CCM si safi

FMES,
Bila shaka Tanzania yote ni Chafu kwani tupo ktk orodha ya juu ya nchi zinazo ongoza kwa Corruption duniani. kila baya au ovu la kiuchumi duniani tupo ktk the best 20s..nini zaidi tunataka tuambiwe ili tukubaliane na ukweli.
Ndio uchafu wenyewe huo mkuu huanzia kwa wazazi..Ukiniuliza mimi kama sisi Watanzania ni wachafu nitakubali hata kama sababu ni mzazi na ndio maana tupo hapa JF kutafuta mbinu za kujisafisha. Wasomi kama nyie ndio mnaotupa darasa kwani sii aibu kumwambia mzazi wako kuacha Ufuska..Ni haramu kula chakula kilichotokana na fedha za ufuska au wizi hata kama wewe ni clean!
Tuwe responsible na accountable..
 
- Strong argument mkuu, tupo pamoja hapa.
 
- Nilifikiri JF ni demokrasia makini kwa hiyo tutakuwa sensitive na tabia hizi za kututukana wanachama wote wa CCM kwa sababu ya ufisadi wa wachache wakati sio sisi wananchama wote ni mafisadi, kitu ambacho hata wananchi wanakielewa sana ndio maana hawana tatizo kwenye kutenganisha haya unapokuja uchaguzi,

Sasa ninaomba tu kuwakumbusha wahusika kuwa kwenye hili hamtutendei haki wanachama wa CCM tulio safi, ambao ni zaidi ya Millioni Tano, as opposed na viongozi mafisadi wasiozidi 15 tu. CCM tutaendelea kama tulivyoanza na in the process tutawashusha pole pole viongozi wabovu na pia tutawarudia wale waliopita pia kisheria, hakuna atakayepona.

Thanxs!

Mkuu taratibu kidogo, naomba kutofautiana na wewe kidogo. Acha tutukanwe na tutafute njia ya kutowapa watu nafasi ya kututukana Tunanuka, inabidi tuondoe harufu yetu hafu kwanza hapo ndio tuanze kuwazodoa wanaoema tunanuka. Nadhni tumepokea vizuri matsi haya na kuyafanyia kazi taratibu, kama asingekuwepo wa kututukana labda hadi leo tungekaa kimya tu na kuwaacha mafisadi kama 1500 kati ya wana CCM milioni 15 (walio ndani ya chama na wasio ndani ya chama) waendelee na ushetani wao. Hao mafisadi ni sehemu ya mwili wetu hatuwezi kuwakataa. Kwa kuw ni wetu taratibu tunawanyoa.
 
FMES,
Bila shaka Tanzania yote ni Chafu kwani tupo ktk orodha ya juu ya nchi zinazo ongoza kwa Corruption duniani. kila baya au ovu la kiuchumi duniani tupo ktk the best 20s..nini zaidi tunataka tuambiwe ili tukubaliane na ukweli.
Ndio uchafu wenyewe huo mkuu huanzia kwa wazazi..Ukiniuliza mimi kama sisi Watanzania ni wachafu nitakubali hata kama sababu ni mzazi na ndio maana tupo hapa JF kutafuta mbinu za kujisafisha. Wasomi kama nyie ndio mnaotupa darasa kwani sii aibu kumwambia mzazi wako kuacha Ufuska..Ni haramu kula chakula kilichotokana na fedha za ufuska au wizi hata kama wewe ni clean!
Tuwe responsible na accountable..

Naam Mkuu na hali haikuwa mbaya kama ilivyo sasa enzi za Mwalimu. Sasa hivi watu wanashindana nani atakuwa tajiri sana kuliko mwingine, nani atajenga hekalu kali zaidi kama yale ya Hollywood kuliko mwingine, nani ataendesha magari ya bei mbaya kuliko mwingine nani na ili kukamilisha adhma yao basi wanakupua mabilioni kila kukicha bila woga wala aibu na kuwaacha Watanzania walio wengi wakiishi maisha ya ufukara uliokithiri.
 
