CCM - The Master Magician - na wale wanaosubiri kushangilia!!!

RussianRoulette , umesema ukiwa makini na ukitaka kuelewa utaweza tu! Sasa mimi nataka nikupe taarifa. Nchi ina watu zaidi ya milioni 40 kiasi ambacho wanaona kinachotokea na kugundua kuwa ni mazingaubwe kitaalaum tunajua kuwa ni kama 20% tu!! Na ni kama wakitaka ...The rest wanachukulia kuwa kinachotokea ni reality ...!! Na Viongozi wetu wanahakika ya ushindi wa hao 80% ... Mimi na wewe tuna ujanja gani wa kuwshtua na kuwazindua ... waliolala usingizi wa kimazingaubwe? ... Mind you ..wengi ni wasomi wakubwa!!?.. lakini mazinagubwe kwao ni reality??
Azimio Jipya, just reveal the trick. Mzee Mwanakijiji anajua kua mwanamazingaombwe wowote would rather die than have his trick revealed. So kama wewe unataka magic yake ionekane for what it really is, you just need to reveal the trick: what he did, what accessories helped him achieve the trick and make the 'sensation effect'. Pia tueleze (sisi 80% tunaosema: damn, how did that happen?) what the wizard is trying to achieve.

Just another tip from magic amateurs: Ule mkono unao zunguashwa zunguushwa ni diversion tupu, things are being changed by the unsuspected part: mguu, the other hand, or even (and most of the time) the subject itself: in this case huyo mdada anae badilishwa nguo.
 
Last edited by a moderator:
ngoja niwapeni clue of what is happening maana nadhani watu wengine msiojua mazingaombwe bado mnashangaa; the trick IS NOT in the changing of dresses; the trick is in the dresses!!
 
MM tena hawa jamaa wasivyo na aibu 2015 watawaletea mtu mwingine kutoka humohumo na kudai ni mpya ili wananchi wamchague kuwa rais wa tano. Na wananchi wamekuwa wakiachwa mdomo wazi kwa kila tukio tokea lile la 1985 la 1995 na la 2005. Cha kushangaza baada ya muda mfupi wanatamani mtu mpya.

Juzi nilikuwa naongea na mzee mmoja akaniambia JK hafai kabisa yaani maisha yamekuwa magumu kwelikweli, nikamuuliza ana mtazamo gani akasema anaomba muda wake uishe atoke labla atakayekuja atakuwa na afadhali. Ukiangalia haya ndiyo mazingaombwe wanayoyaonesha kwa watanzania. Ndani ya CCM hakuna jipya, hapo ndipo mwisho wa uwezo wao.
 
Mara ya kwanza kusikia Zitto na hoja yake ya PM. Niliandika kwa kifupi humu neno moja. Na naomba niandike tena:

MAIGIZO.
 
Mie naona hakuna mazingaombwe bali kuna maigizo.

FP, maigizo mara zote unajua watu wanaigiza na watazamaji wanajua wanaigiza; mazingaombwe watu wanaenda zaidi ya kuigiza; wanaaminisha. Yaani, ukitoka kwenye mazingaombwe unabakia ukishangaa na kwa kweli unaweza hata kuja siku ya pili tena kuangalia kwani jibu la "how did they do that?" halijajibiwa. Lakini kwenye maigizo ukiondoka unajua kabisa what happened; hakuna viini macho kwenye maigizo.
 
Duh kali
Kwa hiyo huyo mwanaume ni jk?
Na huyo mdada anasimama kama nani katika tasnia yetu ya siasa? Pinda am salma?

Dah full uongo jamani
 
Mara ya kwanza kusikia Zitto na hoja yake ya PM. Niliandika kwa kifupi humu neno moja. Na naomba niandike tena:MAIGIZO.
Mimi nafikiri ulikuwa karibu na jibu halisi kabisa!!
FP, maigizo mara zote unajua watu wanaigiza na watazamaji wanajua wanaigiza; mazingaombwe watu wanaenda zaidi ya kuigiza; wanaaminisha. Yaani, ukitoka kwenye mazingaombwe unabakia ukishangaa na kwa kweli unaweza hata kuja siku ya pili tena kuangalia kwani jibu la "how did they do that?" halijajibiwa. Lakini kwenye maigizo ukiondoka unajua kabisa what happened; hakuna viini macho kwenye maigizo.
FairPlayer chukulia JK afanikiwe kubadilisha upepo na asiwafukuze mawaziri ambao wabunge wa chama chake mwenyewe na watanzania wanaona kuwa kweli kabisa hawafai ... Wont you say damn, he is good eh .. "How did he do that"
 
