CCM si safi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM si safi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 22, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280
  Kama CCM safi, inaogopa nini?

  Lula wa Ndali-Mwananzela Januari 21, 2009
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo​

  HIVI ukimuona mtu kwa mbali amevaa suti nzuri yenye rangi ya kupendeza, amevaa viatu vya ‘bei mbaya’ huku ameshikilia mkongojo kwa fahari na akinukia manukato mazuri utaamini kuwa ni msafi?

  Ukimsogelea kwa karibu na kugundua kuwa amechana nywele zake vizuri, kucha zimekatwa vizuri, amejipaka mafuta inavyopaswa na meno yake yamepigwa mswaki kama wale watu wa kwenye matangazo ya Colgate si utakubali kuwa mtu huyo ni msafi?

  Wakati unamuangalia mtu huyo unaangalia aliposimamia na unagundua kuwa amesimama kwenye shimo la takataka lenye kunuka kila aina ya uvundo na akisema kuwa yeye ni msafi utamkubalia?

  Ukichukulia kwa maana ya “mtu msafi” hivi usafi ni usafi wa mtu tu na si mazingira aliyopo pia?

  Kwa muda mrefu sasa nimekaa pembeni nikiangalia kichekesho cha malumbano kati ya CCM na wapinzani wake ambapo wapinzani (wakiongozwa na kina Dk. Wilbroad Slaa na Zitto Kabwe) wakidai kuwa CCM si safi huku wao CCM wakiongozwa na watetezi wake kama Mzee wetu John Malecela na Amos Makalla wanadai kuwa CCM ni safi!

  Baada ya kuangalia kituko hicho kwa muda mrefu na mimi naombe niongeze munyu kwenye mjadala huu kwa kutangaza kuwa CCM ni chama kinachodai kuwa ni kisafi huku kikiwa kimesimama juu ya lundo la uchafu, kikauzoea, kikapoteza hata uwezo wake wa kunusa harufu mbaya inayozunguka.

  Ukiona mtu anakukawiza kawiza kuingia sebuleni basi ujue kuna kitu; na kama umeenda kumtembelea rafiki yako wa mwenye kibanda cha chumba kimoja naye akawa anakuambia “subiri kidogo” basi usiharakishe kwenda ndani! Kuna wakati ambapo mgeni akikaribishwa anaonyeshwa maeneo fulani fulani tu lakini yale mengine “nyeti” anafichwa kwani hadi ‘mazingira yaboreshwe”.

  Inapokuja kwenye vyama vya kisiasa, ukiona chama cha kisiasa hakiko tayari kufungua mahesabu yake mbele ya umma basi usiwe na shaka ndani kuna matatizo. Hakuna chama kilichopokea fedha nyingi za umma za walipa kodi wa Tanzania kama Chama cha Mapinduzi, lakini pia ndicho chama ambacho hakijathubutu kuweka wazi mapato yake yote na matumizi yake kwani si vyote viko sawasawa.

  Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ya mwaka jana inaonyesha kuwa vyama vya kisiasa vyote havikuwasilisha taarifa zao za mwaka za fedha na kutolea mahesabu kiasi cha shilingi bilioni 13. Kwa vile CCM ndicho chama tawala na ndicho ambacho kinadai kusimamia utawala bora na sheria inashangaza sana ni kwanini hakikutoa ripoti hiyo wakati wa ukaguzi.

  Lakini zaidi kinachoshtua ni kutokukaguliwa kwa vitabu vyake na taasisi huru na matokeo yake kuacha chama hicho kikongwe zaidi cha kisiasa nchini kugubikwa na wingu la tuhuma za kuhusika na ufisadi.

  Mwaka 1995 CCM inadaiwa ilipata msaada wa kiasi kikubwa cha fedha kutoka Zimbabwe ili kuweza kufanikisha kampeni yake ya uchaguzi mkuu. Mwaka 2000 kuna habari kuwa CCM ilitumia Benki Kuu kujichotea mabilioni ya shilingi ili kufanikisha kampeni zake. Kuelekea uchaguzi wa 2005 tuhuma za fedha nyingine ziliibuka.

