CCM tupo katika mwanguko mkubwa

CCM tupo katika mwanguko mkubwa

Mkiacha ugaidi na utekaji, mkaacha kuibagua zanziba na kuacha siasa za kibaguzi na kibabe mnaweza kupiga hatua lakini hadi sasa mmeloa. Mwigulu, nape na kinana wanakusalimieni

Hawana jipya wachomvu huyu wameshaona mambo yanawaendea mlama sasa wanaibua hoja za udini Bungeni ili kuwagawa Watanzania.
Ccm hoyeee! Kidumu chama cha mapinduzi.
 
Hata mkitowa povu kama waanguka kifafa lakini ukweli unabaki palepale, ccm imeanguka na haitainuka tena. Rip ccm na mafisadi wako.
 
Hakuna wakati ulio kuwa mgumu kwa ccm kama wakati huu, mahali ambapo ccm walipafanya kama pa kutagia mayai na kutotolea (Mtwara) pamekuwa siyo pao tena. Raia hawataki tena kusikia wala kuona kofia na ma-T shirt ya ccm kwa sababu wamebaini hawa jamaa ni walaghai
 
Kianguke mara ngapi? Acheni wafu wazikane wenyewe.......watatumia kila kilicho ndani ya uwezo wao but hili jahazi kuzama hakuepukiki
 
CCM wangekuwa wanakaa na kujitadhimini wao wamekalia kupingana na kila kitu ata kama ni kizuri
Alafu sikujua kama Juma Nkamia ni Mbunge juzi ndo nilimwona"Naongea na mwenye mbwa sio Mbwa"
 
Anguko la CCM linasababishwa na mambo mengi na moja kati ya hayo ni dhambi iliyosababishwa na waliokiteka chama hicho kuamua kuwakataa wazee na busara zao kwa kuwafungia milango ili wasiwe wanashiriki ama kusikia yale yanayojadiliwa ndani ya vikao vyao wakihofia kukosolewa na kushindwa kupitisha ama kutekeleza agenda zao za kuihujumu nchi yetu.

Mbaya zaidi hata yale mazuri yaliyofanywa na kuaswa na waasisi wa chama hicho wameamua kwa makusudi kutoyazingatia kwa kudhani kuwa hayo yanawazuia katika kutekeleza agenda zao za kuhujumu na kuliangamiza taifa. Hata ukiangalia kwa makini, wanaokiongoza chama hicho kwa sasa wamekigeuza kuwa cha kifamilia/kindugu zaidi na mkakati wanaoufanya kwa sasa ni kuhakikisha kuwa waasisi wa chama hicho kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wanaondolewa ama kufutwa kabisa kwenye historia ya taifa hili ili majina yao na hayo ya ndugu zao yaweze kupata nafasi.

Watanzania ni vyema wakatambua kuwa CCM iliyoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere mwaka 1977 sio CCM iliyopo leo. CCM ya Nyerere ilikuwa ya WAKULIMA na WAFANYAKAZI na ilikuwa inapigania na kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msingi bila upendeleo wowote lakini CCM ya sasa imegeuzwa kuwa club ya wachache fulani, mafisadi na wale wenye uwezo na fursa ya kukwapua rasilimali za taifa
 
Hizi ni pumba, baada ya kuzidiwa hoja kwa vurugu zenu bungeni mmemua kujifanya wana ccm..na bado

kilichowaloga nyie watanzania wenzangu(ccm) masikio yenu mlishaziba pamba kero zote za wananchi mlishawaachia wapinzani wawe wasemaji wa kero wananchi bungeni, mpaka majimbo yenye wabunge wa ccm tunajihisi wanyonge kwa kukosa mwakilishi dhabiti bungeni na sio kuwa hakuna kero tatizo wakisema mnawaita ni chadema(mfano filikojombe) sasa hapa mtegemee anguko tu !! Hapa hamkwepeki
 
Umeeleka vyema mwanatanzania,hapa tunazungumzia Tanzania,yeyote mwenye uchungu na nchi hii huweka maslahi yake pembeni na kuangalia mustakabali wa taifa letu.

Umeeleweka kwa sababu ni dhahiri isiyo na shaka kuwa taifa la Tanzania lipo ktk ombwe kubwa la kiuongozi.Leo hii nchi inaharibika na hakuna wa kumvesha paka kengele.

Leo hii wanainchi wametambua umuhimu wa kuunganisha pamoja nguvu zao na kupigania uhuru wa pili wa Taifa hili tajiri kwa raslimali ila ni masikini wa kutupwa hapa duniani.

Wanawanchi hii wamebaini janja ya watawala na wasomi uchwara wanaopenda vitu na vyeo badala ya kutumia elimu zao kuiokoa nchi yetu,badala yake wanajitajilisha na kujilimbikizia mali wao na watoto wao kana kwamba taifa hili ni mali yao.

Daima tutakukumbuka kambarage jemedali wetu makini na baba wa taifa,wapo tulioupokea usia wako wa kuweka mbele maslahi ya taifa,tunakukumbuka kwa kuongoza kwa mfano hukujilimbikizia mali,hukujaza vilaza,mashemeji,makuwadi ikulu,Hukupendelea wapambe wako,watoto wako wala marafiki wa watoto wako na kuwapa nyadhifa serikalini ilhali uwezo hawana.hukuigeuza nchi kuwa mali ya kundi la wachache wasiozidi hata asilimia 10% wanaonufaika na kuzitumia mali za nchi wanavyotaka.