Mimi nafikiri ulikuwa karibu na jibu halisi kabisa!! FairPlayer chukulia JK afanikiwe kubadilisha upepo na asiwafukuze mawaziri ambao wabunge wa chama chake mwenyewe na watanzania wanaona kuwa kweli kabisa hawafai ... Wont you say damn, he is good eh .. "How did he do that"
Mwanakijiji nilimuuliza FairPlayer the same question Juzi Jumapili ... kabla siku ya jumatatu haijaeisha ... Tumeyaona sio!!

How did 'they' do it? mchezo ulianza kupangwa Jumamosi; watu wakashangilia na kusubiri kufika j'tatu the who act was completed!!

Watanzania hawajui kiasi gani hili ni tatizo kubwa.

Viongozi wetu wanatuelewa kwa kiasi kikubwa lakini sisi hatuwaelewi kabisa. Wao wanatumia "ukweli wa kimazingaubwe" kwenye shuguli zao za kila siku, wananchi hatambui hilo ... wao wanchukulia "ukweli wa uhakika"

Lini Mtanzania atatambua kuwa si kweli kuwa ukiweka kijiko ndani ya glassi yenye maji Kinapindika na kuwa kikubwa ... Ni kweli inaonekana hivyo lakini sio hakika ... Sasa ukimuona mtu analazimisha kuwa kweli kijiko kimependa unamtibu vipi? Unaweza usimtibu lakini UKAMTUMIA kupitia Ujijnaga na udhaifu wake!!

Viongozi wetu wanatambua kuwa Watanzania ni wa kuchezea kwani wana tatizo la kutofautisha "Ukweli wa hakika" na "ukweli wa kimazingaubwe" na wanutumia udhaifu huu kujinemesha wao na familia zao. Na watafanya hivyo tena na tena!

Kiongozi anakuja mblele ya mhadhara anasimulia jinsi miti inavyokwenda kasi kwa nyuma kila gari linavyoogeza speed ...Watanzania wanapiga makofi wanashangilia na kumtukuza ....Kumbe Kiongozi alikuwa anawapima ujuha wao ..anatambua kweli kuwa ..hapa anamboga za kuzitumia!! Yeye mwenyewe Kimoyo moyo anajuliza hivi kweli wanaamini nilichowaambia ... Anashagaa wala hawashituki ... basi kiburi kinampanda na anaendelea kutesa...na kuendelea kuwa tumia kwani .. ni mazombie tu!!

Nina maana gani .... Baada ya kumalizika kwa bunge ... Rais na PM ... wanajua wamecheza mazingaumbwe wanachekelea kwa namnafulani wanasubiri mwitikio wa wananchi ... kama wamegundua mchezo wetu? wansubiriaaaaa ...lo! Wanagundua kuwa wala hawajshtuka wala hachukui hatua yeyote ...wako kimya wananugunika tu ....wanajua ok ....upepo umepita ...Wanasema next..!! Tuendelee kuwafanya vitoweo ... !!
 
We are trapped.
Okada hah hah ... Your signature say it all ... looks like tumefanyiwa mazingumbwe na master magician wa kutufungua is dead long time ...!!

Lakini unajua nini ...ukifanikiwa kujua kuwa yuo have been plaid ... ina maana that alone is solution by 75%!!! The rest is just take action!!!
 
You are right. basing on the nature of the Tanzanians, business as usual, that is the dilemma...
 
Azimio Jipya, just reveal the trick. Mzee Mwanakijiji anajua kua mwanamazingaombwe wowote would rather die than have his trick revealed. So kama wewe unataka magic yake ionekane for what it really is, you just need to reveal the trick: what he did, what accessories helped him achieve the trick and make the 'sensation effect'. Pia tueleze (sisi 80% tunaosema: damn, how did that happen?) what the wizard is trying to achieve.

Just another tip from magic amateurs: Ule mkono unao zunguashwa zunguushwa ni diversion tupu, things are being changed by the unsuspected part: mguu, the other hand, or even (and most of the time) the subject itself: in this case huyo mdada anae badilishwa nguo.