  Mwezi wa Aprili 2005, gazeti mashuhuri la Uingereza la Africa Confidential liliandika habari kuwa fedha karibu shilingi bilioni mbili zilikuwa zimeingia katika mchakato wa uchaguzi kutoka Oman. Baadaye zilikuja habari nyingine kwamba kulikuwa na fedha zimetoka Iran.

  Kinachoshangaza kuhusu habari hizo ni kwamba kampuni moja, Kagoda ilikwisha kupata “mikataba” na makampuni ya kigeni ya Nishizawa ya Ujapani (JPY 956,110.986- Tarehe 10 Septemba, 2005) na kampuni ya Textima (dola 9,057,463.90 – 12 Septemba, 2005), tatizo ni kuwa kampuni ya Kagoda haikuwa imesajiliwa hadi tarehe 29 Septemba, 2005.


  Je, yawezekana hakukuwa na taarifa sahihi za fedha hizo kwa kudhaniwa kuwa ni za “Iran” kumbe zikiwa ni za Kagoda?

  Sasa naweza kusema mengi ambayo tayari yamesemwa na wengine. Leo hii CCM inatumia karibu shilingi bilioni moja (na sehemu nyingine bilioni mbili) katika chaguzi ndogo za kuziba viti vya ubunge. Tukichukulia kwa haraka tu kuwa gharama ya jimbo moja kwa CCM ni shilingi bilioni moja tunajiuliza mwaka 2005 CCM ilikuwa na wagombea katika majimbo yote ya uchaguzi nchini. Je ni kiasi gani cha fedha kilitumika?

  Pamoja na gharama ya uchaguzi mkuu tunakumbuka kuwa katika kila jimbo CCM ilikuwa na kura zake za maoni ambazo iligharimia, je, ni kwa kiasi gani? Kwa hesabu za haraka haraka CCM ilihitaji si chini ya shilingi bilioni 100 (ukizingatia gharama ya jimbo moja ni bilioni moja lakini ukiwa na majimbo mengi kwa wakati mmoja gharama inapungua) kufanya kampeni za madiwani, wabunge na Rais. Fedha hizo zote zilitoka wapi?


  Lakini cha kushtua zaidi ni kuwa hadi hivi sasa kuna kila dalili kuwa kampuni ya Kagoda haitawekwa wazi isipokuwa watu wawili watatu wanaweza kufikishwa mahakamani kwa “udanganyifu, kughushi nyaraka n.k”. Nawahakikishia kama CCM inataka Kagoda ifahamike ingeshafahamika mwaka juzi!

  Wapo wale ambao wanataka tuamini kuwa kufikishana mahakamani kunakoendelea sasa hivi kunaonyesha jinsi gani Serikali iko makini katika kusimamia sheria. Mawazo hayo yameanza kurudiwa na viongozi mbalimbali wa CCM ambao wanataka wananchi waamini kuwa Serikali iko makini kupambana na ufisadi!

  Kwa haraka haraka mtu anaweza kuamini hivyo. Hata hivyo, tunajiuliza hivi haya yote yanayowafikisha watu mahakamani yametokea chini ya utawala wa chama gani? Tunawauliza hivi baadhi (kama siyo wote) wa watuhumiwa ni wanachama wa chama gani cha kisiasa? Je, wale waliokuwa mawaziri ambao wamefikishwa mahakamani kwa makosa wanayodaiwa kuyafanya hivi waliyafanya wakiwa ni mawaziri wa Serikali iliyoundwa na chama gani?

  Mkataba wa IPTL uliingiwa na Serikali ya chama gani? – CCM.
  Mkataba wa Richmond uliingiwa na viongozi wa Serikali ya chama gani?- CCM. Mkataba wa Buzwagi uliingiwa na Waziri wa Serikali ya chama gani? – CCM.
  Mkataba wa ununuzi wa rada iliingiwa na Serikali ya chama gani? – CCM.

  Mkataba wa ununuzi wa dege la Rais uliingiwa na Serikali ya chama gani? – CCM. Kuleta ubia wa uendeshaji wa ATCL na SAA ulifanywa na serikali gani? – CCM.

  Kuleta waendeshaji wa Tanesco kulifanywa na Serikali ya chama gani? – CCM.

  NI serikali gani iliingia mkataba na kampuni ya RITES Consortium kuendesha shirika letu la Reli hadi leo wamewakumbushwa kuwa mataaluma ya reli kumbe yetu? – CCM.