Mwalimu yote uliyoyapigania na kuyatenda tumeyaona na watawala wa leo wameshindwa kuvaa viatu vyako,daima utakumbukwa na kuenziwa.

Ni kweli anguko la CCM ni dhahiri na halina kificho,kujilidhisha kuwa kuna mwenye uwezo wa kuzuia anguko hili ni kujidanganya kwani maumivu vijijini yamekithili na waswahili hunena ukiona tabu na mateso yanazidi ujue ukombozi uko karibu,wanawanchi wanausubiri ukombozi kwa hamu kubwa.
 
Kamuulize mwigulu nchemba madelu ndio atakwambia umakini wa ccm sio ukurupuke na njaa zako za kulipwa kwa thred na post uje uwahadae watu humu.mleta mada shame on you!
Tetetete Ccm hamtaki ukweli mmezoea unafiki kama mwigulo mwenyewe
 
ccm. CDM uozo mtupu, hakuna wazalendo.
 
HAPO ZAMANI ZA KALE KULIWAHI KWEPO CHAMA CHENYE MSIMAMO WA 'WAZAWA KWANZA' ILA LEO HII MAMBO NI 'WAMAASAI WATAJIJU' - MWARABU KWANZA LOLIONDO!!!!

Mkuu 'Kite Munganga', mbona hivo ndani ya nyumba muda wote kimya hivo?? CCM ya J.K. Nyerere MAFISADI waliamua kukichinjilia mbali haakipo teeeena.

Na
sasa hivi CCM ya J.K. Kikwete ndio kama hivyo tena umeondolewa upepo wooote na kundi lile lile la MAFISADI kwa kulipeleka puta kiti cha spika kwa kutumia REMOTE za kila namna hata kwa mambo ya msingi mno kwa uuma wa Tanzania.

Lakini pamoja na yote walau mmoja katika kundi hilo na mwenye uchungu amejitokeza kusema hadharani mambo yanavyokwenda ovyo mote katika serikali hii ya CCM.

Mambo hivi sasa tambalale fyongo tupu!!! Kumebaki ubinafsi kwa kwenda mbele, fitina na majungu kwa sana si kwa baadhi ya vijana tu na wala sana si kwa akina wazee fulani tu - hali si shwari kule CCM ndio kama hivo tumebainishiwa kila kitu humu.

CCM kwishney na mpango mzima makaratasi za mazingaombwe kupiga kura toka Uchina - kila siri njee kweupe kwa 2015!!!!!!!!!
 
Ccm utawajua tu, wanaacha kujadili "hoja" iliyotolewa wao wanamjadili mtoa "hoja". Anguko kuu!
 
Upuuzi mtupu,ccm iko imara kuliko wakati wa mchonga. Muanzisha uzi ni kijana wa Slaa,kitengo cha tindikali
 
HAPO ZAMANI ZA KALE KULIWAHI KWEPO CHAMA CHENYE MSIMAMO WA 'WAZAWA KWANZA' ILA LEO HII MAMBO NI 'WAMAASAI WATAJIJU' - MWARABU KWANZA LOLIONDO!!!!

Mkuu 'Kite Munganga', mbona hivo ndani ya nyumba muda wote kimya hivo?? CCM ya J.K. Nyerere MAFISADI waliamua kukichinjilia mbali haakipo teeeena.

Na
sasa hivi CCM ya J.K. Kikwete ndio kama hivyo tena umeondolewa upepo wooote na kundi lile lile la MAFISADI kwa kulipeleka puta kiti cha spika kwa kutumia REMOTE za kila namna hata kwa mambo ya msingi mno kwa uuma wa Tanzania.

Lakini pamoja na yote walau mmoja katika kundi hilo na mwenye uchungu amejitokeza kusema hadharani mambo yanavyokwenda ovyo mote katika serikali hii ya CCM.

Mambo hivi sasa tambalale fyongo tupu!!! Kumebaki ubinafsi kwa kwenda mbele, fitina na majungu kwa sana si kwa baadhi ya vijana tu na wala sana si kwa akina wazee fulani tu - hali si shwari kule CCM ndio kama hivo tumebainishiwa kila kitu humu.

CCM kwishney na mpango mzima makaratasi za mazingaombwe kupiga kura toka Uchina - kila siri njee kweupe kwa 2015!!!!!!!!!

Ndugu yangu ukiona mgonjwa anaanza ku gasp basi unatakiwa kumweka kitandani ktk mkao mzuri na macho yake kuyafumba ili akate roho vizuri, ila jamani halahala kijiti na jicho kwani kwa mbali namwona Rama mtoa kucha hakubaliani nanyi kabisaa na kaagiza kontena la bisibisi na plaizi toka China
 
Mkiacha ugaidi na utekaji, mkaacha kuibagua zanziba na kuacha siasa za kibaguzi na kibabe mnaweza kupiga hatua lakini hadi sasa mmeloa. Mwigulu, nape na kinana wanakusalimieni

ww najua hutokufa,ila cha moto utakiona...nakuombea uwe hai mpaka chadema watakapoingia ikulu
 
Back
Top Bottom