RussianRoulette you r very right any master magician would rather die than have his trick revealed. Lakini kwenye real life hasa inapokuja kuwa its politics ni vema haya mambo ya kaeleweka vema kwani yanachangia sana kwenye ustawi, afya na maendeleo ya jami! Ni vema kama unataka afya yako na ustawi wako na familia yako viwe under your control lazima uweze kutofautisha Magic tricks and real tricks in life! Vingine you the whole society end up brain washed and manipulated to the worst state this nation has yet to see!! .. You know what am talking about!!

Did you know what gave Hitler all the power to advance about conquering the whole world? Is any Tanzanian really ready to know that?
 
... Kuna wakati tuliambiwa eti serikali "imefuta" mitihani ya kidato cha Pili na watu wakaamini. Lakini Dr. Joyce Ndalichako Mkurugenzai wa Baraza la Mitihani akasisitiza kamba sheria inayomtaka mwanafunzi wa kidato cha Pili ipo pale pale na wala haijafutwa kwani ilitungwa na Bunge na ni bunge linaloweza kuiondoa bado bunge halijaiondoa sheria hiyo.

Mwaka huu eti tumeambiwa tena kwamba serikali "imerudisha" mtihani wa kidato cha Pili na sisi tunaojiita "marafiki wa Elimu" tukaipongeza serikali kwa kitendo chake cha "kurudisha" mitihani ya kidato cha Pili. Haya kama si mazingaombwe ni nini. Inakuwaje jambo la kisheria lililotokana na bunge liondolewe au kurudishwa nje ya taratibu za kibunge?

Haya yanayoendelea bungeni na vugu vugu lote tunaloliona linatokea ni muendelezo wa mazingaombwe na kwa kuwa wahudhuriaji na wapenzi wa siasa za mazingaombwe ni wengi, basi tena ndiyo msemo wa "wengi wape" au msemo wa "mwenye nguvu mpishe" unapotimia. Hivi zitto wakati anapeleka hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu hakujua kwamba kunatakiwa siku kumi na nne ili jambo hilo likubalike kisheria. HAKUJUA??

... Damn... "how did that took place?"
 
Kwa sheria hizi hizi ambazo Dr. Chami amezitumia kujitetea kwamba hana makosa wala mamlaka ya kumuwajibisha Ekelege, then tusitarajie kipya, maana Ekelege atabaki hapo hapo na ufisadi anaofanya utaendelea. Hata akiteuliwa Ekelege Mpya, mianya ya sheria inawaruhusu.

Kesi ya Liyumba serikali ilishindwa baada ya wajumbe kwenda kujiaibisha mahakamani, ni kama vile hawajui wajibu wao. Ukienda Ngorongoro (NCAA), package ya wajumbe wa bodi unaweza kukimbia, sasa unategemea Bodi izuwie kitu na ilihali hawako responsible mahali popote? Bodi nyingi zinateuliwa kwa misingi ya zawadi na ushikaji na ndio maana unakuta akina Msekwa ni Mwenyekiti wa NCAA, hajui hata mambo ya conservation au tourism. Ndio maana mashirika mengi yanakufa. Zama za utawala wa Mkapa, kuna mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco alikuwa na elimu ya darasa la saba tu. Kilichompa ulaji ni upiga debe jimbo la Ubungo.

Ufisadi TAMISEMI utaendelea kwa kuwa hatuna sheria za kuwabana mafisadi wanaotafuna hela huko kwenye halmashauri. Serikali imeweka hayo kwa makusudi ili CCM ikiishiwa iweze kuchota huko.

Ili niwaone wako serious Bunge na serikali waanze zoezi la kupitia sheria zote zenye matobo na Kanuni za Utumishi zenye matobo. Mfano, Idara Kuu ya Utumishi wanasema Waziri na Naibu wake wako entitled kulipwa entertainment allowance kulingana na fungu walilo nalo. Kwanini umpe mtu discretion ya amount ya kujilipa? Huo kama sio ufisadi unalelewa na mfumo ni nini? Kwanini posho nyingine ziwekewe viwango na nyingine zisiwe na viwango?

Wizi mtupu!