CCM ni chama kichafu, chenye watu wachache wasafi, siyo chama chenye watu wengi wasafi na chenyewe siyo kichafu kabisa; Ni watu wanaochafua chama, na chama hakiwachafui watu.

Mtu akileta matope ndani ya nyumba hatusemi nyumba ndiyo imemchafua na ili kuweza kusafisha nyumba ni lazima na yeye mwenyewe asafishwe, vinginevyo ukiondoa viatu vyenye matope ndani ya nyumba, umeifanya nyumba kuwa safi?

Siyo tu kwamba CCM ni chafu, bali pia serikali inayotokana nayo ni chafu vile vile, kama vile mtoto wa nyoka ni nyoka vivyo hivyo serikali inayotokana na chama kichafu, huwa na yenyewe chafu!

Hii hata hivyo haiondoi ukweli kuwa kuna watu wasafi ndani ya CCM, ambao wameuona uchafu wakakaa nao mbali, ingawa wanakaa nao nyumba moja. NI sawa na mtu ambaye anatunza chumba chake kwa usafi, na sebuleni kwa usafi lakini ukienda jikoni na msalani itabidi ukimbie. Hata hivyo usafi huo wa sehemu sehemu haufanyi kuwa nyumba nzima kuwa safi. Uchafu huambukiza, usafi hauambukizi!

Shuka nyeupe ambayo imekojolewa upande mmoja na mtoto, hatusemi kuwa ni "shuka safi, isipokuwa kona ile". Tunasema "shuka imechafuka" na hivyo unapoenda kuifua, inabidi ufue shuka nzima!
Mzee Mwanakijiji umetoa taarifa ambayo sikubalianai nayo kabisa maana huwezi ukalinganisha chama na nyumba mimi nasema CCM ni kisafi mimi nalinganisha CCM na baba mwenye familia unapokuwa na watoto hutarajii watoto hao wawe wezi na inapotokea mmoja akiwa jambazi mzazi husikitika na kufanya kila awezalo ili mtoto huyo asiendelee na tabia hiyo ya ujambazi na ndivyo CCM inavyofanya na kwamba mtoto akiwa jambazi huwezi kusema kuwa na baba ni jambazi
 
Tutake tusitake, CCM inaongozwa na baadhi ya watu wachafu na hakuna sababu ya kuitetea kuwa ni safi. Kama kiongozi/viongozi wakiwa wanatetea uchafu, hakuna mtu ndani ya chama anaeweza kuwafanya wabadilike hadi siku watakapoamua kubadilika wenyewe, ama kuondoka katika uongozi. Kuna sababu nyingi zinazopelekea watu wengi humu kusema CCM ni chafu. Na zote ni sababu za msingi.

Ukichukulia mfano wa nyumba (Chama): Kama ukiingia ndani ya nyumba unakutana na sebule chafu (Kiongozi) na sehemu hiyo ya nyumba ndio inayotumika kukaribishia wageni, ni dhahiri kuwa sehemu nyingine za nyumba hiyo zitakuwa ni chafu zaidi (Ngazi mbalimbali za uongozi). Hii inasababishwa na ukweli kwamba, si rahisi sana kwa kiongozi mdogo kuwa msafi kuliko mkubwa wake, hasa akiona mkubwa wake anafaidika na uchafu anaofanya na yeye akiendelea kuwa na hali duni.

Kinachotakiwa ni CCM kuhakikisha kinaweka miiko ya uongozi na kuisimamia kwa nia thabiti na kwa nguvu zote.

