CCM si safi

CCM si safi

Hayo ni mawazo yako tu.... Unaweza hata kuandika kitabu cha kurasa 10,000 kwamba CCM sio safi...CCM ni safi na itaendelea kuwa safi. Wale wachafu ndani ya CCM tunawatoa pamoja na mazagazaga yao.

Mkuu inawezekana unachosema ni kweli. CCM ni safi lakini ndani yake kunawachafu. Swali linalokuja ni vipi chama kiwe safi wakati kampeni zake zilifanywa kwa hila,fedha za wizi na mbinu chafu? Tunakitenganisha vipi chama chetu na watu wanaoheshimiwa ndani ya chama na waliokuwepo dania ya chama kwenye safu za juu za uongozi ambao ni mafisadi na wanawatetemea mafisadi? Tunaweza kumshawishi kweli mtu kuwa chama chetu ni safi?
 
Kibunango unaweza toa mfano halisi for the last five yrs wachafu wangapi na akina nani waliondolewa CCM???? Au ndio kusema wachafu hawajaokea into that period????????
 
Wanabodi,
Msitake kuharibu kiswahili hapa Huu USAFI/UCHAFU - mnaozungumzia ni Upi?...
waswahili wanasema hivi FEDHA ni sabuni ya roho!

Sasa chukueni maneno hayo kisha myabandike ktk hoja zenu mtaona kwamba mmetoka nje ya hoja ya wananchi.. Hakuna asiyependa kuwa msafi na hakika fedha ni sabuni ya roho..unazo utapendeza machoni mwa watu hata kama umevaa msuli na kandambili..
Wanachouliza wananchi ni jinsi gani sabuni hiyo (fedha) imepatikana..
 
Mkuu usafi au uchafu unatokana na wao wenyewe vigogo wa CCM akiongozwa na muungwana, Makamba, Chiligai etc. maraa kwa mara wamesikika wakisema CCM NI SAFI ila tu kuna watu wachache ambao si safi (wachafu).
 
Nyambala,
Naelewa vizuri kuhusiana na CCM...na mawazo yao ndio mtazamo wa mtu maskini mwenye kiburi.
Usafi ni matokeo tu ya jitihada zilizofanyika iwe haramu au halali.. ni sawa na Utajiri.. Mtu tajiri ni matokeo ya vitendo ambavyo hata jambazi linaweza kuwa tajiri sawa na yule ambaye ni mnyenyekevu..
Ni ujuha mkubwa kusema CCM ni safi kwa sababu sio chama kinachojenga kielelezo cha usafi wa tabia isipokuwa ni WATU wake...Na unapokubali kuwepo kwa baadhi ya watu wachafu wa Tabia ndani ya nyumba yako kisha ukawajengea hoja ni kutokukubali wajibu...lack of responsibility!
Hata siku moja huwezi kumwona mtu mchafu wa tabia ndani mwako ukaendelea kula naye sahani moja..
 
That is all true mkuu Mkandara. Ila kinachonistaajabisha ni kwamba kuna watu wengi tu tena hata the learned ones wanayaamini maneno hayo ya watawala wetu kwa dhati!!!!
 
Suala la uchafu si CCM ni hulka ya mtu binafsi na ifahamike kuwa cc inaundwa na watu na tabia ya mtu binafsi si ya CCM.

nAHESHIMU SANA MAWAZO YAKO MKUU ILA NAPENDA KUWATOFAUTI NA WEWE KIHOJA NA KIFIKRA KAMA IFUATAVYO,

CCM ni safi naitaendelea kuwa safi daima kwa kuwa inania ya dhati ya kuwatumika wananchi wa Tanzania, na wanachi wengi wanatambua hilo ndiyo kilipata ushindi wa kishindo 2005

Hayati baba wa Taifa alisema ,Chama cha siasa ni kama kokoro linavua samakia kama sangara, chura,dagaa na vinginevyo hivyo si vyema kusema CCM si safi kwani utakuwa umeangalia katika individual aspects.

Kama CCM IMESIMAMA KWENYE LUNDO LA TAKATAKA KINACHOTAKIWA NI KUTOKA NA KUSIMAMA MAHALI PASIPO NA LUNDO LA TAKATAKA NA MKONGOJO WAKE HUKU IKINUKIA MANUKATO.

NA KWATAAFIRA IMESHAANZA KUONDOKA ENEO LENYE LUNDO LA TAKA LINALONUKA.

