CCM tatizo ni Sitta na genge lake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM tatizo ni Sitta na genge lake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjenda Chilo, Jul 22, 2011.

 1. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Wandugu, ni mawazo tu, mi nafikiri tatizo litakaloiua CCM si ufisadi bali ni makamanda feki wa kupinga ufisadi, kisa uwaziri mkuu machungu yakazidishwa na uspika. vita vya panzi na furaha ya kunguru. matokeo yake ndo haya tunayoyaona hakuna vita halisi juu ya ufisadi. Ningekuwa presida ningeanza nae potelea pote.
   
 2. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  ndio hivyo presida wa jmt ni jakaya m. Kikwete sio ww
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mfumo mbovu ,uzembe,wizi na ufisadi,kukosa uongozi bora,unafiki na ufitini unameshakimaliza chama hakuna namna watajiokoa tena
   
 4. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mwenyekiti wa chama chenu hawawezi kugusa maana sasa Sitta ana nguvu kuliko wakati wowote poleni sana.
   
 5. m

  morganbingo Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  We umepewa hela na mafisadi nini. KAma umeshiba maharage nenda kalale sio unatuletea upuuzi hapa. Sitta ni mtuu pekee aliyewapinga mafisadi bila kuogopa sasa wewe unataka awakenulie meno huku moyoni analia kama mlivyo watz wengi!!!!
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena vema. Sitta ndio chanzo cha vurugu kwenye Chama cha Mapinduzi. Pamoja na kupewa uwaziri lakini bado anaipinga serikali amesahau collective responsibility. Kama ni kamanda kweli wa ufisadi na anajua serikali ni ya kifisadi asingekubali kuwa waziri angebaki tu back bencher ili aisimamie na kuikosoa vizuri serikali akiwa nje ya serikali lakini amekumbatia uwaziri na huku anaikosoa serikali. Kama si undumila kuwili ni nini. Mkuu ningekuwa mimi Rais ningemfukuza kupitia radioni na kama noma na iwe noma!! Huwezi kukaa na watu kama sitta serikalini wangebaki nje tu hawa. Eti kamanda wa kupigana vita dhidi ya ufisadi kumbe ni kamanda wa kupigania maslahi binafsi!
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona tunasahau kirahisi? Hivi kujenga ofisi ya spika jimboni kwa mbunge si ufisadi? Hivi kupigia upatu maposho lukuki ya wabunge si ufisadi huo?
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Pole sana ndugu kama bado umenasa kwenye mtego wa Sitta, huyu Sitta ni sawa na popo si ndege na wala si mnyama, Sitta ni fisadi kama walivyo mafisadi wengine ndani ya ccm, chunguza kwa makini malengo ya kisiasa ya Sitta na fuatilia kwa makini maisha anayoishi ndio utaujuwa upande wa pili wa huyu mnafki.

  Kama hujui ngoja niongee na wewe kwa lugha rahisi, Samuel Sitta na Zitto Kabwe sio wanasiasa wa kuwaamini katika nchi hii. wapo wengi lakini hao ndio good sample. hawa ni wanasiasa wanafki kuliko maelezo ambao walifanikiwa kuziteka akili za Watanzania kwamba wako upande wa Umma kumbe tumeliwa, usiwaamini kabisa watu hawa ni hatari kwa Taifa.
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Kamanda Sitta akisikiliza kwa makini hotuba bungeni.
  ccm cham cha mazuzu***** na watu wenye akili za kawaida na mbaya kabisa, Sitta kilema wa ufahamu, na hao wengine ni watu wasio aminika kabisa, hiko ni chama kinachoangamia ....! kazi yao malumbano,. kelele na rushwa kama si Ufisadi
  [​IMG]
   
 10. M

  Makupa JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Rais wa Jumahuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama tawala CCM TUNAKUOMBA umtimue huyu BABU SITA kwenye baraza la mawaziri na hata kama ikiwezekana anyanganywe kadi ya CCM
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Umenena vyema Matola,ni wengi walinasa kwenye mtego wa Sitta kumbe anachokiongea siyo anachokifanya kwa kifupi yeye ndio mnafiki nambari wani,huwezi kuishi kwenye nyumba ya spika wakati wewe siyo spika afu bado ukaona ni sahihi..

  Hawa viongozi ndio wakwanza kuvunja kanuni na miongozo mbalimbali wakijua kwamba kwa mifumo waliyoiasisi wao haiwezi kuwashughulikia,tunapoongelea Katiba mpya tushuke na chini kujadili upya kanuni zinanazosimamia maadili ya utumishi wa umma kwa hawa viongozi waandamizi huku mkazo ukiwekwa kwa adhabu kali kwa wote watakaokiuka...
   
 12. CHIMPANZEE

  CHIMPANZEE Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Kinachotakiwa ni kuvunja baraza lote kisha kuchagua ambao hawajawahi kushika madaraka, mbona CCM ina wabunge wengi?
   
 13. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  kama unataka kujua sita ni fisadi kiasi gani,kaulize jimboni kwake alivyokuwa akigawa hela kipindi cha kampeni! wasalaam
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Sitta ilikuwa anyang'anywe kadi kule Dodoma lakini akalia kinafiki na kuomba msamaha!! Kweli Rais asipomfuta kazi atakuwa hatendi haki. SItta ni wa kufutwa kazi tu
   
 15. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwani Sitta wako Mwadilifu!?Hana anachopigania zaidi ya Kuwadanganya wasiojua Kupima Mambo,Sita ana Sura 2
  1)Kutaka aonekane mpigania wanyonge na Mali za Umma
  2)Mpenda Raha kwa Kutumia fedha za Umma!

  Muulize sitta yeye ni Spika?Alipoona Uspika umeisha kwanini ang'ang'anie nyumba inayolipiwa Shs 12Million kwa mwezi kwa ajili ya spika wakati yeye sio spika?
  Sita hakuna kitu ndio wale wale! lA CCJ sisemi
   
 16. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,638
  Likes Received: 4,746
  Trophy Points: 280

  Hapa bila ya shaka yoyote alikuwa anaota anapigiwa mizinga 21. Hizi mbio za urais wa 2015 ndiyo kaburi la CCM. RIP CCM
   
 17. jasirimali

  jasirimali Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa unataka akae Daslama halafu jimboni kwake utakaa wewe?
   
 18. MWAGONA

  MWAGONA Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa ndio sehemu ya kuonesha mawazo tofauti lakini yenye kutuelekeza kwenye fact.Mimi nitatofautiana kidogo na mtoa hoja kwa kusema sitta cyo chazo cha tatizo siyo sita ila ni kuwa Mwisho wa CCM ndio unafika au ndio unaenda kufika tukikumbuka kufall kwa state za Afrika za kina mali soghai na nyingine.mwanzo wake zili kuwa maarufu kama ccm lakini mwisho wa siku zikaanguka tukubali tusikubali kufall kwa ccm kumefika,nani alifikili kuwa nchi za kiarabu zitafanya mabadiliko kama yanayo endelea,hivyo Sitta,mwakyembe,lowasa na wengine wengi watasaidia mwisho wa ccm ufike na Msemo wa kuwa Tanzania bila CCM inawezekana.kukataliwa kwa bajeti ya umeme hiyo ni dalili tosha coz tumezoea ninaunga Bajeti aslimia zaidi ya miamoja, coz waliogopa kuwa wangepigwa mawe na wale walio wachagua ccm.
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hapo ulipo jibu ni tosha kabisa ingawa nami ni CCM, nadhani kuna dhana moja ambayo CCM inajisahau siku zote wao wana dhani bado tuko na zidumu fikra za mwenyekiti no none tuko karne nyingine sasa Democrasia imekuwa, Pili dhani nyingine ni ile CCM wao ni kulinda Chama inamaana chama hakijitegemei inamaana chama hakina mfumo wa kujiendesha kama chama pekee inapo fika mahali chama kinatakiwa kijijue ni chama cha wananchi wanao kisupport na kama kina ongoza nchi kitambue kimebeba mzigo mkubwa wa wananchi bila kuangalia itikadi zao,

  sasa tukirudi hapo kwa ndugu yangu anaposema Sitta ndi chanzo sijakuelewa kabisa inapo bidi kuipinga serikali yako pinga hata kama umo ndani ya chama au serikali yako hapo wewe unge mwambia tu sitta labda kwani usijitoe katika nyazifa na ukabaki kuwa mwanachama na ukapinga zaidi ili kuwaeleza watu nini dhamila yako kama mwalimu alivyo jitoa bungeni kwenye serikali ya mkoloni kabla ya uhuru na akaenda kwa wananchi kuwaeleza serikali haikubaliani na mawazo yangu ambayo yatwasaidia wananchi bali serikali inataka minifanya visivyo.

  CCM inakufa yenyewe na viongozi wake walipo madarakani kwa kutokuwa na Uaminifu kwa wananchi, Uadilifu wa kuwa kiongozi na dhamila ya kweli kwa nchi na kukosekana kwa uzalendo ndani ya viongozi wetu na ndilo hilo jinamizi linawatafuna viongozi wa CCM kila kukicha ni kurumbana na mbaya zaidi Kulikana Azimio la Arusha ambalo lilitaka marekebisho madogo tuu na wange songa mbele zaidi.matokeo yake ndio haya Ufisadi umekithili viongozi hao hao ndio wamiliki njia kuu zote za uchumi wanaiongoza serikali kama miradi yao binafsi.

  Usi mlaumu sitta laumu mfumo mzima wa uongozi wa CCM yetu ilipotufikisha
   
Loading...