Inavyoonekana sasa, kila mtu anaweza kuwa kiongozi wa chama bila kujali uwezo, nia na heshima ya mtu huyo katika jamii. Kila mwenye kuhisi kuwa anaweza kuingia katika matatizo na vyombo vya usalama ama mamlaka ya kodi anakimbilia kwenye chama na kukaa karibu na viongozi (ili wamlinde). Hii inafanana na mtoto mtundu/mkorofi anaekwenda kuchokoza wenzake halafu anakimbilia kwa Baba yake ili azuie asipigwe. Mabadiliko ni lazima wakati huu, maana viongozi wakichelewa kuyafanya sasa, chama kitakuwa na hali mbaya zaidi, kwa kuwa kitakuwa na watu wengi wasiofaa na kukifanya kisiwe na nguvu yoyote katika jamii.
 
Tutake tusitake, CCM inaongozwa na baadhi ya watu wachafu na hakuna sababu ya kuitetea kuwa ni safi. Kama kiongozi/viongozi wakiwa wanatetea uchafu, hakuna mtu ndani ya chama anaeweza kuwafanya wabadilike hadi siku watakapoamua kubadilika wenyewe, ama kuondoka katika uongozi. Kuna sababu nyingi zinazopelekea watu wengi humu kusema CCM ni chafu. Na zote ni sababu za msingi.

.
Kama CCM ni chafu ni sawa na kusema kuwa Watanzania wote ni wachafu. Ikumbukwe kuwa Vyama vya siasa zaidi ya CCM vimerudi miaka ya tisini, na muda mrefu baada ya uhuru watanzania wamekuwa wakiishi katika mfumo wa chama kimoja. Mfumo wa vyama vingi una miaka kama kumi na sita hivi, hivyo bado u kijana na unaongozwa na wale ambao walikuwa CCM, na sidhani kama wanaweza kujiita wao ni safi.

Sifa za Watanzania wa leo zimejaa maneno yenye kila aina ya uchafu, tofauti ni linatoka katika kinywa cha nani. Hakuna ubishi kuwa Watanzania wengi wanapenda njia za mkato na kutofuata taratibu. Huu ni uchafu, na hivi majuzi CHADEMA wameonyesha wao ni wachafu kiasi gani kwa kushindwa kufuata taratibu badala yake kukimbilia njia ya mkato(uchaguzi mdogo wa ubunge Mbeya Vijijini). Uchafu wa aina hii ndio uzaa rushwa.

Watanzania wa leo wengi ni matapeli na wasio penda kufanya kazi, humu humu JF kuna ombi la kumchangia fedha za dhamana mtanzania mmoja anayeshikiliwa na vyombo vya dola kutokana na utapeli. Huu ni uchafu vilevile.

Wale ambao ni wazandiki, wapika majungu na wasanii wa siasa, wao kwa kutaka kujificha na aina yao ya uchafu wanapenda kutumia neno fisadi dhidi ya CCM, huku wakisahau kuwa ufisadi ni aina tu ya uchafu uliowajaa watanzania. Na katika mkutano wa hivi karibuni wa NCCR Mageuzi, mwenyekiti wao alikubali kuwa watanzania ni wachafu na kuhoji ni nani mwenye ubavu wa kumnyoshea kidole mwenzie kama ni fisadi ilhali nae yupo kundini?

Sio siri ule wakati wa Watanzania kutembea vifua mbele kutokana na uadilifu wa hali ya juu mpaka kuwa kioo kwa nchi jirani kama sio ulimwenguni haupo tena. Leo hii watanzania ni wapenda starehe na wavivu na mbaya zaidi ni mafisadi. Huu uchafu ni wa watanzania wote na ni vema kwanza watanzania wote wakajisafisha badala ya kukimbilia kusema kuwa CCM ni chafu.
 
Jamaani mwezetu katoa hoja tena hoja zito inayogusa masirahi ya Taifa, haina budi kuchangia kwa umakini sana na kuondoa itikadi zetu za vyama.

Haina ubishi CCM ni chafu sana tena sana, hakuna kiongozi hata mmoja ndani ya CCM ambaye ni msafi, nitajie kama unamfahamu? si tawi, shina, mkoa au Taifa wote ni wezi wakubwa, kila jambo wanalofanya hata mtoto mdogo atauliza pesa hizo wametoa wapi? mbona kufuru, angalia mapokezi ya mama Simba na comment mwenyewe.