Katika makosa ambayo watanzania wengi tunafanya ni kuamini kuwa elimu mtu aliyonayo ndio suluhisho la kila kitu. Bodi za Mashirika ya umma enzi za Nyerere zilijaa watu kama wenye elimu ya msingi Darsa la 7 na chini ya hapo na ndio ziliweza kujenga kwa upande wa TANESCO mitambo na mabwawa ya Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu n.k zikaweza kuendesha Reli ya Kati na kujenga Reli ya TAZARA zikaweza kuanisha AIR TANZANIA na viwanda vyote wenye vilivyojengwa wakati wa utawala wa Nyerere.

Tokea umeingia huu ubaguzi wa kielimu kwa wasio na elimu kubaguliwa ndio tumejenga tabaka la mafisadi wanaouza nchi bila aiibu.

Hebu tujiulize hawa wanaoendesha ufisadi hapa nchini tokea enzi za utawala wa Mwinyi, Mkapa na sasa Kikwete ni wangapi hawana digrii moja, mbili na hata tatu?

Ni bora nchi hii tuirejeshe mikononi mwa wale tunaowabagua kuwa hawana elimu japokuwa kwani wataweza kurejesha maadili ndipo wasomi wataajiriwa kufanya kazi za kitaalamu ili nchi iweze kusomnga mbele.
 
... Damn how "how did that took place?"

Maneno haya yalitamkwa tarehe 10/01/2012, Jisomee!!

SERIKALI imesema kuanzia mwaka huu imerudisha hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, hivyo mwanafunzi atakayepata wastani wa chini ya asilimia 30 hata ruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu, bali ataruhusiwa kukariri darasa mara moja tu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la Serikali la kupandishwa hadhi ya mitihani hiyo na gharama za uendeshaji wa mitihani ya taifa.
Imesema kuwa mwanafunzi atakariri na kushindwa kufikia wastani wa asilimia 30 ataondolewa katika mfumo rasmi wa elimu. Mbali na hilo imesema ina mpango wa kurudisha hadhi mtihani wa darasa la nne, hivyo itatoa maelekezo hapo baadaye baada ya kumalizika kwa uchunguzi.

Aidha imeongeza kuwa wazazi na walezi watapaswa kuchangia gharama za uendeshaji wa mitihani hiyo, ikiwemo mingine ya kitaifa ya kidato cha nne na sita kuanzia mwaka huu. “Kuanzia leo tunarudisha hadhi yake,” alisema Waziri Mulugo.
Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi uliofanyika mwaka jana kubaini kuwa moja ya sababu zilizochangia ufaulu duni wa wanafunzi wa kidato cha nne, mwaka 2010 ni kutokana na kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo hata baada kushindwa kufikia alama ya ufaulu. Uchunguzi Ulifanyika baada ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kuagiza serikali na wadau wengine kufuatilia chanzo cha kushuka kwa ufaulu huo. Waziri Mulugo alisema ufaulu wa kidato cha pili umekuwa ukishuka kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010 hivyo kuashiria wanafunzi na walimu kutofanya bidii za makusudi katika kujifunza na kufundisha.

Akizungumzia kuhusu uchangiaji wa elimu wa gharama za uendeshaji wa mitihani ya Taifa alisema uendeshaji wa mtihani umekuwa mgumu kufutia ongezeko la gharama za uendeshaji linaloendana sambamba na ongezeko la idadi ya shule pamoja na wanafunzi mwaka hadi mwaka, ambapo alitolea mfano wa mtihani wa kidato cha pili gharama za zake ni sh. bilioni sita wakati wa kidato cha nne ni sh. bilioni 27.9. Alisema katika mtihani huo wazazi na walezi watakiwa kuchangia sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali.

Kwa upande wa mitihani ya kidato cha nne na sita wazazi na walezi watapaswa kuchangia sh .35,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali. Katika hatua nyingine Waziri Mulugo alisema serikali inatarajia kutangaza ajira za walimu wa msingi na sekondari mwezi huu , na hivi karibuni itatangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili.

Hii ni ni mara ya pili kwa serikali kurejesha mtihani wa kidato cha pili mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1999 tangu ulipoanzishwa mwaka 1984.

Eti Azimio Jipya haya siyo mazingaombwe!!??
 
Maneno haya yalitamkwa tarehe 10/01/2012, Jisomee!!

