,we ni Mtz kweli? Naanza kuamini sasa kuwa kuna watu huwa wanalipwa kwa kupost ishu za kushabikia CCM,ndio maana mnakaa na kupanga sh.bilion 1 kwa ajili ya mazish ya viongozi,tuweni wazalendo tuache ushabik wa vyama jamani!
 
Sawa inabidi tukubaliane kihivo hivo tu na nyie watani zetu kwa kuwa huo ndio mkondo mpya wa demokrasia bungeni.

Lakini sasa kosa la wabunge watano kwa kambi ya upinzani ndio sasa iwe ni utakaso wa zile lugha chafu mwisho za uswahilini kwa sehemu kubwa ya wabunge wa upande wa CCM kweli ndio haki inavyokwenda kweli mtani???

Ninavyomkosa Mzee Samwel Sitta a.k.a mzee wa viwango na kasi salama bungeni, ama kweli sipati picha mimi. Naona kuna haja tena ya dharura kwake Mheshimiwa Sitta akaandae darasa la uspika kwa hawa wanagenzi au akajitwalie kabisa mkoba wake uuuupya!!!!!!

Mpaka hivi sasa ni dhahiri kwa namba SITA katika uwanja wa mpira pale bungeni inapwaya hakuna mfano wake na hivyo kulazimisha timu yetu ya maendeleo kwa taifa kucheza muda wote golini kwao bila kiungo muhimu huyu wa kuweza kuwalisha washambuliaji mahiri akina Zitto, Lema, Lissu, Sugu, ... Msigwa ... kwenda kuwafungia bao umma wa Tanzania.

Kama kuna yeyo anabisha juu ya madai haya mazito ajitokeze apate kuhesabisa si kwa povu bali hoja tu.

Naamini kulikuwa na mgongano wa lugha, ndughai alisisitiza mh lisu atoke nje hakufafanua kawa atoke nje aende wapi? Si abaki ndan?
kumwambia mtu toka nje manake nini kama si haingie au habaki ndani?
Elimu za maghamba ata kiswahili hakipandi tabu kweli kweli
 
UTASHI BINAFSI WA NDUGAI KUJIPANDISHA GHADHABU KUMFUKUZA MJUMBE BUNGENI NI UKIUKWAJI WA HAKI NA WAJIBU WA SPIKA KUSIMAMIA CHOMBO HIKI CHA UMMA

Kama kweli Mhe Tundu Lisu aliamriwa na 'Kiti Cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania' KUTOKA NJE kwa kuwekewa wazi kosa lake na kusomewa KIFUNGO fulani kinachotamka mbunge kufanya hivo kwa mujibu wa kifungu kinachojulikana wazi na bila ya kuwepo hata chembe cha ushawishi wa tofauti za kiitikadi hapo kidogo tungeelewa.

Lakini kitendo tu cha Mwana-CCM mmoja kwa jina la Job Ndugai kuhisi kwamba kikao cha bunge kimechukua muda mrefu sana kwisha hivyo akajiamulia tu kwa utashi wake tu mwenyewe na kuanza kukoromea mjumbe eti atoke nje bila hata ya kutamkiwa kosa wala kifungu cha kanuni za bunge zinazounga mkono uamuzi kama huo kamwe haikubaliki na wala bunge lisiendeshwe kwa misingi hii hata siku moja kwani kanuni zina kazi zake maalumu mle.
 
umenena hoja nzito..watu wanakushambulia?....tuitizame tanzania jamani ccm haitokupeleka popote pale...sante mchambuzi.
 
asante kwa kukumbushana haya mambo muhimu.

Chama cha Mwalimu Nyerere na Rashidi Kawawa, chama cha Bi Titi Mohamed na akina John Rupia, chama cha Sykes na wazee wote waliokwisha tangulia.
Sikutegemea kama mbunge wake angetamka neno 'f...y you' na spika aliye kwenye chama hicho hicho akaridhia na kusema "endelea mkuu". Wengi wetu hatukutegemea kuyashuhudia haya katika uhai wetu!

mkuu umemaliza yote sioni cha kujadili kwa sababu ccm wenyewe wanajua anguko lipo 2015 too late acha wafu wazikane hakuna marefu yasiyo na ncha ni mwisho wao ndo maana hawana cha kuchangia au kuwambia wananchi zaidi ya matusi makubwa bungeni alafu kiti cha spika kinafunika na wapinzani wanatolewa nje wao wajiona wajanja
kumbe ndo wanajimaliza wenyewe bila kujijua.da acha chama kife aje dk atuongoze sio kutawaliwa na ccm tena
 
Ushauli wameanza kupewa na mwl.Nyerere lakini responce ilikuwa zero.Hivyo kwa wewe hata ungewaimbia mashairi gani wasingekuelewa.Waache wakafie mbali.
 
