Ndugu Mchambuzi nakushukuru kwa majibu, ingawa yamezaa maswali mapya.
Binafsi naona kama haujawa clear ni nini hasa unachokisimamia hapa. Maana post zako zina jicontradict hata within the same post.
Ningeshauri ukae chini ujue hasa ni nini conscience yako inakiamini halafu kama ikibidi ubadili ID ili ujadili kwa uhuru mpana fanya hivyo,
maana najua bado unapolitical ambitions na si vizuri kuwaparua wakubwa hasa unapokua na picha yako kwenye forum.
Tuanze na suala la akina Mramba, hapo hapo umesema CCM na serikali yake ilitaka kuwaonesha wananchi kuwa wako serious na vita ya ufisadi. Wakati huohuo Mwenyekiti ameonekana Rombo, Igunga, Bariadi na Monduli akiwanyanyua mkono na kuwaombea kura wagombea wa CCM kwenye uchaguzi mkuu wa 2010, Hata Makongoro Nyerere alipigia sana kelele hili kwenye kikao cha NEC, Aprili. Haingii akilini na haiitaji kwenda shule kuona CCM inawachezea watu kwenye suala la Ufisadi.
Halafu naomba nipingane na wewe, kwenye ukubwa wamNEC na mbunge. Kwa kuangalia mishahara na marupurupu na kwa vyama visivyokua na serikali ni kweli mbunge ni cheo cha juu. Lakini kwa chama chenye kuunda serikali kama CCM. NEC ndiyo chombo kinachounda sera ya kutekelezwa na serikali. Hivyo hata mbunge, midhali umepata ubunge kupitia hicho chama, mNEC atakupangia uende bungeni kupigania mambo gani, lakini siyo vice versa kwamba mbunge anaweza kumpangia mNEC aseme nini au kupigania nini kwenye NEC. Hapo naomba ukajipe maarifa zaidi.
Unamuongelea Nape the whole thread. Nashangaa unamuona Nape anachafua hali ya hewa wakati hata Mwenyekiti wenu kwenye tamasha la Injili alitamka waziwazi kwamba anayoyasema NAPE ndiyo msimamo wa NEC, na hakuna aliyejitokeza kumpinga JK kwa kauli yake hiyo, sasa mkuu mbona unarudia kulekule kwa wapambe wa mafisadi?...unajua Mzee Mwanakijiji aliwahi kusema, Where there is Right or Wrong, Good or Bad, a position of NEUTRALITY is a sign of WEAKNESS. Wewe unataka kuhave your cake and eat it too. CCM ikipasuka sasa haitakua kama unavyofantasize, kwamba ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar, ikipasuka itakua ni CCM pro Mafisadi na CCM against Mafisadi, which side will you take sir?
Unasema Mwenyekiti ni nafasi ya usimamizi tu!!... Please mkuu. Mwenyekiti anaset agenda ya term yake, anaset priority za policy, na ni wajibu wa mwenyekiti kuset ITIKADI ya chama, kwa kutambua dunia inabadilika. Baada ya kujua haya mambo makuu matatu zaidi ya kuongoza vikao, anatakiwa atumie USHAWISHI wake kama mwenyekiti ili yapite kwenye vikao vya maamuzi. Watu wanaposema Mwenyekiti anayumba ni kwa sababu hajatumia ushawishi wake unaoendana na kofia aliyoikalia kupitisha direction ya anapotaka chama kiende.
By the way NEC imeanza kuwa na nguvu kipindi hiki cha Awamu ya nne tu au hata huko nyuma? Na Wenyeviti waliotangulia walikua wanawaandaaje wajumbe kukiwa na very sensitive issue?
Hiyo ya 2012 inawezekana akafanya makubwa, ila kwa kweli its a toss!
Alwatan,
Nashukuru sana kwa mchangi wako mzuri; Kwanza na awali ya yote, sipo humu kutafuta cheo au uongozi; nipo humu kuzungumzia hoja zinazotokana na kukerwa kwangu na chama changu cha CCM kuyumba na msimamo wangu ni kwamba jambo la msingi linayokifanya kuyumba ni yaleyale aliyoyanena Marehemu Kolimba - hakuna dira; hatuna itikadi inayoeleweka, wapo wanaokiongoza kwa kupitia azimio la arusha, na wapo wanaokiongoza kwa kupitia azimio la zanzibar - kisera;
Suala la mimi kubadili ID yangu ili niweze kuzngumza kwa mapana sidhani kana ni jambo la maana kwangu kwani sina
woga au
unafiki katika nayoyazungumza, na hayo ni matatizo makubwa sana katika uongozi wa chama chetu, ukiongezea na
fitina na
ubinafsi;
Kuhusu Mwenyekiti kuwanadi watuhumiwa wa ufisadi katika kampeni, ni hoja yenye mashiko kwani imeshazungumziwa sehemu nyingi vilevile; lakini sote tunaelewa kwanini ilitokea hivyo; vinginevyo suala la msingi hapa ni kwamba utaratibu wa kuwashughulikia hao watuhumiwa ulitakiwa usiwe wa majukwaani, na wangewahi wakati ule kabla ya kampeni kufanyia haya mambo kupitia vikao ambavyo sasa ndio wameamua kufanya hivyo, pengine wangepatikana na hatia na tusingekuwa nao katika uongozi, who knows; vinginevyo as it stood as of October 2010, kwasababu utaratibu huo haukufuatwa, sikuona tatizo la mwenyekiti kwenda kuwainua mikono majimboni; kisiasa inawezekana lilionekana ni usanii, lakini kwa taratibu za chama, ilikuwa ni sahihi kama nilivyokwisha eleza;
Kuhusu Nape, sio kweli ninamuongelea the whole thread lakini kila inapotokea namna hiyo ni sahihi given title ya hii thread kwani
Nafasi ya katibu Itikadi, Siasa na Uenezi na Siasa katika chama cha Siasa ni nyeti na ni kiungo muhimu katika kujenga BRAND ya chama katika siasa za ushindani. Kwahiyo Nape ni Marketing Manager wa CCM; suala la brand equity lipo mikononi mwake, sasa kwanini nisimzungumzie? Nafasi ya katibu mwenezi ni sura ya Chama mbele ya umma, kwahivyo ni muhimu kwa kiongozi wake kuwa mbunifu na kuwa mwepesi wa kusoma mabadiliko ya mazingira ya siasa za nchi ili kuhakikisha kwamba chama kinaenda na wakati na kinakuwa kwenye mstari wakati wote. Ni kosa mimi kusema ni hatari kama anakuwa hana majibu ya uhakika juu ya itikadi ya chama chetu?Ni kosa mimi kuumizwa pale vijana wa UVCCM wanapoimba mbele yake kwamba 'KAULI YETU NI KULINDA SIASA YA UJAMAA NA KUJITEGEMEA' na yeye kutabasamu na kupiga makofi? Suala hili ni timing bomb, na Nape ana nafasi ya ku influence ili haya yabadilike kabla vijana wa UVCCM hawajagundua kwamba kumbe wanadanganywa kwani wanaokaa meza kuu ni mabwanyenye na mabepari yanayofurahia nyimbo za vijana wa UVCCM wakiimba kwa furaha na shangwe kazi yao ni kulinda siasa ya ujamaa na kujitegemea; Kama hulioni tatizo hili, basi ni sahihi kuona kana kwamba ninamuandama Nape;
Vinginevyo, kama umekuwa unanisoma tangu mwanzo, ninachosema kuhusu Nape kimsingi ni kwamba aachane na siasa za mafisadi kwani ni uzao wa azimio la Zanzibar, suala la gamba haliwezi tatuliwa kwa mwendo wa sasa, lazima itikadi zigawanywe; na Nape ana mengi ya kufanya to rebrand the party in public while mengine yanafanyika kwenye vikao;
vinginevyo bila kutenganisha itikadi za vyama, gamba hili sio la kobe au nyoka, ni la kitunguu, uta peal mpaka kitunguu kiishe;
Kuhusu nafasi ya ubunge na MNEC, maelezo yako yamegusa palepale ninapozungumza kwani umeonyesha jinsi gani nafasi ya NEC ina nguvu katika maamuzi ingawa haina maana kwamba ni nafasi ya juu kuliko ubunge; kwahiyo vikumbo vya sasa ni kupigana ili kubaki katika nafasi za maamuzi ya huko tuendako, otherwise wasingekuwa wanahimiza watu kujitoa MNEC bila kujali mtuhumiwa kubakia kwenye ubunge;
Kuhusu Mwenyekiti kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi magumu, upo sahihi lakini mkitoka kwenye vikao, kama watendaji wanaenda tekeleza kinyume inakuwaje? tumesoma kwenye magazeti juzi jinsi gani kiongozi mmoja mzito wa kamati kuu alivyokuwa anapingana na katibu mkuu wake - CCM - Mukama na kufikia hatua ya kutishia kujiuzulu, only to calm down later alipogundua kwamba hata mwenyekiti ana msimamo ule ule; huu ni ushahidi tosha kwamba pamoja na kwamba mwenyekiti kuwa ndiye kiongozi mkuu wa chama, huko chini madudu mengi sana kiutendaji na kiutekelezaji hutokea; solution ya yote haya mimi nadhani ni uchaguzi mkuu wa chama 2012, ingawa nakubaliana nawe kwamba its a toss.