CCM si wa kuwaamini, wapumzishwe sasa | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM si wa kuwaamini, wapumzishwe sasa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Petro E. Mselewa, Aug 23, 2015.

 1. Petro E. Mselewa

  Petro E. Mselewa Verified User

  #1
  Aug 23, 2015
  Joined: Dec 27, 2012
  Messages: 7,664
  Likes Received: 10,705
  Trophy Points: 280
  Katika ufunguzi wa kampeni za CCM katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam,CCM haikuonyesha jipya. Kama yaliyosemwa na Mgombea wao Dr. Magufuli na Mgombea mwenza Mama Samia ndiyo yaliyo kwenye Ilani,basi Ilani yao haina jipya.

  Karibu mambo yote ni yale yale ya miaka nenda rudi na yalikuwa kwenye Ilani zote tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Jangwani leo hakukuwa na jipya zaidi ya kauli zisizo na staha toka kwa waheshimiwa.

  Mambo yote yaliyosemwa yameshasemwa na kubuma katika kutekelezwa. Kama kampeni za CCM zitafuata mwelekeo wa mashambulizi ya watu na kurudia mambo ya tangu kale,CCM haifai kuaminika tena hata kwa mwezi mmoja.

  Rais Mstaafu Mkapa amesikika akimwita Sumaye mpumbavu na lofa. Timamu yeyote lazima ashangazwe na Mzee Mkapa kumuamini mpumbavu na lofa kwa miaka 10 kama Waziri Mkuu wake. CCM imejibomoa na kujianika zaidi kuliko kujijenga. Haifai kuaminiwa tena na ipumzishwe ili ijipange.
   
 2. S

  Subira the princess Senior Member

  #21
  May 3, 2018
  Joined: Mar 3, 2018
  Messages: 167
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Sio kweli, ccm walipoteza dira kwa kufuta azimio LA ARUSHA na kutengeza azimio LA ZANZIBAR ambalo lilifuta maadili kwa viongozi na kuuza Tanzania yetu kwa majizi
   
 3. MLA PANYA SWANGA

  MLA PANYA SWANGA JF-Expert Member

  #22
  May 3, 2018
  Joined: Jul 31, 2015
  Messages: 2,996
  Likes Received: 3,004
  Trophy Points: 280
  Ndo umejua leo.
   
 4. magnifico

  magnifico JF-Expert Member

  #23
  May 3, 2018
  Joined: Jan 14, 2013
  Messages: 3,108
  Likes Received: 2,435
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio waliosaini mikataba ya hovyo?! Hopeless kabisa.
   
 5. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #24
  May 3, 2018
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 14,423
  Likes Received: 7,610
  Trophy Points: 280
  Tukimaliza kujadili hili tutaamia thread yenye title " ili uwe Chadema yakupasa kuwa Mnyonge" huko ni kulia lia kwa kila kitu...
   
 6. mosabiy

  mosabiy JF-Expert Member

  #25
  May 3, 2018
  Joined: Jul 3, 2017
  Messages: 241
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 60
  IN SHORT KUWAAMINI WANASIASA INAHITAJI UWE NA AKILI ZA KUSHIKIWA SI LUMUMBA SI UFIPA
   
 7. B

  Babeli JF-Expert Member

  #26
  May 3, 2018
  Joined: Jul 20, 2015
  Messages: 3,990
  Likes Received: 1,369
  Trophy Points: 280
  Haya mambo kabla ya kuandika kwanza ungetaka ushauri wa mchungaji Msigwa kabla ya kututapikia hapa....halafu pia ungewasiliana na watuhumiwa wa ufisadi waliokimbia ccm ma kukimbilia chademaa..hahahah...chama cha mafisudi...karne hii tutaona mengi
   
 8. B

  Babeli JF-Expert Member

  #27
  May 3, 2018
  Joined: Jul 20, 2015
  Messages: 3,990
  Likes Received: 1,369
  Trophy Points: 280
  Hahahah Zito Kabwe aliwaambia. Msiwaamini wanasiasa hasa hasa wa upinzani..ni bora uunge mkono chama tawala kinachopambana na mafisadi ambao wengi wao wamekimbilia chademaaa..na kusafishwa
   
 9. B

  Babeli JF-Expert Member

  #28
  May 3, 2018
  Joined: Jul 20, 2015
  Messages: 3,990
  Likes Received: 1,369
  Trophy Points: 280
  Hahahahahah sindano zimeingiaaaa...
   
 10. reginaldkaijage

  reginaldkaijage JF-Expert Member

  #29
  May 3, 2018
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 1,639
  Likes Received: 3,386
  Trophy Points: 280
  Mchuano huu mkali zaidi ya washa washa, Sijui nani ataibuka na kombe!
   
 11. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #30
  May 3, 2018
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 28,144
  Likes Received: 12,563
  Trophy Points: 280
  Hazungumzii Chadema anazungumzia CCM
   
 12. ZOPPA

  ZOPPA JF-Expert Member

  #31
  May 4, 2018
  Joined: Jan 20, 2017
  Messages: 2,342
  Likes Received: 2,342
  Trophy Points: 280
  Kwli kqbisa
   
 13. sinajinasasa

  sinajinasasa JF-Expert Member

  #32
  May 4, 2018
  Joined: Dec 10, 2013
  Messages: 923
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 180
  Sisomi hata dhima ya uzi zako kwa vile hii thread ungeileta mwaka 1992.
  Unaleta thread ambayo wenzio washasema hawatoki
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...