CCM sawa na mbwamwitu

CCM sawa na mbwamwitu

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
23,251
Reaction score
28,406
Hawa wanachama wa CCM wameishiwa hoja badala yake wanatumia mashambulizi kwa mtindo wa mbwamwitu, wanadhani wakishambulia kwa wingi wa kundi lao basi watakuwa wamejenga hoja!

CCM imeishiwa watu wenye uwezo wa kufikiri kabla ya kujibu. Mtu mmoja anatoa hoja zake linaibuka kundi la watu zaidi ya hamsini linaanza kubwabwaja kila mmoja na lake japo hakuna mwenye hoja bali viroja.
 
wanashambuliana kwa zamu na huu umekuwa kama utaratibu wao wa kawaida. Kina Bushiri na mzee polepole walifanya hivyo hivyo kuwasurubu wazee wastaafu wa chama, kina nape nk Sasa leo imemgeukia mzee Bushiru anayeshambuliwa kila kona. Mzee wa Nazaleti na yeye pia yalimkuta makubwa ila kaona anyamaze kujinusuru nafsi.

Kifupi tu watanzania ni kwamba chama kama hiki je unategemea kuna maendeleo kweli?
 
wanashambuliana kwa zamu na huu umekuwa kama utaratibu wao. Kina Bushiri na mzee polepole walifanya hivyo hivyo kuwasurubu wazee wastaafu wa chama, kina nape nk Sasa leo imemgeukia mzee Bushiru na yeye anashambuliwa kila kona.

Kifupi tu watanzania ni kwamba chama kama hiki je unategemea kuna maendeleo kweli?
CCM haijajikita kuijenga Tanzania bali imejikita kujijenga japo imeishiwa mbinu, CCM inadhani kuteuana kwenye safu ya uongozi ndiyo kukijenga chama! Inasahau humo kwenye safu yamo pia manyangarakasha yanayotumia kuvaa sare inayompendeza ndiyo kuiva kiuongozi.
 
Back
Top Bottom