CCM siku zote wanataka kumiliki pande zote mbili za mijadala mizito!

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Embu niwadokezee jambo moja ambalo ningependa mchukue muda wenu mlitafakari.

Kwa sisi wakongwe na wafuatiliaji wa mambo ya nchi hii, tumeshuhudia mambo mbalimbali yakitokea na kufanyika nchi hii.

Kuna masuala ya muungano, kuna masuala ya mfumo wa vyama vingi, kuna masuala ya mabadiliko ya kiuchumi kwenda soko huria.

Hayo sitayaongelea sana ila itoshe tu kuwaambia sababu moja kubwa iliyoifanya CCM na serikali zake isidhurike na mabadiliko yale ni kuhakikisha kuwa pande zote mbili za mijadala zinaongozwa na watu wao.

Kwa mfano, serikali ilipeleka watu waongoze vyama vya wafanyakazi kiasi kwamba mpaka leo vimekuwa butu na wafanyakazi hawana wasemaji. Hata pale wanapotoa matamko, yanakuwa hayana nguvu iliyo thabiti.

Ningetoa mifano mingine ila nadhani nitakuwa nimewapa pa kuanzia.

Kwenye suala la corona, hawa kina Gwajima wanaoleta misimamo yao na wanaachwa tu wabwatuke wanachotaka, ni jitihada kuhakikisha kuwa wanamiliki upande wa wapingaji wa chanjo na maamuzi mengine ya serikali. Hii inawahakikishia ushindi hata huko mbele mambo yakienda ndivyo sivyo.

Hilo ndiyo nataka mlizingatie na mlitafakari.
 
Ujanja ujanja una mwisho
 
Back
Top Bottom