  Wizi wa mabilioni ya EPA umefanyika wakati Serikali gani ikiwa imelala kwenye usukani? – CCM.

  Ufujaji mkubwa wa matumizi ya fedha za walipa kodi ulioonyeshwa katika ripoti ya CAG ulifanyika ndani ya Serikali ya chama gani? – CCM.

  Rais anayedaiwa kufanya biashara akiwa Ikulu na kujitajirisha kinyume na maadili ya uongozi alitoka chama gani? CCM!

  Hiyo ni mifano michache ya kitaifa tu, wakitaka turudi kwenye halmashauri na miji mbalimbali nchini, na ufisadi kwenye idara na vitengo mbalimbali tunaweza!

  Leo wanapokamatana wenyewe kwa wenyewe ndiyo wanataka tuanze kuwashangilia kuwa wao ni safi? Hivi kama hayo hapo juu ni “usafi” basi uchafu umepoteza maana yake!

  Hivi, wanaposimama majukwaani na kudai kwa kiburi cha chama kuwa “CCM ni safi” wanatufikiriaje sisi, majuha?

  Mpaka pale chama nikipendacho, chama nilichokulia, chama cha Baba wa Taifa kitakapokubali kuwa “kinanuka” kitakapokubali kuwa ni “kichafu” kitakapokubali kuwa si tu “mtu mmoja mmoja ni mchafu” bali mfumo mzima wa chama na utamaduni wa chama ni mchafu ndipo hapo tu kitakapoanza kweli kujisafisha na kusafishika.

  Na ndugu zangu CCM washukuru Mungu kuwa huko kwenye Upinzani usafi wenyewe nao wa kutafuta! Vinginevyo kikija chama kilicho kisafi kweli, CCM uchafu wake utakuwa ni dhahiri kuliko gari la taka!

  Nilichotaka kusema kwa kifupi ni kuwa CCM isiringie uzuri wa suti zake, na utamu wa sauti za wapambe wake; isiringie uzuri wa makada wake au ukuu wa vyombo vyake vya kijeshi. CCM isichanganye wananchi kukubali wachafu kidogo waongoze kuwa ni kuwa wananchi wanaamini kuwa CCM ni safi kweli. Siku moja watakaposhikiwa sabuni na kutupwa mtoni kuogeshwa ndipo watakapogundua uchafu wao ulivyo.

  Kuna njia moja ya uhakika na isiyo na shaka itakayoisafisha CCM mbele ya umma. Njia hiyo haiwahusishi kina Yusuf Makamba wala Malecela kujipigia debe. Njia hiyo ni ya kisayansi na ambayo inaweza kuzima mjadala wote wa CCM chafu. Njia hiyo ni kwa CCM kualika kampuni ya kimataifa ya mahesabu, ifanye ukaguzi wa maheshabu yake kuanzia angalau 2005, na kutoa taarifa hiyo hadharani.

  Endapo taarifa hiyo itasema kuwa mahesabu yote ya CCM ni mazuri na hayana shaka na ya kuwa vyanzo vyote vya fedha vinaeleweka, na ya kuwa fedha zote zinajulikana zilikotoka na zilivyotumika, na vyanzo hivyo vyote vikawekwa hadharani kwa mwananchi yeyote kuvitambua, basi ni hapo tu nitakaposimama na mimi kwa fahari kusema “CCM ni safi”. Sasa hivi tunazugana kwa maneno ya mapambo, na kwa kauli za ulimbo!

  Wito wangu ni kuwa CCM ianze kujisafisha sasa na kutoka kwenye shimo la taka ambako imesimama huku ikitangazwa kwa kipaza sauti “mimi msafi”. Usafi si mavazi tu, na si kuonekana tu, usafi ni pamoja na mazingira uliyopo. Kwa sasa mazingira ya CCM ni machafu, na hivyo yanaifanya CCM kutokuwa safi. Mwenye kubisha abishe, habari ndiyo hiyo!
  Barua-pepe: lulawanzela@yahoo.co.uk
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hayo ni mawazo yako tu.... Unaweza hata kuandika kitabu cha kurasa 10,000 kwamba CCM sio safi...CCM ni safi na itaendelea kuwa safi. Wale wachafu ndani ya CCM tunawatoa pamoja na mazagazaga yao.
   