Chama hiki kinakoelekea hapafaa hata kidogo, inachofanya serikali ya Kikwete ni kutoa kafala baadhi ya watu wasiokuwa na umuhimu wowote katika chama, wanatumia triki ya watanzania kuwa ni wepesi wa kusahau wakipewe pilau na kaka, hii yote ni kampani kwa ajili ya 2010 hasa kwa wananchi wa vijijini amako hakuna maendeleo yeyote.

Angalia maisha ya mtanzania wa kawaida yanapoelekea sasa, gharama za maisha zimepanda kupita kiasi, pesa yetu inashuka samani kila kukicha, angalia wanafunzi wa vyuo vikuu watoto wa wakulima wataweza kusoma angalau kama tulivyosoma sisi na si kama walivyosoma kina Kikwete na wengineo.

Jamaani imefika wakati watanzania tukabadilika na kuwa watu tunaojali masihara ya taifa letu, hatuna budi kuwaambia tumechoka.
 
Kama CCM ni chafu ni sawa na kusema kuwa Watanzania wote ni wachafu. Ikumbukwe kuwa Vyama vya siasa zaidi ya CCM vimerudi miaka ya tisini, na muda mrefu baada ya uhuru watanzania wamekuwa wakiishi katika mfumo wa chama kimoja. Mfumo wa vyama vingi una miaka kama kumi na sita hivi, hivyo bado u kijana na unaongozwa na wale ambao walikuwa CCM, na sidhani kama wanaweza kujiita wao ni safi.

Sifa za Watanzania wa leo zimejaa maneno yenye kila aina ya uchafu, tofauti ni linatoka katika kinywa cha nani. Hakuna ubishi kuwa Watanzania wengi wanapenda njia za mkato na kutofuata taratibu. Huu ni uchafu, na hivi majuzi CHADEMA wameonyesha wao ni wachafu kiasi gani kwa kushindwa kufuata taratibu badala yake kukimbilia njia ya mkato(uchaguzi mdogo wa ubunge Mbeya Vijijini). Uchafu wa aina hii ndio uzaa rushwa.

Watanzania wa leo wengi ni matapeli na wasio penda kufanya kazi, humu humu JF kuna ombi la kumchangia fedha za dhamana mtanzania mmoja anayeshikiliwa na vyombo vya dola kutokana na utapeli. Huu ni uchafu vilevile.

Wale ambao ni wazandiki, wapika majungu na wasanii wa siasa, wao kwa kutaka kujificha na aina yao ya uchafu wanapenda kutumia neno fisadi dhidi ya CCM, huku wakisahau kuwa ufisadi ni aina tu ya uchafu uliowajaa watanzania. Na katika mkutano wa hivi karibuni wa NCCR Mageuzi, mwenyekiti wao alikubali kuwa watanzania ni wachafu na kuhoji ni nani mwenye ubavu wa kumnyoshea kidole mwenzie kama ni fisadi ilhali nae yupo kundini?

Sio siri ule wakati wa Watanzania kutembea vifua mbele kutokana na uadilifu wa hali ya juu mpaka kuwa kioo kwa nchi jirani kama sio ulimwenguni haupo tena. Leo hii watanzania ni wapenda starehe na wavivu na mbaya zaidi ni mafisadi. Huu uchafu ni wa watanzania wote na ni vema kwanza watanzania wote wakajisafisha badala ya kukimbilia kusema kuwa CCM ni chafu.

CCM kuwa chafu si sawa na kusema waTanzania wote ni wachafu, hata kidogo. WaTanzania si CCM ila CCM ni waTanzania. CCM ina wanachama wasiozidi milioni 5 nchi nzima, walio hai na wasio hai. Hii ni asilimia ndogo sana ya waTanzania wote.

