Azimio Jipya, just reveal the trick. Mzee Mwanakijiji anajua kua mwanamazingaombwe wowote would rather die than have his trick revealed. So kama wewe unataka magic yake ionekane for what it really is, you just need to reveal the trick: what he did, what accessories helped him achieve the trick and make the 'sensation effect'. Pia tueleze (sisi 80% tunaosema: damn, how did that happen?) what the wizard is trying to achieve.RussianRoulette , umesema ukiwa makini na ukitaka kuelewa utaweza tu! Sasa mimi nataka nikupe taarifa. Nchi ina watu zaidi ya milioni 40 kiasi ambacho wanaona kinachotokea na kugundua kuwa ni mazingaubwe kitaalaum tunajua kuwa ni kama 20% tu!! Na ni kama wakitaka ...The rest wanachukulia kuwa kinachotokea ni reality ...!! Na Viongozi wetu wanahakika ya ushindi wa hao 80% ... Mimi na wewe tuna ujanja gani wa kuwshtua na kuwazindua ... waliolala usingizi wa kimazingaubwe? ... Mind you ..wengi ni wasomi wakubwa!!?.. lakini mazinagubwe kwao ni reality??
Siamini macho yangu
Mie naona hakuna mazingaombwe bali kuna maigizo.
Mimi nafikiri ulikuwa karibu na jibu halisi kabisa!!Mara ya kwanza kusikia Zitto na hoja yake ya PM. Niliandika kwa kifupi humu neno moja. Na naomba niandike tena:MAIGIZO.
FairPlayer chukulia JK afanikiwe kubadilisha upepo na asiwafukuze mawaziri ambao wabunge wa chama chake mwenyewe na watanzania wanaona kuwa kweli kabisa hawafai ... Wont you say damn, he is good eh .. "How did he do that"FP, maigizo mara zote unajua watu wanaigiza na watazamaji wanajua wanaigiza; mazingaombwe watu wanaenda zaidi ya kuigiza; wanaaminisha. Yaani, ukitoka kwenye mazingaombwe unabakia ukishangaa na kwa kweli unaweza hata kuja siku ya pili tena kuangalia kwani jibu la "how did they do that?" halijajibiwa. Lakini kwenye maigizo ukiondoka unajua kabisa what happened; hakuna viini macho kwenye maigizo.
Mwanakijiji nilimuuliza FairPlayer the same question Juzi Jumapili ... kabla siku ya jumatatu haijaeisha ... Tumeyaona sio!!Mimi nafikiri ulikuwa karibu na jibu halisi kabisa!! FairPlayer chukulia JK afanikiwe kubadilisha upepo na asiwafukuze mawaziri ambao wabunge wa chama chake mwenyewe na watanzania wanaona kuwa kweli kabisa hawafai ... Wont you say damn, he is good eh .. "How did he do that"
How did 'they' do it? mchezo ulianza kupangwa Jumamosi; watu wakashangilia na kusubiri kufika j'tatu the who act was completed!!
Okada hah hah ... Your signature say it all ... looks like tumefanyiwa mazingumbwe na master magician wa kutufungua is dead long time ...!!We are trapped.
Okada hah hah ... Your signature say it all ... looks like tumefanyiwa mazingumbwe na master magician wa kutufungua is dead long time ...!!
Lakini unajua nini ...ukifanikiwa kujua kuwa yuo have been plaid ... ina maana that alone is solution by 75%!!! The rest is just take action!!!
Azimio Jipya, just reveal the trick. Mzee Mwanakijiji anajua kua mwanamazingaombwe wowote would rather die than have his trick revealed. So kama wewe unataka magic yake ionekane for what it really is, you just need to reveal the trick: what he did, what accessories helped him achieve the trick and make the 'sensation effect'. Pia tueleze (sisi 80% tunaosema: damn, how did that happen?) what the wizard is trying to achieve.
Just another tip from magic amateurs: Ule mkono unao zunguashwa zunguushwa ni diversion tupu, things are being changed by the unsuspected part: mguu, the other hand, or even (and most of the time) the subject itself: in this case huyo mdada anae badilishwa nguo.
... Kuna wakati tuliambiwa eti serikali "imefuta" mitihani ya kidato cha Pili na watu wakaamini. Lakini Dr. Joyce Ndalichako Mkurugenzai wa Baraza la Mitihani akasisitiza kamba sheria inayomtaka mwanafunzi wa kidato cha Pili ipo pale pale na wala haijafutwa kwani ilitungwa na Bunge na ni bunge linaloweza kuiondoa bado bunge halijaiondoa sheria hiyo.
Mwaka huu eti tumeambiwa tena kwamba serikali "imerudisha" mtihani wa kidato cha Pili na sisi tunaojiita "marafiki wa Elimu" tukaipongeza serikali kwa kitendo chake cha "kurudisha" mitihani ya kidato cha Pili. Haya kama si mazingaombwe ni nini. Inakuwaje jambo la kisheria lililotokana na bunge liondolewe au kurudishwa nje ya taratibu za kibunge?
