Elections 2015 CCM si wa kuwaamini, wapumzishwe sasa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,173
25,446
Katika ufunguzi wa kampeni za CCM katika Viwanja vya Jangwani Dar es Salaam,CCM haikuonyesha jipya. Kama yaliyosemwa na Mgombea wao Dr. Magufuli na Mgombea mwenza Mama Samia ndiyo yaliyo kwenye Ilani,basi Ilani yao haina jipya.

Karibu mambo yote ni yale yale ya miaka nenda rudi na yalikuwa kwenye Ilani zote tangu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Jangwani leo hakukuwa na jipya zaidi ya kauli zisizo na staha toka kwa waheshimiwa.

Mambo yote yaliyosemwa yameshasemwa na kubuma katika kutekelezwa. Kama kampeni za CCM zitafuata mwelekeo wa mashambulizi ya watu na kurudia mambo ya tangu kale,CCM haifai kuaminika tena hata kwa mwezi mmoja.

Rais Mstaafu Mkapa amesikika akimwita Sumaye mpumbavu na lofa. Timamu yeyote lazima ashangazwe na Mzee Mkapa kumuamini mpumbavu na lofa kwa miaka 10 kama Waziri Mkuu wake. CCM imejibomoa na kujianika zaidi kuliko kujijenga. Haifai kuaminiwa tena na ipumzishwe ili ijipange.
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Lowassa aliyewaibia watanzania akajitajirisha na familia yake ana yepi mapya ya kuwaambia watanzania? Acha ulofa na upumbavu.
 
Cdm siyo yakuiamini ilituambia lowassa ni fisadi naushahidi wanao leo lowasa msafi. Na lowassa anasema mwenye ushahidi aende mahakamani cdm mpo kimya hampaswi kuaminiwa tena cdm
 
Watayaacha kwenye vitabu tu ikifika 2020 wanatuletea kijitabu tena. Mimi nilitamani sasa hivi wangekuwa wanatuletea mafanikio yao kwenye hivyo vitabu si ahadi hewa tena.lol!
 
Wasalaam, ccm chama dola chama tawala tokea uhuru kimefika hatamu kimechoka kinaongoza kwa nguvu za vyombo vya dola na kutumia nguvu kubwa dhidi ya RAIA wa Tanzania.

Kwanini nasema haya,;
1.ccm ndicho chama kilichotuingiza watanzania kwenye mikataba ya makaburi hasa ktk umeme na gesi. Pale kuna mikataba ya miaka hadi99 huku serikali ikipata 3% ktk 100%. Hii ni mikataba ya hovyo hata babu zetu wakati wakitawaliwa na mkoloni hawajawahi ingia na kusaini.

2.ccm ambao ni mabigwa wa ulaghai, walishirikiana wao na wezi kuchota pesa hazina ambazo ni kodi za wavuja katika ufisadi wa kutisha wa Richmond, epa, tegeta escrow, arv feki, barabara kujengwa chini ya viwango na kuharibika ndani ya muda mfupi.

3.ccm wameongoza kwa kuvunja katba walioipotisha wenyewe, kufanya siasa za kibaguzi kwa kuzuia vyama vingine vya siasa kufanya siasa, kuibuka mauji ya viongozi wa kisiasa wa upinzani, utekaji na kupotezwa kwa kila anaowakosoa na kuwapinga.

4.kuingilia vyombo vya habari, uhuru wa kuongea kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba, kuzuia bunge live, mahakama kutokuwa huru, kuibuka kwa kundi LA wauaji na watesi dhidi ya RAIA ambao ccm wamewabatiza jina WATU WASIOJULIKANA ili hali tuna vyombo vya dola km tiss, jeshi imara, police, magereza na uhamiaji. Kweli km taifa tumeshindwa kuwajua watu wasiojulikana? Kwa kweli inasikitisha tumepoteza utaifa, kwani siku zote kubomoa ni rahisi kuliko kujenga. Nanukuu maneno ya marehemu HORACE KOLIMBA katibu wa ccm aliwahi kusema, nanukuu," CCM IMEPOTEZA DIRA. je alikurupuka au maneno yake yanaishi?
 
Mtoa mada

Maoni na ushaur wako havitakua na msaada kwa taifa letu.

endapo utaendelea kua upande wa wasaliti wanaotumika na wasiolitakia mema taifa letu.

Nakushauri:
Rudi kundini Tujenge Taifa letu
FB_IMG_1525104048981.jpg
 
Ukizisoma sheria na taratibu za chama cha mapinduzi unaweza kukuta hakuna chama kizuri kama ccm. Ila watu wake sijui wamelogwa na nani
 
Mtoa mada jitafakari kwani hujitambui bdo. Cjui una umri gani nahisi uko darasa la 5.
 
Maana yake ni hii. Je hawa wanaaminika?
Hawajawahi kuongoza dola mkuu, kwanza naona hawa sio ccm na mmoja wao huyu amekutana na watu wasiojulikana mpaka Leo anaugulia alinusurika na kifo, na chaajabu hawa waliomtia risasi policeccm hawajawakamata hata kivuli, pia binge halijamlipia matibabu. Wape nafasi Siku moja tuone wanaaminika au LA.
 
Yaani Ufipa watakuwa wamejaa wa p.. maana mtu anatoa mada kama katoka usingizini.
Hebu atwambie nini cha kutuaminisha kutoka upinzani hasa CDM kwanza kumbe
  1. Kiongozi wao mkuu halipagi kodi kabisa.
  2. wafadhili wamechanga weee ili ofisi ijengwe lakini mkuu wenu wenyewe mnajua, Ufipa aibu
  3. Viongozi wakuu wanausika na madawa ya kulevya
  4. Katiba imechezewa na hakuna democrasia ndani, tena ukimgusa mkuu au kutofautiana naye umefukuzwa.
  5. wanalolisema leo sio watakalolisema kesho
  6. chama kina mwenyekiti wa maisha kama Kamuzu Banda na Mobutu Seseko
  7. Akili imegota mnafundishwa kususa na maandamano tu.
  8. Kwa sababu za uchu wa madaraka mkawa tayari kuuza chama
sasa muone aibu ni bora kukaa na hiki kilicho chakaa kuliko mliochoka kwa taamaa binafsi, CCM oyeeeeee hadi mwaka 3020
mtachukua vumilieni kwa tabia zenu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom