Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Katika ufunguzi wa kampeni za CCM katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam,CCM haikuonyesha jipya. Kama yaliyosemwa na Mgombea wao Dr. Magufuli na Mgombea mwenza Mama Samia ndiyo yaliyo kwenye Ilani,basi Ilani yao haina jipya.
Karibu mambo yote ni yale yale ya miaka nenda rudi na yalikuwa kwenye Ilani zote tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Jangwani leo hakukuwa na jipya zaidi ya kauli zisizo na staha toka kwa waheshimiwa.
Mambo yote yaliyosemwa yameshasemwa na kubuma katika kutekelezwa. Kama kampeni za CCM zitafuata mwelekeo wa mashambulizi ya watu na kurudia mambo ya tangu kale,CCM haifai kuaminika tena hata kwa mwezi mmoja.
Rais Mstaafu Mkapa amesikika akimwita Sumaye mpumbavu na lofa. Timamu yeyote lazima ashangazwe na Mzee Mkapa kumuamini mpumbavu na lofa kwa miaka 10 kama Waziri Mkuu wake. CCM imejibomoa na kujianika zaidi kuliko kujijenga. Haifai kuaminiwa tena na ipumzishwe ili ijipange.