Haya yanayoendelea bungeni na vugu vugu lote tunaloliona linatokea ni muendelezo wa mazingaombwe na kwa kuwa wahudhuriaji na wapenzi wa siasa za mazingaombwe ni wengi, basi tena ndiyo msemo wa "wengi wape" au msemo wa "mwenye nguvu mpishe" unapotimia. Hivi zitto wakati anapeleka hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na Imani Waziri Mkuu hakujua kwamba kunatakiwa siku kumi na nne ili jambo hilo likubalike kisheria. HAKUJUA??
Kwa sheria hizi hizi ambazo Dr. Chami amezitumia kujitetea kwamba hana makosa wala mamlaka ya kumuwajibisha Ekelege, then tusitarajie kipya, maana Ekelege atabaki hapo hapo na ufisadi anaofanya utaendelea. Hata akiteuliwa Ekelege Mpya, mianya ya sheria inawaruhusu.
Kesi ya Liyumba serikali ilishindwa baada ya wajumbe kwenda kujiaibisha mahakamani, ni kama vile hawajui wajibu wao. Ukienda Ngorongoro (NCAA), package ya wajumbe wa bodi unaweza kukimbia, sasa unategemea Bodi izuwie kitu na ilihali hawako responsible mahali popote? Bodi nyingi zinateuliwa kwa misingi ya zawadi na ushikaji na ndio maana unakuta akina Msekwa ni Mwenyekiti wa NCAA, hajui hata mambo ya conservation au tourism. Ndio maana mashirika mengi yanakufa. Zama za utawala wa Mkapa, kuna mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco alikuwa na elimu ya darasa la saba tu. Kilichompa ulaji ni upiga debe jimbo la Ubungo.
Ufisadi TAMISEMI utaendelea kwa kuwa hatuna sheria za kuwabana mafisadi wanaotafuna hela huko kwenye halmashauri. Serikali imeweka hayo kwa makusudi ili CCM ikiishiwa iweze kuchota huko.
Ili niwaone wako serious Bunge na serikali waanze zoezi la kupitia sheria zote zenye matobo na Kanuni za Utumishi zenye matobo. Mfano, Idara Kuu ya Utumishi wanasema Waziri na Naibu wake wako entitled kulipwa entertainment allowance kulingana na fungu walilo nalo. Kwanini umpe mtu discretion ya amount ya kujilipa? Huo kama sio ufisadi unalelewa na mfumo ni nini? Kwanini posho nyingine ziwekewe viwango na nyingine zisiwe na viwango?
Wizi mtupu!
... Damn how "how did that took place?"
Kigarama,Maneno haya yalitamkwa tarehe 10/01/2012, Jisomee!!
SERIKALI imesema kuanzia mwaka huu imerudisha hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, hivyo mwanafunzi atakayepata wastani wa chini ya asilimia 30 hata ruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu, bali ataruhusiwa kukariri darasa mara moja tu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tamko la Serikali la kupandishwa hadhi ya mitihani hiyo na gharama za uendeshaji wa mitihani ya taifa.
Imesema kuwa mwanafunzi atakariri na kushindwa kufikia wastani wa asilimia 30 ataondolewa katika mfumo rasmi wa elimu. Mbali na hilo imesema ina mpango wa kurudisha hadhi mtihani wa darasa la nne, hivyo itatoa maelekezo hapo baadaye baada ya kumalizika kwa uchunguzi.
Aidha imeongeza kuwa wazazi na walezi watapaswa kuchangia gharama za uendeshaji wa mitihani hiyo, ikiwemo mingine ya kitaifa ya kidato cha nne na sita kuanzia mwaka huu. "Kuanzia leo tunarudisha hadhi yake," alisema Waziri Mulugo.
Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi uliofanyika mwaka jana kubaini kuwa moja ya sababu zilizochangia ufaulu duni wa wanafunzi wa kidato cha nne, mwaka 2010 ni kutokana na kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo hata baada kushindwa kufikia alama ya ufaulu. Uchunguzi Ulifanyika baada ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kuagiza serikali na wadau wengine kufuatilia chanzo cha kushuka kwa ufaulu huo. Waziri Mulugo alisema ufaulu wa kidato cha pili umekuwa ukishuka kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010 hivyo kuashiria wanafunzi na walimu kutofanya bidii za makusudi katika kujifunza na kufundisha.
Akizungumzia kuhusu uchangiaji wa elimu wa gharama za uendeshaji wa mitihani ya Taifa alisema uendeshaji wa mtihani umekuwa mgumu kufutia ongezeko la gharama za uendeshaji linaloendana sambamba na ongezeko la idadi ya shule pamoja na wanafunzi mwaka hadi mwaka, ambapo alitolea mfano wa mtihani wa kidato cha pili gharama za zake ni sh. bilioni sita wakati wa kidato cha nne ni sh. bilioni 27.9. Alisema katika mtihani huo wazazi na walezi watakiwa kuchangia sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali.
Kwa upande wa mitihani ya kidato cha nne na sita wazazi na walezi watapaswa kuchangia sh .35,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali. Katika hatua nyingine Waziri Mulugo alisema serikali inatarajia kutangaza ajira za walimu wa msingi na sekondari mwezi huu , na hivi karibuni itatangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili.
Hii ni ni mara ya pili kwa serikali kurejesha mtihani wa kidato cha pili mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1999 tangu ulipoanzishwa mwaka 1984.
Eti Azimio Jipya haya siyo mazingaombwe!!??