 3. L

  Labibah Member

  #3
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe mwehu nini? kama ni chafu kwanini mnatoa hayo mazagazaga yao na hao.
  CCM itabaki kuwa chafu mpaka kikwete na RA watoke na vibaraka wake wengine hapo ndipo itakuwa safi.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Shika adabu yako... nani amekupa ruhusa ya kuedit bandiko langu. Tena naona unakuja kasi sana kijana.. angalia utaukalia
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280

  Mmeshawatoa wangapi hadi hii leo!? Mzee wa Vijisenti, Rostam Azizi, Lowassa, Mramba, Mgonja, Msabaha, Mkapa, Yona na wengineo chungu nzima bado wanapeta bila wasiwasi wowote ndani ya CCM. Kinachotia moyo ni kwamba Watanzania wameanza kuelewa kwamba matatizo yetu makubwa yanasababishwa na Chama Cha Mafisadi.
   
 6. A

  AndrewMwanga Member

  #6
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Suala la uchafu si CCM ni hulka ya mtu binafsi na ifahamike kuwa cc inaundwa na watu na tabia ya mtu binafsi si ya CCM.

  nAHESHIMU SANA MAWAZO YAKO MKUU ILA NAPENDA KUWATOFAUTI NA WEWE KIHOJA NA KIFIKRA KAMA IFUATAVYO,

  CCM ni safi naitaendelea kuwa safi daima kwa kuwa inania ya dhati ya kuwatumika wananchi wa Tanzania, na wanachi wengi wanatambua hilo ndiyo kilipata ushindi wa kishindo 2005

  Hayati baba wa Taifa alisema ,Chama cha siasa ni kama kokoro linavua samakia kama sangara, chura,dagaa na vinginevyo hivyo si vyema kusema CCM si safi kwani utakuwa umeangalia katika individual aspects.

  Kama CCM IMESIMAMA KWENYE LUNDO LA TAKATAKA KINACHOTAKIWA NI KUTOKA NA KUSIMAMA MAHALI PASIPO NA LUNDO LA TAKATAKA NA MKONGOJO WAKE HUKU IKINUKIA MANUKATO.

  NA KWATAA**** IMESHAANZA KUONDOKA ENEO LENYE LUNDO LA TAKA LINALONUKA.

  AM
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  mtu mchafu mwenye nia ya kununua sabuni ya kuogea na kufulia, amekuwa msafi kwa sababu ya nia yake hiyo?
   
 8. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  CCM iliwahi kuwa safi wakati wa Mwalimu Nyerere, ila tangu walipoondoa Axzimio la Arusha na kuja na lile la Zanzibar ndio chimbuko la uchafu wao.

  CCM ni wachafu sana na kama kungekuwa na neno baya zaidi la kuuelezea uchafu wa CCM basi lingeweza kutumika sasa kwani huu ni uchafu wa kupindukia.

  Mara leo wanasema KAGODA nyaraka zimepotea mara wanasema IKULU haijui lolote kuhusiana na nyaraka wakati aliyepaswa kuzihifadhi alisema kuwa zilichukuliwa na Timu ya rais .

  Kama wanataka kujua waende CRDB BANK na kuwauliza ni nani aliyesaini hundi zilizochukua shilingi bilioni 40 kwa siku moja kwenye matawi sita ya CRDB JIJINI DSM.
  KUANZIA LILE LA KIJITONYAMA, HOLLAND,AZIKIWE.........

  Uchafu wa CCM ni mkubwa kiasi kwamba wameshauzoea na ndio maana wanadhubutu kujitetea eti kuwa wao ni wasafi kwani wanaona hawawezi kuwa tofauti na walivyo hivi sasa.
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Na hatutegemei mtu msafi kutumia nguvu nyiingi majukwaani kushawishi wengine kwamba yu safi........
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jan 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa kawaida usafi hauitaji kutetewa.. unaonekana!
   