Uchafu wa kundi moja la watu, hauwezi kuwa uchafu wa nchi nzima. Ni sawa na kusema, uchafu katika mji mmoja wa nchi hii ni uchafu wa Taifa zima. Sio kweli hata kidogo. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha chama kuwa kichafu. Moja ya sababu hizo (ambazo ni kubwa) ni jinsi ya kupata viongozi wake (uchaguzi). Kama chama kitashindwa kudhibiti na kuweka ustaarabu wa upatikanaji wa viongozi kwa haki na usawa, ni dhahiri kuwa hakiwezi kuwa na watu safi kukiongoza. Maana, ili uwe kiongozi, itabidi uwe fisadi wa namna moja ama nyingine (uchafu mkubwa zaidi). Pili, uchafu wa chama unaweza kutokana na jinsi wanavyothamini na kuzingatia sheria za nchi, kujali mawazo mbadala na pia kujali ustawi wa jamii nzima (hii ya ustawi haijali kama chama kinaongoza dola ama lah).
 
FMES,
Bila shaka Tanzania yote ni Chafu kwani tupo ktk orodha ya juu ya nchi zinazo ongoza kwa Corruption duniani. kila baya au ovu la kiuchumi duniani tupo ktk the best 20s..nini zaidi tunataka tuambiwe ili tukubaliane na ukweli.
Ndio uchafu wenyewe huo mkuu huanzia kwa wazazi..Ukiniuliza mimi kama sisi Watanzania ni wachafu nitakubali hata kama sababu ni mzazi na ndio maana tupo hapa JF kutafuta mbinu za kujisafisha. Wasomi kama nyie ndio mnaotupa darasa kwani sii aibu kumwambia mzazi wako kuacha Ufuska..Ni haramu kula chakula kilichotokana na fedha za ufuska au wizi hata kama wewe ni clean!
Tuwe responsible na accountable..

Mkuu Mkandara, ukisema waTanzania wamechaliwa, nitakuelewa. Katika nchi hii, hakuna mchango mkubwa wa kimaendeleo, kijamii, kiulinzi na kadhalika unaotokana na wananchi. Dola limeshika nyanja zote hizo. Na nadhani hapo ndipo tunapoanza kupata matatizo makubwa. Maana Serikali ni watu wachache sana kulinganisha na umma mzima. Maendeleo yetu hayawezi kupatikana bila kila mtu kushirikishwa kwa namna zote inavyowezekana. Huwezi kuamini Mkuu, kwamba Taifa hili halijui lina idadi gani ya Engineers, Doctors, Scientists n.k. na mbaya zaidi haijui wako wapi na wanafanya nini. Hiyo ni licha ya kutokujua kuwa wana uwezo gani na unahitajika wapi katika kuendeleza nchi hii. Ndio maana unaona wanaona hakuna haja sana kulipia watoto wa vyuo vikuu ada zao zote (tena kwa mkopo). Mkuu, katika nchi hii, inaelekea kila mtu na lwake. Kila mtu atajenga nyumba kwa fedha zake kutoka mfukoni kwake, atalipa ada kwa fedha zake mwenyewe, atanunua samani kwa fedha zake mwenyewe n.k. Hivyo kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. HAPO NDIPO TULIPOISHIA, NA NDIPO TUNAPOKOSEA.
 
Tafadhali bainisha na uchafu wa vyama vingine vya siasa nchini! Unataka kuniambia kwamba chama kingine kikiingia madarakani hakiwezi kuiba?
 