AM

AM

Tuache unafiki wa wazi!!!! Kelele zote hizo za ufisadi wa wazi uliofanywa na viongozi waandamizi wa CCM bado tuendelee kusema ni safi?

Achana na utetezi wa aibu kwamba waliofanya hivyo ni mtu mmoja mmoja na si Chama. Chama si majengo au eneo la utawala (Nchi) bali ni wanachama wakiongozwa na VIONGOZI WAO.

Wanachama walishangamua ufisadi wa viongozi wao, tatizo ni kamba za ufisadi zilizowafunga wana CCM mithiri ya kuni zilizovingirwa na kamba poli wasiweze kufurukuta na kuwatoa warafi hawa wanaoendeleza unyonyaji kwa wapiga kura wao.

Tuwe wakweli vinginevyo vita hii itakuwa ngumu hata kwa wanasisemu wenyewe. Hivi sisi wenyewe uchafu hatuuoni? CCM si safi.
 
Unaweza vipi kutenganisha chama na watu waliomo ndani ya chama hicho; si watu ndio wanaounda chama?
 
Mkuu inawezekana unachosema ni kweli. CCM ni safi lakini ndani yake kunawachafu. Swali linalokuja ni vipi chama kiwe safi wakati kampeni zake zilifanywa kwa hila,fedha za wizi na mbinu chafu? Tunakitenganisha vipi chama chetu na watu wanaoheshimiwa ndani ya chama na waliokuwepo dania ya chama kwenye safu za juu za uongozi ambao ni mafisadi na wanawatetemea mafisadi? Tunaweza kumshawishi kweli mtu kuwa chama chetu ni safi?

Hivi CCM kuna mtu msafi kweli!!? Ni nani huyo..Makamba!! au Rostam Azizi!!!? 😕
 
Wale wote wachafu wamekuwa wakitimiliwa ndani ya chama tangia kuanzishwa kwake.

Hebu taja wachache tu kati ya hao waliotimuliwa na nyadhifa zao katika chama.

CCM sio chama cha mtu mmoja ama genge la watu fulani najua unalijua hilo, na imekuwa ikiwaondoa wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakienda kinyume na katiba ya chama, kupitia vikao vyake vya kawaida na dharura katika ngazi zinazohusika.
Je unayo habari kwamba usemi, "CCM ina wenyewe" ilianzishwa lini, na nani na kwa malengo gani ? CCM ina "untouchables" ambao serikali yenyewe ya CCM imesema wazi kuwa wakiguswa nchi itayumba. Je, wewe Kibunango umo miongoni mwa hao - sidhani kwa sababu you are so misinformed.

Na wengine kwa kushindwa kufuata katiba ya chama hicho wamekuwa wakijiengua wenyewe kabla ya kutimuliwa.

Watiifu wa CCM kamwe hawawezi kujiengua wala kutimuliwa - huo ubavu utapatikana wapi. Adui mkubwa wa CCM kwa wakati huu ni yule anayejaribu kukisafisha na huyu wana CCM hawasiti kumwona dui kwa kutaka kutia mkate wao mchanga - wakale wapi ?

Kauli ya usafi ama uchafu ni kauli ambayo tupo nayo katika miaka hii, CCM kama chama inaenda sambamba na kauli hiyo kwa kuendelea kuwaondoa wale wote wanabainika kuwa ni wachafu. Taratibu za kuwaondoa wachafu hao ni zilezile ambazo zimekuwa zikitumika tokea kuanzishwa kwa chama hicho.

Ama wewe hujui kinachotokea ndani ya CCM au unaamua kwa sababu zako kusema uwongo. Tabia na taratibu iliyojengeka ndani ya CCM siku zote ni ya kulindana na hili hata mtoto mdogo analifahamu. Kwa hivi sasa KAGODA ni mfano hai wa kulindana ndani ya CCM kunavyozidi kukomazwa - je, ni kweli hata hili hulioni ?

Uzuri wa miaka hii ni kuwa wale wachafu ambao hutimuliwa CCM hupata sehemu za kwenda na mazagazaga yao ya uchafu.
Wataje hao. Ninavyojua wachafu wanaoondoka CCM hukosa pa kutua na mwishowe hulazimika kurudi huko huko na kupokelewa kwa vifijo na nderemo. Huko nje baada ya muda hugundua kuwa hakuna mabwawa ya Richmond, Kiwira, Kagoda, n.k - sasa wataogelea wapi ?