 11. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,188
  Trophy Points: 280
  Naam huhitaji kupiga debe kila kona ya nchi kutetea usafi wako maana usafi wako utaonekana tu machoni mwa Watanzania bila matatizo yoyote, lakini hivyo sivyo ilivyo hivi sasa. Tunaona uchafu chungu nzima ulivyolundikana ndani ya CCM na hatuoni juhudi zozote za kweli za kusafisha uchafu huo maana wahusika wote bado CCM imewakumbatia tena wanaitwa waheshimiwa ndani ya chama hicho.!!!
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Na wewe hayo ni mawazo yako kama mtu ambaye ameamua kuukumbatia huo uchafu na kwa jeuri inayopatikana tu ndani ya CCM anaamua kuufumbia macho huo uchafu.

  Na wewe unaweza kupayuka unavyotaka kwa kuupaka rangi uchafu na kuuita usafi kwa sababu toka lini nzi akautolea uvivu dampo - ni eneo lake la kujidai na uvundo kwake ni harufu ya halua.

  Na CCM ni chafu na itaendelea kuwa kimbilio na kivutio kwa wachafu kwa sababu uchafu kwao umekuwa way of life. Waliomo tayari wameonja damu ya wakulima, waalimu, wastaafu, wagonjwa na wale wote wanaoteseka na kusumbuliwa na uvundo wa CCM.

  Mnawatoa wewe na nani ? Mpaka sasa wanaotamba ni hao hao na wapiga debe wao wakiongozwa na watu aina yako. Waliojaribu kujisafisha wamevutwa na kufungwa pingu humo humo katika uchafu na sauti zao zimenyamazishwa. Hebu nitajie hao waliotoswa pamoja na mazagazaga yao.

  Hivi ndugu yangu Kibunango unisaidie - chama ni kitu gani ? Je tunaweza kuwa na chama bila watu ? Mbona msajili wa vyama vya siasa anahitaji chama kabla ya kusajiliwa kitimize lengo la kuwa na idadi fulani ya watu ? Kwa nini inakuwa lazima hao watu wawe wamekaa na kuchagua watakaowaongoza kwa kipindi maalumu ? Chama kiwe kisafi, wanachama wawe wachafu - kweli watatekeleza nia na malengo ya chama - Birds of a feather fly together.
   
 13. L

  Labibah Member

  #13
  Jan 22, 2009
  Joined: Jan 20, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe mpuuzi sana ,uukalie wanani unadhani watu wote humu ni mabasha eeeeh? **** wewe umezoe kupimwa oil
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wale wote wachafu wamekuwa wakitimiliwa ndani ya chama tangia kuanzishwa kwake. CCM sio chama cha mtu mmoja ama genge la watu fulani najua unalijua hilo, na imekuwa ikiwaondoa wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakienda kinyume na katiba ya chama, kupitia vikao vyake vya kawaida na dharura katika ngazi zinazohusika. Na wengine kwa kushindwa kufuata katiba ya chama hicho wamekuwa wakijiengua wenyewe kabla ya kutimuliwa.

  Kauli ya usafi ama uchafu ni kauli ambayo tupo nayo katika miaka hii, CCM kama chama inaenda sambamba na kauli hiyo kwa kuendelea kuwaondoa wale wote wanabainika kuwa ni wachafu. Taratibu za kuwaondoa wachafu hao ni zilezile ambazo zimekuwa zikitumika tokea kuanzishwa kwa chama hicho.

  Uzuri wa miaka hii ni kuwa wale wachafu ambao hutimuliwa CCM hupata sehemu za kwenda na mazagazaga yao ya uchafu. Na huko hukutana na wachafu wenzao na kuendeleza tabia zao za uchafu uchafu, huku wakiota siku moja wataongoza nchi na mauchafu yao.
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Jan 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  nyumba inayokaliwa na wachafu ni nyumba safi? au ni safi pale wachafu wanapoondoka lakini wakiwa ndani hawaichafui hiyo nyumba? Kama wale wachafu wanapotoka na kwenda kuungana na "wachafu wenzao" yawezekana kwamba huko walikokuwa wamewaacha wachafu wenzao wengine?
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Nyumba safi inaweza kukaliwa na wachafu vilevile, hata hivyo kutokana na sifa ya uchafu kuwa unuka ni rahisi kwa wachafu kujulikana katika nyumba safi. Na pua za wasafi wengi wa CCM siku zote zimekuwa zikinusa wale wote ambao awali walikuwa wasafi, lakini wakaanza kuwa wachafu. Uzuri utimuliwa mapema kabla ya kueneza tabia zao mbaya za uchafu.

