CCM: Taarifa za miradi ziwekwe wazi Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba,

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
[h=2][/h] Ijumaa, Novemba 30, 2012 05:20 Na Audax Mutiganzi, Bukoba


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera, kimeiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, kutoa taarifa sahihi kwa wananchi juu ya miradi inayotekelezwa na itakayotekelezwa.

Agizo hilo lilitolewa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kagera, Costancia Buhiye, kwamba kumekuwa na usiri mkubwa wa taarifa za utekelezaji wa miradi.

Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, ihakikishe inatoa taarifa sahihi kwa wananchi, juu ya miradi ya upimaji wa viwanja 5,000, mradi wa ujenzi wa soko kuu la kisasa la Bukoba na kituo cha mabasi.

Alisema CCM kimefikia uwamuzi wa kutoa agizo hilo, baada ya kupokea kwa mguso wa aina ya kipekee hali ya siasa na kiuongozi iliyojitokeza mkoani humo.

Alisema katika kuimarisha mshikamano na kuhakikisha hali ya uvunjifu wa amani haijitokezi, Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Kagera, imeuagiza uongozi wa CCM wa Wilaya ya Bukoba Mjini, kufanya vikao vya kikatiba kujadili hali ya malumbano yaliyopo.

"CCM tunawaomba wananchi kuendelea kuwa wamoja, umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu na pasipo na amani hakuna maendeleo,” alisema.

Katika siku za karibuni, kumeibuka mgogoro unaomhusisha Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika manispaa ya Bukoba, umeanza kukumbana na vizingiti ambapo wafanyabiashara walioko ndani ya soko kuu, wamefungua kesi Mahakama Kuu Kanda kupinga kuondolewa ndani ya soko hilo.
 
Back
Top Bottom