Na huko hukutana na wachafu wenzao na kuendeleza tabia zao za uchafu uchafu, huku wakiota siku moja wataongoza nchi na mauchafu yao.

Huko nje hukutana na wazalendo wenye nia ya kweli ya kukomboa nchi na inabidi ama wajioshe wawe wasafi au warudi CCM. Mifano iko mingi tu lakini ukweli unabaki pale pale kuwa CCM wanaongoza nchi kwa kuwa wako madarakani kwa uchafu wao nambari wani - rushwa.

Nyumba safi inaweza kukaliwa na wachafu vilevile, hata hivyo kutokana na sifa ya uchafu kuwa unuka ni rahisi kwa wachafu kujulikana katika nyumba safi. Na pua za wasafi wengi wa CCM siku zote zimekuwa zikinusa wale wote ambao awali walikuwa wasafi, lakini wakaanza kuwa wachafu. Uzuri utimuliwa mapema kabla ya kueneza tabia zao mbaya za uchafu.

Kweli kabisa ni rahisi kwa wachafu kujulikana kwenye nyumba safi kuliko msafi kujulikana ndani ya nyumba chafu. Pua za wasafi ndani ya CCM kama wapo zimeshindwa kunusa wachafu kwa sababu wote tayari wanaogelea kwenye uchafu na kupakana uchafu. Sasa hapa wa kunyosha kidole atapatikana wapi !!

Kimsingi Wachafu bado kwisha ndani ya CCM, lakini hii haina maana kama CCM ni chafu.

Ahaa, sasa unaanza kupata ka mwanga ila uchafu wenyewe umeshaligharimu taifa matrilioni ya shilingi na CCM haina tena nia wala uwezo wa kujisafisha. Kati ya uchafu na usafi wamechagua uchafu na kansa sasa imeenea mwili mzima na hakuna tena tiba.

Baba wa nyumba ya CCM ameshasema bayana kuwa mchafu yoyote atakayebainika ndani ya nyumba ataondolewa na kupelekwa kunako husika na usafishaji wa wachafu.

Baba mwenyewe alikubali kutawazwa kwenye nyumba yenye uchafu na hivyo kuogelea humo humo - sasa hiyo jeuri ataitoa wapi ? Sana sana atabaki anawashangaa wanaopigia kelele uchafu wa nyumba anamoishi yeye.

Kauli za Baba huyu zimeshaanza kuonekana licha ya maneno ya kejeli toka katika katika nyumba za Wachafu wengi ambao kutwa wamekuwa wakitamani Nyumba safi ya CCM iwe chafu kama zao.

Kwa nini kelele zitoke nje ya hilo jumba tu na zisitoke humo ndani kama kweli nyumba bado ina wasafi. Unasema nyumba ya CCM ni safi halafu unakubali kuwa bado kuna wachafu humo ndani yake - kweli hii inaingia akilini.

Kibunango which makes more sense - wachafu kutoka kwenye usafi au wasafi kutoka kwenye uchafu ?
 
Hayati baba wa Taifa alisema ,Chama cha siasa ni kama kokoro linavua samakia kama sangara, chura,dagaa na vinginevyo hivyo si vyema kusema CCM si safi kwani utakuwa umeangalia katika individual aspects.

Ila ukigundua umevua chura au samaki usiyemtaka si unamtupia majini aende zake na kubaki na wale unaowataka.

Sasa kwa nini CCM inawaona vyura na mazagazaga kibao ambayo yanaharibu dhana nzima ya samaki wazuri haiwarushii majini?, inaendelea kuwahesabu nao ni samaki? je unataka sokoni wateja (wananchi wapiga kura) walazimishwe kuamini na kununua vyura wakiambiwa ni nao ni samaki?.

Vyura wanajulikana ila ndiyo wanatoa harufu katika CCM zaidi ya Samaki, Je huoni hapo kuwa ni sawa na kusema CCM ni vyura (Inanuka vyura) kwa sababu samaki ni wachache sana kuliko vyura? na kuwatupa vyura ni kupunguza cargo iliyovuliwa?.

Basi ili mtuaminishe kuwa CCM ni samaki basi anzeni kuwatosha majini vyura kabla hamjafika sokoni. Hapo ndipo tutaona kuwa kweli CCM ni safi vinginevyo ni CCM yenyewe ndiyo inaonekana ina upofu wa kuona kipi ni kizuri na kipi ni kibaya na kwa mantiki hiyo hata nchi mlipoifikisha ni kwa ajili ya upofu wenu wa kutulazimisha Chura tuwaite samaki.