Mkuu, katika nchi hii, inaelekea kila mtu na lwake. Kila mtu atajenga nyumba kwa fedha zake kutoka mfukoni kwake, atalipa ada kwa fedha zake mwenyewe, atanunua samani kwa fedha zake mwenyewe n.k. Hivyo kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. HAPO NDIPO TULIPOISHIA, NA NDIPO TUNAPOKOSEA.
.....Na ndipo uchafu unapoanzia
 
Kama CCM ni chafu ni sawa na kusema kuwa Watanzania wote ni wachafu ............................................................
Sio siri ule wakati wa Watanzania kutembea vifua mbele kutokana na uadilifu wa hali ya juu mpaka kuwa kioo kwa nchi jirani kama sio ulimwenguni haupo tena. Leo hii watanzania ni wapenda starehe na wavivu na mbaya zaidi ni mafisadi. Huu uchafu ni wa watanzania wote na ni vema kwanza watanzania wote wakajisafisha badala ya kukimbilia kusema kuwa CCM ni chafu.

Ndio maana nasema kuwa Watz ndio wachafu na sio CCM

CCM kuwa chafu si sawa na kusema waTanzania wote ni wachafu, hata kidogo. WaTanzania si CCM ila CCM ni waTanzania. CCM ina wanachama wasiozidi milioni 5 nchi nzima, walio hai na wasio hai. Hii ni asilimia ndogo sana ya waTanzania wote.

Uchafu wa kundi moja la watu, hauwezi kuwa uchafu wa nchi nzima. Ni sawa na kusema, uchafu katika mji mmoja wa nchi hii ni uchafu wa Taifa zima. Sio kweli hata kidogo. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha chama kuwa kichafu. Moja ya sababu hizo (ambazo ni kubwa) ni jinsi ya kupata viongozi wake (uchaguzi). Kama chama kitashindwa kudhibiti na kuweka ustaarabu wa upatikanaji wa viongozi kwa haki na usawa, ni dhahiri kuwa hakiwezi kuwa na watu safi kukiongoza. Maana, ili uwe kiongozi, itabidi uwe fisadi wa namna moja ama nyingine (uchafu mkubwa zaidi). Pili, uchafu wa chama unaweza kutokana na jinsi wanavyothamini na kuzingatia sheria za nchi, kujali mawazo mbadala na pia kujali ustawi wa jamii nzima (hii ya ustawi haijali kama chama kinaongoza dola ama lah).

Mkuu Mkandara, ukisema waTanzania wamechafuliwa, nitakuelewa. Katika nchi hii, hakuna mchango mkubwa wa kimaendeleo, kijamii, kiulinzi na kadhalika unaotokana na wananchi. Dola limeshika nyanja zote hizo. Na nadhani hapo ndipo tunapoanza kupata matatizo makubwa. Maana Serikali ni watu wachache sana kulinganisha na umma mzima. Maendeleo yetu hayawezi kupatikana bila kila mtu kushirikishwa kwa namna zote inavyowezekana. Huwezi kuamini Mkuu, kwamba Taifa hili halijui lina idadi gani ya Engineers, Doctors, Scientists n.k. na mbaya zaidi haijui wako wapi na wanafanya nini. Hiyo ni licha ya kutokujua kuwa wana uwezo gani na unahitajika wapi katika kuendeleza nchi hii. Ndio maana unaona wanaona hakuna haja sana kulipia watoto wa vyuo vikuu ada zao zote (tena kwa mkopo). Mkuu, katika nchi hii, inaelekea kila mtu na lwake. Kila mtu atajenga nyumba kwa fedha zake kutoka mfukoni kwake, atalipa ada kwa fedha zake mwenyewe, atanunua samani kwa fedha zake mwenyewe n.k. Hivyo kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake. HAPO NDIPO TULIPOISHIA, NA NDIPO TUNAPOKOSEA.

.....Na ndipo uchafu unapoanzia

Asanteni ndugu zangu - yote mliyoongea ni kweli tupu. Sasa je, ni nani katufikisha watanzania hapo, ni nani katuchafua, ni dola iliyoundwa na nani ambayo imeshika nyanja zote, na nani katufikisha HAPO NDIPO TULIPOISHIA, NA NDIPO TUNAPOKOSEA Na ndipo uchafu unapoanzia.
Nawashukuru kwa kukitambua chanzo cha matatizo yetu - CCM.
 
Back
Top Bottom