  Tatizo ni pale wachafu wanapokwenda kukaa na wachafu wengine, kwani sio rahisi kwa mchafu kunusa harufu chafu ya mchafu mwenzie.
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Jan 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  unataka tuamini kuwa wachafu wote wameshatoka CCM? Kama wapo ina maana pua za CCM hazinusi vizuri hivyo, kama wote wameshatoka tunatarajia hakuna kiongozi au mtu mwingine yeyote atakayetoka CCM au kushtakiwa kwa sababu ya "uchafu".

  Je hivi sasa kuna watu CCM ambao ni wachafu na wanachafua hiyo nyumba na harufu yao haijanusika vilivyo?
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wachafu bado wapo ingawa wanajitahidi kujificha kwa kujipaka manukato ya aina kwa aina, ila watazidi kunuka kwa harufu ya mchanganyiko huo, kwani uchafu kamwe haujifichi na ni hapo ndipo utimuliwa kwa aibu tele.

  Kimsingi Wachafu bado kwisha ndani ya CCM, lakini hii haina maana kama CCM ni chafu. Baba wa nyumba ya CCM ameshasema bayana kuwa mchafu yoyote atakayebainika ndani ya nyumba ataondolewa na kupelekwa kunako husika na usafishaji wa wachafu. Kauli za Baba huyu zimeshaanza kuonekana licha ya maneno ya kejeli toka katika katika nyumba za Wachafu wengi ambao kutwa wamekuwa wakitamani Nyumba safi ya CCM iwe chafu kama zao.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jan 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo CCM ina wachafu; wachafu ambao bado wamo wamejificha na kujipambisha kwa manukato... kwamba harufu ya uchafu wao inadhaniwa ni manukato kiasi kwamba ni vigumu kugundulika..

  Mojawapo ya vitu nilivyojifunza kwenye falsafa ni kutokuwa na internal contradition. Kitu hakiwezi kuwa au kutokuwa kuhusiana na kitu kile kile kama kizima na si sehemu yake. CCM ni chafu au safi; kama ndani yake kuna watu wachafu (kama ulivyokiri) then CCM haiwezi kuwa safii yote kwani CCM siyo box au chupa fulani bali ni watu.

  Nikukumbushe Muongozo wa Maadili ya Chama (2002) unasema hivi:

  Hivyo CCM inasema kuwa kuna uhusiano kati ya maadili ya mtu (kiongozi) na uhai wa chama. Ukiwa na kiongozi mwenye maadili yaliyotetereka basi "chama kitavurugika".


  Chama hiki ambacho tunaambia kuwa ni "kisafi" kinasema hivi kuhusu kushughulikia uchafu wake:

  Ndg. Kibunango, chama chetu kimemuondoa nani katika chama au katika uongozi kwa sababu ya uchafu? Hata leo yule kigogo wa CCM toka Kigoma ambaye amesimama kizimbani hajaondolewa uongozi wake au kufukuzwa uanachama! Lowassa bado ni mwanachama, Rostam bado ni mwanachama,.. n.k!!

  Muongozo huo huo unasema hivi:

  Ndg. Kibunango.. kweli CCM na viongozi wake wanazingatia maadili hayo. Ungependa nitoe mifano michache ya jinsi gani baadhi ya viongozi wana mahusiano ya karibu na watu au makampuni ?

  tatizo baba mwenyewe naye ni mchafu (angalia ripoti ya mkaguzi mkuu kuhusu Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wakati yeye akiwa ni waziri wake). Leo baba anasimama na kukemea uchafu? Uchafu ambao yeye mwenyewe amekaa kwa karibu miaka 20 akiushuhudia ukiingia na kukua kwa haraka kama uyoga?
   
 20. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  By the way,
  Chawa, Kunguni na viroboto wote huvutiwa na uchafu. Wote hawa kazi yao ni kunyonya, na wazeza kumnyonya kiumbe hadi akapoteza maisha nao wakafia humo. Daima hawa hawwambatani na kiumbe aliye safi.

  Watafute hao chawa, kunguni na viroboto wako wapi. Ukipata waliko basi, utakuwa umepata jibu kama usafi umo ndani yake au la!
   
Loading...