"CCM ni CHAFU" maana hata kusema si safi wanaweza wasielewe kinyume cha si SAFI ni nini?
 
- Mkuu Kibunango, ubarikiwe kwa msimamo thabiti sana tuko pamoja ila tatizo ni computer yangu imerushiwa vitu vikali sana siwezi kuingia lakini itatengemaa karibuni, CCM ni chama safi sana na ndio kimetufikisha wa-Tanzania wote hapa tulipo, tunajua uzuri na ubaya wa siasa kutokana na malezi bora ya CCM,

baada ya Mwalimu kuondoka CCM ikavamiwa na viongozi wachache wabovu, hilo linaeleweka na ndio maan sasa hivi Mbeya hakuna kiongozi mbovu kwenye kampeni, tulitegemea wenzetu watakwua huko kusaidia wengine lakini wapi wapo hapa kupiga filimbi zisizoweza kulisaidia taifa, very sad indeed!

Kubunango tupo wote mkuu!
 
Nyambala, Hata siku moja huwezi kumwona mtu mchafu wa tabia ndani mwako ukaendelea kula naye sahani moja..

Halafu bila aibu ukapita huku na kule huku ukijipiga kifua eti wewe ni safi!!! Wanataka kutufanya wote majuha kumbe wao ndiyo majuha kutaka kujipa sifa wasizostahili!!! Hebu tuwekewe majina hapa kama ndani ya CCM kuna msafi yeyote ni nani huyo!!!!? Mkapa, Kikwete, Makamba, Msekwa, na wengineo chungu nzima wote tunajua si wasafi. Sasa wasafi ndani ya CCM ni akina nani?
 
- Inaonekana huko upande wa pili kuna dhana ya viongozi kua ndio chama, kwa mtizamo huo ni kweli Chadema nzima kama chama kinakua kimeoza kwa sababu Shitambala, hajui sheria za uchaguzi, na CCM pamoja na sisi wanachama zaidi ya millioni tano tunakua wachafu kwa sababu ya ufisasdi wa viongozi wetu wachache wasiozidi 15,

- Nilifikiri JF ni demokrasia makini kwa hiyo tutakuwa sensitive na tabia hizi za kututukana wanachama wote wa CCM kwa sababu ya ufisadi wa wachache wakati sio sisi wananchama wote ni mafisadi, kitu ambacho hata wananchi wanakielewa sana ndio maana hawana tatizo kwenye kutenganisha haya unapokuja uchaguzi,

Sasa ninaomba tu kuwakumbusha wahusika kuwa kwenye hili hamtutendei haki wanachama wa CCM tulio safi, ambao ni zaidi ya Millioni Tano, as opposed na viongozi mafisadi wasiozidi 15 tu. CCM tutaendelea kama tulivyoanza na in the process tutawashusha pole pole viongozi wabovu na pia tutawarudia wale waliopita pia kisheria, hakuna atakayepona.

Thanxs!
 
FMES,
Mkuu tunakuelewa sana isipokuwa tu mnachokosea ni pale tunaposema hivi..nyumba yako chafu sii safi, na majibu yako yanakuja kuwa hapana nyumba yangu sii chafu ni swafiiii isipokuwa mke wangu ndiye mchafu...mmmhhhhn!

Hivyo, tatizo ni kwamba wewe unaangalia vitu kwa kutafuta mbaya wakati unaishi ktk nyumba hiyo hiyo chafu ilofagiliwa sebuleni na uchafu wote umefichwa uvunguni..Au niseme hivi mkeo/Mmeo ni mchafu kwa ufuska anaofanya lakini upo ktk ndoa kwa kisingizio ufuska ni wake sio wako..

Mkuu achana na habari za Chadema, tatizo lao linaeleweka ni sawa na mwanamke mzuri aliyefunga ndoa na Mlalahoi..
Binafsi kwa yote yaliyotokea ndani ya Chadema nimejifunza moja kwamba Umaskini ni adui mkubwa wa haki.. Yaliyotendeka na yanazodi kutendeka baina ya Chadema na CUF ni ruzuku tu za serikali zinazowasumbua..Hivyo uchafu wao ni kupigania mabaki ya chakulka kinachotupwa na CCM...Na hakika nimechoshwa na siasa za Bongo inapofikia Upinzani.
Sasa tukirudi ktk usafi mkuu wangu, CCM -CHAFU imeingiliwa tena sii kidogo na principal wanayotumia ni hiyo FEDHA sabuni ya roho!..
 
FMES,
Mkuu tunakuelewa sana isipokuwa tu mnachokosea ni pale tunaposema hivi..nyumba yako chafu sii safi, na majibu yako yanakuja kuwa hapana nyumba yangu sii chafu isipokuwa mke wangu ndiye mchafu...

Sasa tukirudi ktk usafi mkuu wangu, CCM -CHAFU imeingiliwa tena sii kidogo na principal wanayotumia ni hiyo FEDHA sabuni ya roho!..

- Mkulu Bob, ninakusikia ila baadhi ya mifano ya maisha sio rahisi kuyaa-apply kwenye siasa kwa sababu maana zinakuwa ni mbali sana from each other, na ukijaribu kulazimisha kwa nguvu ukaribu then unaishia kupata jibu ambalo sio makini kua wananchi wote wa Tanzania sio safi, kwa sababu how CCM imeweza kutawala kwa miaka 47 huku ikiwa chafu na wananchi wake wakiwa wasafi? It does not make a sense at all!
 
- Inaonekana huko upande wa pili kuna dhana ya viongozi kua ndio chama, kwa mtizamo huo ni kweli Chadema nzima kama chama kinakua kimeoza kwa sababu Shitambala, hajui sheria za uchaguzi, na CCM pamoja na sisi wanachama zaidi ya millioni tano tunakua wachafu kwa sababu ya ufisasdi wa viongozi wetu wachache wasiozidi 15,

- Nilifikiri JF ni demokrasia makini kwa hiyo tutakuwa sensitive na tabia hizi za kututukana wanachama wote wa CCM kwa sababu ya ufisadi wa wachache wakati sio sisi wananchama wote ni mafisadi, kitu ambacho hata wananchi wanakielewa sana ndio maana hawana tatizo kwenye kutenganisha haya unapokuja uchaguzi,

Sasa ninaomba tu kuwakumbusha wahusika kuwa kwenye hili hamtutendei haki wanachama wa CCM tulio safi, ambao ni zaidi ya Millioni Tano, as opposed na viongozi mafisadi wasiozidi 15 tu. CCM tutaendelea kama tulivyoanza na in the process tutawashusha pole pole viongozi wabovu na pia tutawarudia wale waliopita pia kisheria, hakuna atakayepona.

Thanxs!

Tawire mkuu umenena! Kama CCM inanuka sababu ya viongozi wachache inawakuwaje hao hao wakitoka na kwenda Chadema wanakuwa wasafi papo hapo...
 
CCM ni chama kichafu, chenye watu wachache wasafi, siyo chama chenye watu wengi wasafi na chenyewe siyo kichafu kabisa; Ni watu wanaochafua chama, na chama hakiwachafui watu.

Mtu akileta matope ndani ya nyumba hatusemi nyumba ndiyo imemchafua na ili kuweza kusafisha nyumba ni lazima na yeye mwenyewe asafishwe, vinginevyo ukiondoa viatu vyenye matope ndani ya nyumba, umeifanya nyumba kuwa safi?

Siyo tu kwamba CCM ni chafu, bali pia serikali inayotokana nayo ni chafu vile vile, kama vile mtoto wa nyoka ni nyoka vivyo hivyo serikali inayotokana na chama kichafu, huwa na yenyewe chafu!

Hii hata hivyo haiondoi ukweli kuwa kuna watu wasafi ndani ya CCM, ambao wameuona uchafu wakakaa nao mbali, ingawa wanakaa nao nyumba moja. NI sawa na mtu ambaye anatunza chumba chake kwa usafi, na sebuleni kwa usafi lakini ukienda jikoni na msalani itabidi ukimbie. Hata hivyo usafi huo wa sehemu sehemu haufanyi kuwa nyumba nzima kuwa safi. Uchafu huambukiza, usafi hauambukizi!

Shuka nyeupe ambayo imekojolewa upande mmoja na mtoto, hatusemi kuwa ni "shuka safi, isipokuwa kona ile". Tunasema "shuka imechafuka" na hivyo unapoenda kuifua, inabidi ufue shuka nzima!
 
Yo Yo,
Muflisi kwa sababu hujui nilichoandika, ktk akili yako huwezi kuelewa na nina hakika huelewi wala hutakuja elewa!..
 
Back
Top Bottom