SERIKALI imesema kuanzia mwaka huu imerudisha hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, hivyo mwanafunzi atakayepata wastani wa chini ya asilimia 30 hata ruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu, bali ataruhusiwa kukariri darasa mara moja tu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la Serikali la kupandishwa hadhi ya mitihani hiyo na gharama za uendeshaji wa mitihani ya taifa.
Imesema kuwa mwanafunzi atakariri na kushindwa kufikia wastani wa asilimia 30 ataondolewa katika mfumo rasmi wa elimu. Mbali na hilo imesema ina mpango wa kurudisha hadhi mtihani wa darasa la nne, hivyo itatoa maelekezo hapo baadaye baada ya kumalizika kwa uchunguzi.

Aidha imeongeza kuwa wazazi na walezi watapaswa kuchangia gharama za uendeshaji wa mitihani hiyo, ikiwemo mingine ya kitaifa ya kidato cha nne na sita kuanzia mwaka huu. "Kuanzia leo tunarudisha hadhi yake," alisema Waziri Mulugo.
Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi uliofanyika mwaka jana kubaini kuwa moja ya sababu zilizochangia ufaulu duni wa wanafunzi wa kidato cha nne, mwaka 2010 ni kutokana na kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo hata baada kushindwa kufikia alama ya ufaulu. Uchunguzi Ulifanyika baada ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kuagiza serikali na wadau wengine kufuatilia chanzo cha kushuka kwa ufaulu huo. Waziri Mulugo alisema ufaulu wa kidato cha pili umekuwa ukishuka kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010 hivyo kuashiria wanafunzi na walimu kutofanya bidii za makusudi katika kujifunza na kufundisha.

Akizungumzia kuhusu uchangiaji wa elimu wa gharama za uendeshaji wa mitihani ya Taifa alisema uendeshaji wa mtihani umekuwa mgumu kufutia ongezeko la gharama za uendeshaji linaloendana sambamba na ongezeko la idadi ya shule pamoja na wanafunzi mwaka hadi mwaka, ambapo alitolea mfano wa mtihani wa kidato cha pili gharama za zake ni sh. bilioni sita wakati wa kidato cha nne ni sh. bilioni 27.9. Alisema katika mtihani huo wazazi na walezi watakiwa kuchangia sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali.

Kwa upande wa mitihani ya kidato cha nne na sita wazazi na walezi watapaswa kuchangia sh .35,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali. Katika hatua nyingine Waziri Mulugo alisema serikali inatarajia kutangaza ajira za walimu wa msingi na sekondari mwezi huu , na hivi karibuni itatangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili.

Hii ni ni mara ya pili kwa serikali kurejesha mtihani wa kidato cha pili mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1999 tangu ulipoanzishwa mwaka 1984.

Eti Azimio Jipya haya siyo mazingaombwe!!??
Kigarama,

Binafsi sifikiri ni heshima wala hekima kwa Mtaalam au tuseme Mtu mzima kumchezea Mtu mwingine Mazingaubwe na kumuaminisha kuwa anampa huduma au anamtendea haki ya jambo fulani. Ukiangalia kilichotokea pale bungeni kwa mara ya kwanza ni Watu wajasiri na wanaojiheshimu wameweza Kusimama kidete na kusema ..NO! That Is Magical Trick ..No no That is Just an Illusion! NO! We cant take it any more!!

Unafahamu kama Magical trick zinafanywa kama viburidisho majukwaani na kuchukuliwa kama mizaha ya kupoteza muda hilo halina Tatizo!! Lakini Kila wizara inapotumia mbinu hiyo ya kiini macho na kuchezea taifa zima hilo ni tatizo kubwa. Ukianagalia mfano uliouleta hapo wa mfumo wa shule zetu ... Hivi ianwezekanaje kweli hiyo kutokea na hakuna wa kusema NO ... We cant take more than this?

Swali la msingi inakuwaje Mazingaumbwe ambayo ni sanaa za michezo ya kuburudisha vinafanyika mbele ya macho ya Mtanzania na bado haoni kabisa ...? Kwa nini taifa linapenda kushikilia Mazingaumbwe/Magical tricks kama ukweli na kufubaa kwa upole na kukumbatia mizaha hiyo kama ndio njia ya kwenda peponi au kutuletea maendeleo ya kweli? Nani anajua namna ya kuwazindua watu toka kwenye Tatizo hili??? Kigarama au una dondoo ya ... the way Out?

Huu ugonjwa wa kuchukulia Mazinagubwe/Iluusions/Magical trikcs kama msingi wa maendeleo wa Taifa letu ... Unatibiwaje??????!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom