CCM - The Master Magician - na wale wanaosubiri kushangilia!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM - The Master Magician - na wale wanaosubiri kushangilia!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 21, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mazingaombwe ni mazingaombwe; mwanamazingaombwe mzuri ni yule ambaye anaweza kuaminisha watu kuwa kitu ambacho hakipo kipo na kile ambacho kipo hakipo. Lengo la mwanamazingaombwe yoyote yule ni hatimaye kuwafanya watazamaji wake waseme "how did he do that?" yaani wapigwe na mshangao na wasimame kwa pamoja midomo ikiwa wazi wakipiga makofi ya kumpongeza.

  Niliwahi kuandika kwa kirefu sana hili la mazingaombe - I myself being an amateur in the art -kuwa siasa za TZ zimefunikwa na mazingaombwe ya kila namna ambayo watu wengi hujikuta wanashangilia bila kujiuliza sana kuwa ni nini kimetokea. Wapo ambao wanaweza kabisa kuaminisha - hata kwa kiapo ikibidi - kuwa kilichotokea siyo mazingaombwe kabisa kwani 'waliona mbele ya macho yao' mchanga ukigeuzwa kuwa sukari!!

  Naomba uangalia onesho hili la mazingaombwe ili uelewe ni nini kinaendelea katika siasa za "kujiuzulu"!

  Guess what?
  Wakijiuzulu mawaziri wote wa CCM, mawaziri wengine watatokawapi? CCM na ni kwenye Bunge hili hili!!!

  Illusion per excellence!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hakuna jinsi. labda bunge likivunjika ufanyike uchaguzi mwingine.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hahahaaa! Mwanakijiji bana, sii wanajivua gamba jamani? au nyoka ni nyoka tu habadiliki kuwa Kenge.....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  hapa hakuna mazingaombwe ya 'aina yake'
  ni yale yale ya siku zote....mazingaombwe too common...
  cha ajabu yana washabiki bado
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  unajua kuna raha yake wakati mwingine kuangalia wanachofanya hawa wanamazingaombwe; unaweza kujikuta unakirudia mara kwa mara
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mmmh! Nyoka hafi hadi upige kichwa chake.
   
 7. U

  Uswe JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  well said MM, ingawa pia nina imani kubwa kwamba baadhi ya wanaCCM wanaweza kufanya kazi vizuri japo kidogo kuliko hawa, nitataja wawili Filikunjombe na Makamba, hebu wapewe wizara hawa watu
   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa sheria hizi hizi ambazo Dr. Chami amezitumia kujitetea kwamba hana makosa wala mamlaka ya kumuwajibisha Ekelege, then tusitarajie kipya, maana Ekelege atabaki hapo hapo na ufisadi anaofanya utaendelea. Hata akiteuliwa Ekelege Mpya, mianya ya sheria inawaruhusu.

  Kesi ya Liyumba serikali ilishindwa baada ya wajumbe kwenda kujiaibisha mahakamani, ni kama vile hawajui wajibu wao. Ukienda Ngorongoro (NCAA), package ya wajumbe wa bodi unaweza kukimbia, sasa unategemea Bodi izuwie kitu na ilihali hawako responsible mahali popote? Bodi nyingi zinateuliwa kwa misingi ya zawadi na ushikaji na ndio maana unakuta akina Msekwa ni Mwenyekiti wa NCAA, hajui hata mambo ya conservation au tourism. Ndio maana mashirika mengi yanakufa. Zama za utawala wa Mkapa, kuna mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco alikuwa na elimu ya darasa la saba tu. Kilichompa ulaji ni upiga debe jimbo la Ubungo.

  Ufisadi TAMISEMI utaendelea kwa kuwa hatuna sheria za kuwabana mafisadi wanaotafuna hela huko kwenye halmashauri. Serikali imeweka hayo kwa makusudi ili CCM ikiishiwa iweze kuchota huko.

  Ili niwaone wako serious Bunge na serikali waanze zoezi la kupitia sheria zote zenye matobo na Kanuni za Utumishi zenye matobo. Mfano, Idara Kuu ya Utumishi wanasema Waziri na Naibu wake wako entitled kulipwa entertainment allowance kulingana na fungu walilo nalo. Kwanini umpe mtu discretion ya amount ya kujilipa? Huo kama sio ufisadi unalelewa na mfumo ni nini? Kwanini posho nyingine ziwekewe viwango na nyingine zisiwe na viwango?

  Wizi mtupu!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hamuwapendi wenzenu; gari likishaharibika haijalishi dereva anayeendesha ana ujuzi gani
   
 10. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Bosi...

  HUjawahi kuangali movie ya komedi zaidi ya mara tatu na bado ukacheka???
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Leo nimekaa nikawaza sana, halafu wazo moja la kijinga likanijia

  "kama uchawi upo active, basi umepiga camp Tanzania, haiwezekani wenye dhamana wote kuwa kama wamepigwa butwaa kiasi cha kutojua kwamba tulipofikia hapahitaji tena siasa"

  ATI HATA EKELEGE NAYE TUNAMJADILI MIEZI NENDA MIEZI RUDI!!! THERE MUST BE SOMETHING BEYOND OUR NATURAL SELVES
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  Ni kweli amekosekana mkereketwa jasiri mshika korombo akayabobonyoa haya magamba-gandamizi sugu na korofi
  KWA NGUVU
  ? Kubembelezana mpaka lini wakati nyoka wetu mpendwa anazidi kudhoofika? Kipi ni cha muhimu zaidi: magamba machafu yaliyopauka na kumaliza muda wake au afya ya nyoka wetu mpendwa? Aiiii !!!…

  [​IMG]


   
 13. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Damn! How did they do that?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  exactly!!! wakikuambia jinsi walivyofanya haitakuwa magic! Remember macho yanadanganyika kirahisi zaidi kuliko kitu kingine chochote!
   
 15. Kwisimla

  Kwisimla Senior Member

  #15
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  probably u r right, mimi pia nimefikiria na kujiuliza hiki kitu mara nyingi. Haiwezekani watu wanalalamika weeee... na hakuna hata hatua moja serikali inachukua.
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na kwa kawaida!

  Watazama mazingaunbwe wengi wanapenda kushikilia na kutaka kuendeleza kuwa walichokiona ni kweli na hakika. Wale waliozidiwa na ulimbukeni Hypnotic zombies ... wanapenda zaidi "ukweli wa kimazingaubwe" ndio utawale maisha yao ya kila siku zaidi ya "ukweli halisi usio kuwa wa kimazingaumbwe"!

  Nina maana wanataka kuona kuwa ukweli wa kujiuzulu mawaziri sio mazingaumbwe ila ni ukweli halisi usiokuwa wa kimazngaubwe...! Watapenda kuona hivyo hata milele na kumbuka hili linavyompa nguvu mcheza mazingaumbwe!!

  Lakini its just an illusion!!

  Lakini hata ukiwadadavulia hatua kwa hatua kuwa jamani hii ni janja ya macho tu hakuna ukweli wowote.. kama kwenye clip hii hapa hatakubali!! Wanapendezwa na uwongo kuliko ukweli!!!  Unapokuwa na jamii iliyopofuka kiasi hiki ... Unaiamsha je?

  Unawapeleka shule ili waelimike zaidi au?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kumbe wewe makali wa baiolojia, karibu huku kwetu tumepungukiwa waalimu ... Ni kweli Kuvua gamba hakubadilishi jenietik! Lol!!

  Lakini Mimi niulize swali lisilo la kisomi kabisa ...!!

  Hivi unapokuwa na mgonjwa "anayesisitiza" kuwa ni kweli na ni hakika kuwa akiwa ndani ya gari vilivyo nje navyo pia vinakuwa kwenye mwendo sawa na wa gari lakini kwa kinyume ... Unamtibu vipi?

  Ukizubaa kabla hujapata dawa ... Mara unasikia ugonjwa umesabaa na baraza la mawaziri nalo nimeathirika wanakuwa na Mtizamo huo huo ... Wanakuwa na lugha ya kiutendaji inayoashiria kuwa wanaamini kuwa Miti na nyumba navyo hua vinakuwa kwenye mwendo ..kwa kuwa tu aliye ndani ya gari yuko kwenye mwendo... yaani wanaami ukweli wa mazingaubwe kama sehemu ya maisha na msingi wa kufanyia kazi zao!!

  Mkandara unapogundua kuwa baraza lako la mawaziri linafikiria kwa dhana hiyo, linapanga bajeti kwa dhana hiyo, waziri wa afya, kilimo, mawasiliano, tamisemi nk wanafikiria, lugha yao na kuona kwao ni namna hiyo ... unawafanya nini?

  Vibaya zaidi ... Wananchi hajawagundua ... wanaendelea kuwaunga mkono ..!!!

  Binafsi nashangaa walifikiaji kuwa na nyadhifa hizo!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Makamba yupi huyu? Yusufu, January au Mwanvita?
   
 19. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #19
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji hoja uliyoitoa inahitaji sana tafakuri ya kina jambo ambalo sisi watanzania tulishaachana nalo zamani sana!!

  Kuna wakati tuliambiwa eti serikali "imefuta" mitihani ya kidato cha Pili na watu wakaamini. Lakini Dr. Joyce Ndalichako Mkurugenzai wa Baraza la Mitihani akasisitiza kamba sheria inayomtaka mwanafunzi wa kidato cha Pili ipo pale pale na wala haijafutwa kwani ilitungwa na Bunge na ni bunge linaloweza kuiondoa bado bunge halijaiondoa sheria hiyo.

  Mwaka huu eti tumeambiwa tena kwamba serikali "imerudisha" mtihani wa kidato cha Pili na sisi tunaojiita "marafiki wa Elimu" tukaipongeza serikali kwa kitendo chake cha "kurudisha" mitihani ya kidato cha Pili. Haya kama si mazingaombwe ni nini. Inakuwaje jambo la kisheria lililotokana na bunge liondolewe au kurudishwa nje ya taratibu za kibunge?

  Haya yanayoendelea bungeni na vugu vugu lote tunaloliona linatokea ni muendelezo wa mazingaombwe na kwa kuwa wahudhuriaji na wapenzi wa siasa za mazingaombwe ni wengi, basi tena ndiyo msemo wa "wengi wape" au msemo wa "mwenye nguvu mpishe" unapotimia. Hivi zitto wakati anapeleka hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu hakujua kwamba kunatakiwa siku kumi na nne ili jambo hilo likubalike kisheria. HAKUJUA??
   
 20. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  2015 mwisho wao.
   
Loading...