Nilipofikia hapo, ndipo nikaamua kujiunga rasmi na CHADEMA! Nichukue nafasi hii kukukaribisha CDM kwa mikono miwili! Hamna dawa ya kuponya ccm! Ukiendelea kukaa huko utakufa kwa uchungu!
 
Leo wote humu jukwaani mtavaa kijani bila kupenda..kinana anazidi kuwacharaza mboko za mgongo huko morogoro..

Unajua linalozungumzwa katika thread hii lina asilimia nyingi za ukweli ndani yake. Mchangiaji anayeingiza mada ya KINANA AZIDI KUWACHARAZA MBOKO ZA MGONGO HUKO MOROGORO , kwa mtu mwenye kufikiria vizuri utagundua ni mmoja kati ya waliotajwa katika thread hii, kwani hatofautiani kabisa na mawazo ya mchangiaji aliyesema "sikio la kufa.........." Hakupaswa kuingiza jambo jipya la kina kinana badala ya kutafakari thread ile kwa undani na aondoe machungu kama imemtouch.
 
Umewasilisha ujumbe mzuri kwa chama cha zamani endapo watauzingatia maana anguko hili hata Mzee Mzindakaya ameliona japokuwa wenyewe wanajifanya hawaoni.
 
Dah kweli kabisa....atakaekupinga hana mapenzi mema na Chama cha Mapinduzi
 
hali sio nzuri chama kipo icu na nasikia wameshaanza kuchanganya dawa ya kumdunga akiwa mochuari lakini cha ajabu dawa yenyewe imegoma kuchanganyika. Rip chama changu ccm.:a s cry::a s cry::a s cry:

vp babuu rogger,hawa kuku chakachua kwenye mabaraza ya katiba ndugu,
 
Hali sio nzuri chama kipo ICU na nasikia wameshaanza kuchanganya dawa ya kumdunga akiwa mochuari lakini cha ajabu dawa yenyewe imegoma kuchanganyika. RIP chama changu CCM.:A S cry::A S cry::A S cry:

Huku mwenyekiti akiwa bize kuhudhuria mazishi ya wasanii!
 
wewe bungeni wewe,we ni mtz kweli? Naanza kuamini sasa kuwa kuna watu huwa wanalipwa kwa kupost ishu za kushabikia ccm,ndio maana mnakaa na kupanga sh.bilion 1 kwa ajili ya mazish ya viongozi,tuweni wazalendo tuache ushabik wa vyama jamani!

usipate sida mkuu,mtu yoyote leo ukimwona anashabikia ccm,ujue ni njaatu zinamsumbua alafu unazani wanapewa nini,2,000 na kuvalishwa kofia na tisheti,mtu mwanzo wa hasubui mpaka jioni utamkuta ofc za chama,na kushabikia ujinga wa ccm,huku ni kukosa akili na kufa kifikra,tunatakiwa kwanza tuwa fufue hawa watu wanamna hii,nape,akija wanakimbia mpaka wana anguka chini yaani wamelogwa kweli na chama cha wapiga dili,
 
Mkuu hapa unaipigia tarumbeta MAITI, sidhani kama utasikika. Tunawaacha wafu muwazike wafu wenzenu...
 
hali halisi ya maisha wanayo ish wanayo ishi watanzania...na upuuzi wa wabunge waccm hasa mwigulu..ndio vinafanya ccm ife
 
Napenda mawazo chanya kama haya. Ya kukubaliana na hali halisi
 
Haijalishi nani kaandika, awe ni magamba au magwandwa hiyo ndio hali halisi na kwa kweli ametoa changamoto kwa wahusika. Chukueni mkazifanyie kazi badala ya kuendesha ubabe. Ebu someni Mwongozo wa CCM wa 1981 Ibara 59. mnaoropoka tu eti mnategemea Nape, Mwigulu, Kigwangala, lusinde, Mkamia na Serukamba kukijengea hoja chama. Hao ni zero kabisa tena ndio wanaharakisha ANGUKO KUBWA LA CCM.
 
Watanzania wenzangu wana CCM wenzangu leo hii napenda kutoa ukweli mchungu ambao wenzetu hawataki kuusema aidha kwa makusudi ili liwalo na liwe, au kwa woga wa madaraka,au kuogopa kuwaudhi wakubwa au kwa faida ya matumbo yao wasiharibu nafasi na vyeo vyao hivyo wote tupo kimya kila mtu anamtazame mwenzake asijue lakufanya tupo katika mwanguko mkubwa wa chama chetu cha CCM.

Wana ccm wenzangu leo hii chama chetu hakina mkubwa wala mdogo wote tumekuwa kambale huu ni mwanguko mkubwa mfano ni bungeni wabunge wetu ndiyo wamekuwa wakijibu tuhuma za serikali badala ya kuibana serikali huu ni mwanguko ulio dhahiri.

Wana ccm wenzangu leo wabunge wetu wameamua kuwaachia vijana mahiri wa upinzani kuwasemea wananchi na wao wamebaki kupiga kelele za ndiyo na kutetea uovu wa serikali huu ni mwanguko mkubwa kwa chama chetu cha ccm.

Chama chetu bungeni huwezi kumtofautisha mbunge na waziri wote wamekuwa watetezi wa maovu ya serikali hili ni mwanguko mkubwa wana ccm wenzangu.

Vijana wetu mahiri wengine kama wachumi nambari moja kina Mwigulu mchemba yeye akisimama ananza kutukana ,CHADEMA, DR slaa ambaye hata bungeni hayupo ,MBOWE na wapinzani wakati vijana wa upinzani wanaogelea kwenye hoja na matatizo makubwa ya wananchi wana CCM wenzangu hili ni anguko kubwa ni mwanguko mkubwa

Wana CCM wenzangu mawaziri wetu wamefikia hawana hata uwezo wakujibu maswali kuanzia waziri mkuu na mawaziri wake hivi sasa wanatumia asilimia 90 ya mda wao kuwa attack wapinzani badala ya kujibu hoja murua na maridadi za wapinzani huu ni mwanguko mkubwa wana ccm wenzangu .

Wana CCM wenzangu spika na naibu wake wanasaidia kukiua chama chetu kwa kuwawekea kinga wajibu maswali ya umma hasa mawaziri kwa kuruhusu majibu yasiyokidhi haja ya wauliza maswali huu ni mwanguko mkubwa kwa chama chetu.

Wana ccm wenzangu spika wetu kupendelea chama chetu kwa wazi kabisa na naibu spika kuonyesha waziwazi hawapendi upinzani huko ni kuwapa wapinzani nguvu na mashabiki wengi nje ya uwanja na kutudhoofisha chama chetu huu ni mwanguko mkubwa wana ccm wenzangu.

Wana ccm wenzangu wabunge wetu hawawezi kujenga hoja tena kazi yao ni kupiga makofi na kuitikia ndiyoooooooooo.... HUU NI MWANGUKO MKUBWA WANA CCM WENZANGU.

Hata pale spika anapopunguza nguvu za upinzani kwa kuwapa adhabu eti kwa kuomba muongozo lakini wabunge wetu na mawaziri wetu bado hawawezi kukabili na kujibu hoja za wapinzani wanne tu kama ilivyokuwa alhamisi hoja ya wizara ya utawala bora ya waziri wassira na Kombani, mawaziri karibu sita mwanasheria mkuu na wabunge wote wa CCM walishindwa kujibu hoja za msingi kabisa toka kwa vijana mahiri wa upinzani mh.Mkosamali, HAlima Mdee, Mnyika na mzee wao professor Kahigi kwa walioshuhudia chama chetu kilishindwa kujibu hoja za msingi wabunge wetu na mawaziri wetu walishinda hoja ile kwa kura za ndiyoooo huo ni Mwanguko mkubwa wana CCM.

Wana CCM wenzangu ninaona mwanguko wa chama chetu ni kama UNIP ya mzee wetu KAUNDA au KANU ya mzee wetu MOI Tupo katika mwanguko mkubwa.

Wana ccm wenzangu chama chetu kinapowatetea watumishi waandamizi kabisa wa UMMA wa vyombo vya usalama wametuhumiwa katika kashfa kubwa kabisa na kuwaachia waendelee na kazi wakiwa katika kashfa nzito namna hiyo huo ni mwanguko mkubwa wa chama chetu na serkali yetu pia.

Wana ccm wenzangu inapofikia chama hakiwezi kufanya mkutano bila kuwahonga wanachama wetu kwa kanga kofia na kuwanunulia vyakula huo ni mwanguko mkubwa tena mwanguko mbaya sana.

Wana ccm wenzangu inapofikia ili kufanya mikutano inabidi tu import watu kwa maroli kuwaleta sehemu ya mkutano ili tujaze uwanja au ukumbi huku ni kujidanganya na hili ni anguko ni anguko kubwa sana huu ni mwanaguko ulio dhahiri.

Wana ccm wenzangu inapofikia hoja ya mbunge mmoja wa upinzani inajibiwa na mawaziri na wabunge wote wa chama chetu na bado haijitoshelezi hilo ni anguko ni mwanguko mkubwa. 0%

Wana ccm wenzangu tupo katika mwanguko mkubwa mwanguko mkubwa mwanguko mkubwa sana....

Wana ccm wenzangu hatuna wabunge wawakilishi wa wananchi na nchi tuna makada ambao kazi yao ni kuwajibu wapinzani hata katika zile hoja za msingi kabisa na za wazi wabunge wetu wao kazi ni kuwajibia mawaziri huwezi kujua mbunge wa chama chetu ni yupi na waziri we serikali ni yupi wote wamekuwa wakiijibia serikali hili ni anguko huu ni mwanguko mkubwa na 2015 utakuwa ni mwanguko mkubwa sababu wananchi watataka kupeleka wabunge watetezi wao na si watetezi wa dola.(?????)

Wana ccm wenzangu huu ni mwanguko mkubwa chama kubakia na wabunge wawili tu wawakilishi wa wananchi chama kuwakilishwa na Deo filikunjombe na Kange lugola pekee yao hili ni anguko ni anguko kubwa huu ni mwanguko wote tu mashahidi wa mashujaa wetu hawa wanavyotetea maslahi ya umma na siyo watu wa nddiyooo .

Tupo katika mwanguko wana ccm wenzangu chama chetu kinaangushwa kwa maslahi ya kwao tumekubali kuangushwa huu ni mwanguko mkubwa.

wana CCM wenzangu wabunge wetu wamechanganyikiwa kabisa husimama kwa kuponda hoja zilizotolewa na upinzani tena zile zenye maslahi kwa Taifa, hapo hapo anaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja 100% lakini hapo hapo huitoa kasoro na kuonyesha mapungufu ya hoja hiyo wana ccm wenzangu kama kitu kina kasoro kinaweza kuungwa mkono mia kwa mia huu ni mwanguko mkubwa kwa chama chetu.

Wana ccm wenzangu kuwanyima wapinzani viwanja vya kusemea kuwazuia mikutano yao bila sababu huku ni kuwaunganisha zaidi wapinzani na wananchi na huku ni kujihujumu wenyewe wanaofanya hivyo wanasaidia huu mwanguko na wamedhamilia kutuangusha.

Wana ccm wenzangu huko mawilayani kuwatumia ma RPC,OCD ,RC's na maDCkuzuia mikutano ya wapinzani kunajaza sana mori wananchi kuhisi wanahitaji ukombozi wa kuwatimua hao wakoloni weusi na kufanya chama chetu kizidi kuchukiwa hawa watu hawatusaidii ni sehemu ya mwanguko wetu.

Wana ccm wenzangu viongozi wetu wamekuwa ni kundi la kulindana hata inapotakiwa mmojawapo kuwajibika kwa heshima ya chama na serikali yetu hawako tayari kufanya na watatea kwa nguvu zote huu ni mwanguko tena mwanguko mkubwa.

Inapofikia waziri mkuu anatumia 90%ya mda wake kumsema tu mbowe na chadema badala yakueleza serikali imefanya na itafanya nini huo ni mwanguko tena ni mwanguko mkubwa na kama waziri mkuu ameanguka basi ndiyo wote tumeanguka tupo katika mwanguko.

Wana ccm wenzangu Kama naibu katibu mkuu wetu amekuwa akihusika kama inavyosemekana kuhonga na kununua wapinzani akifikiri ndiyo silaha ya ushindi wetu huko mbele hili ni anguko ni anguko dhahiri ni anguko lililo kubwa na kama tunataka kujenga taswira ya chama chetu kuepusha huu mwanguko basi tumpatie kazi nyingine sababu hana heshima tena mbele ya wananchi huu ni mwanguko.

Wana ccm viomgozi wetu hivi sasa hawana uwezo wa kushawishi wanachama wapya badala ya kurudisha imanai na kuendeleza misingi ya chama wao sasa hivi ni kurubuni wapinzani na kuwahonga viongozi wa upinzani na kitembea mbele uetu na makapi ya viongozi waliofukukuzwa na vyama vingine hii ni kuonyesha tumefika mwisho tupo katika mwanguko mwanguko ulio dhahiri huu ni mwanguko.

Wana ccm wenzangu tupo wengi tunaona mwanguko huu lakini tunapotoa ushauri hausikilizwi sababu chama kimekuwa genge la watu fulani hawataki mawazo nje huu ni mwanguko mwanguko uliodhahiri.

Wana ccm wenzangu tunajenga chama saa ngapi tunajibu kero za wananchi na kuzitatua saa ngapi kama kila ziara za chama utasikia inatajwa chadema na viongozi wakati chama kina mambo ya msingi hayajatekelezwa kwa miaka 50 sasa na hayana majibu sisi kila siku ni kuimba chadema, DR slaa ,mbowe nk huu ni mwanguko wana ccm wenzangu.

Wana ccm wenzangu pimeni wenyewe uelewa wa wabunge wa upinzani hotuba zao, hoja zao linganisha na wabunge wetu na mawaziri wetu mtajua kama kweli tupo katika mwanguko.

Wana ccm wenzangu wapinzani wana sema mbunge wao mmoja ni sawa na wabunge wa ccm 40 mimi ni mwana ccm mwandamizi nathubutu kusema wabunge wetu 40 na mawaziri watano ndiyo sawa na mbunge mmoja wa upinzani mwenye kubisha aangalie bunge kwa uangalifu na apime hoja za pande mbili atagundua tupo katika mwanguko.

Wana ccm wenzangu Maneno haya yatawakera wengi hasa wale wenzetu wanafiki wenye kuogopa ukweli kwa maslahi yao huu ni mkweli mchungu na lazima usemwe na wenye uchungu sababu tupo katika mwanguko mbaya.

Wana ccm wenzangu leo chama chetu kinazunguka nchi nzima kinasema CHADEMA ni chama cha kidini na kikabila wakati chama hiki kina wabunge toka mbeya, iringa , biharamulo, Mwanza, kigoma, maswa,dar es salaam kina wabunge dini zote kutuaminisha uongo wa dhahiri na kutufanya wanachama sisi ni ndondocha huu ni mwanguko mwanguko uliodhahiri.

Wana ccm wenzangu mwanguko huu hautazuiwa na polisi, wala vyombo vya usalama kama hatutakubari ukweli huu ni mwanguko mwanguko ulio dhahiri.

Watanzania wenzangu naombeni tujadili mwanguko huu katika hali ya utulivu bila kashfa sababu huu ni mwanguko mkubwa uliodhahiri namalizia kwa kusema tupo katika mwanguko.

Karibuni tujadili.


Haihitaji akili ya ziada kutambua kuwa wewe ni Mwanachama wa Chama cha KIGAIDI(cdm).
Hatuhitaji Mafumbo, jiweke wazi tu kuwa umetumwa au umejituma?
Kwakuwa Chama chako kimekosa mvuto sasa umeanza kuigiza Chama kubwa CCM.
 
Back
Top Bottom