CCM sasa wamtumia Warioba kuimaliza CHADEMA? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM sasa wamtumia Warioba kuimaliza CHADEMA?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Oct 12, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimesoma habari ya Jaji Warioba katika gazeti la Raia Mwema la leo, nikagundua kuwa CCM bado inafikiri kuwa Watanzania kuwa ni wajinga kiasi hicho, wanachofikiri wao ni kuwa bado kuna watu wanaweza kufikiri vizuri kwa ajili ya watu wengine.

  Kingine nilichogundua ni kuwa CCM wanaweweseka, na CCM ndio itakayoleta vurugu nchi hii kwa kuwa haiko tayari kushindwa kidemokrasia yamejidhihirisha katika mazungumzo hayo ya Jaji Warioba.

  Lingine nililojifunza ni kuwa CCM sasa wanatumia mbinu zozote zile zidi ya CHADEMA kuwa kuwa haiwezi tena kushindana na CHADEMA kisera imebakia kuropoka, sasa wamebuni mbinu za kuwatumia watu maarufu kama Warioba kujifanya wanazunguzia mustakabali wa nchi bila upendeleo huku wakiingiza maoni ya kuiponda CHADEMA.

  Warioba anasema Chadema kule igunga wasifikiri wanapanda chati ile inaweza kuwa nguvu ya soda halafu anaingiza propaganda za CCM za udini na kuwa CHADEMA si chama cha watu.

  Tumuulize Warioba atupe data zinazoonyesha kuwa kule si kupanda chati bali ni nguvu za soda si kuzungumza kisiasa na kinadharia. Wengine sisi si wanasiasa tunataka analysis and fact.

  Angalizo kwa CHADEMA ni kuwa kuna nguvu iliyo nyuma ya pazia ya kuiangamiza ambayo ni kubwa sana, sasa hivi wanawatumia wakongwe hao wameanza na Warioba, atafuata Salim, gazeti la Raia Mwema limeshachukuliwa! Kumbuka Warioba na Jenerali na Mkapa walikuwa marafiki wakubwa sana kabla ya wawili wao hawajagombana.

  Mimi nimefanya kazi kwa Jenerali Ulimwengu wakati wanaanzisha gazeti la Mtanzania nawafahamu vizuri.

  Watanzania tusikubali kuruhusu watu kufikiri kwa niaba yetu, CCM hawako tayari kuona chama kingine kwa kuwa wanaogopa utawala mwingine kwa kuwa wanajua katika CCM hakuna aliyemsafi kamili. Watajifanya kujikosoa wenyewe ili wabaki madarakani ili kulinda madhambi yao. Tuendelee kupambana mapaka ukombozi kamili upatikane.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu mabadiliko yanatokea sasa hivi nchini na nchi zingine ni ya lazima kutokea kutokana na mwamko wa watu kila kona.

  Teknolojia ya habari imesaidia sana watu kuelewa nini pumba na nini mchele, kinachotakiwa ni hao ndugu zetu wa kijijini kupata ujumbe na kuwatoa uoga.

  Serikali saizi inaishi wa kuvitisho, watu wengi huko vijijini mfano Ukenyenge kijijini kwangu wanamwamko, hawadanganyiki.

  CCM waendelee kutumia vitisho ila the changes are non-stoppable. Mabadiliko yatatokea nchi zote jirani, Tanzania watayazuia na nini? Kwa mikwara, No no no way! Kwa risasi? No no no no! kwa kuchakachua kura?

  Tusubiri watu watakaoandikishwa; safari hii ni mguu kwa mguu hakuna mtu kuibiwa.
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kila anayejaribu kushauri, kuonya, kukemea baadhi ya mapungufu ya CHADEMA mtasema anatumiwa na CCM. Hivi kama mtu au chama unakipenda utakaa kimya tu na kukisifia hata kama unaona kinakoelekea siko? Sasa hivi Jaji Warioba anajaribu kuwa juu kidogo ya siasa za vyama. Jana alivikosoa vyama vyote ikiwemo CCM yake. Wewe umeyaona maoni haya ya CHADEMA tu. Kwa namna ulivyoleta, utaungwa mkono sana tu humu JF. Umeongea lugha ya wengi humu.
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kushindana kwa sera. Sera zipi? Ninachojua ni kwamba Chadema wamaekuwa tu wakosoaji bila kueleza ni kipi walichoandaa ambacho watawaletea wananchi iwapo wataingia madarakani. Ni kulia lia na kulalamika wakati kwenye majimbo wanayoyaongoza hali ni hoi bin taabani na wala huoni kama kuna kitu kinachoweza kuipambanua Chadema na CCM na kuwapa watu matumaini kwamba chama hicho ni mbadala wa CCM.
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wamekosa watu wa kutumia. Kuna wengingine ni watoto wa mjomba hao. hawana jipya.
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Huyu fisadi mzee naye anatafuta pa kufia, anafikiri tumesahau ile ishu yake ya Mwananchi Gold? Akafie mbali huyo kikongwe.
   
 7. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Yeye Warioba amelifanyia nini taifa hili hadi atuchagulie chama. Ameshiriki katika ufisadi wa madini, ni fisadi tu kama mafisadi wengine. Hana mashiko katika jamii na alipewa madaraka na Mwalimu kwa vile wanatokea njia moja, sio objectively. Ni mmoja wa viongozi wanaodaiwa na nchi hii kwa umaskini huu tulionao na miaka 50 ya uhuru. Hakuna atakayejali kauli zake zaidi ya sisi vijana kujiuliza huyu mzee atakufa lini atuachie nchi yetu aliyoinyonya enzi za uhai wake?
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Poti anaota kuwa Waziri Mkuu tena kama Machina anavyoota kuwa Rais.
   
 9. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ukiwa ndani ya magamba na wewe ni gamba tu hata iweje haibadiriki!
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Oct 12, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kabisa mkuu. KInachotuumiza watanzania hivi sasa ni kuzama zaidi kwenye siasa za vyama. Mbaya zaidi, hata humo kwenye siasa za vyama tunaangalia mambo kwa ushabiki kuliko dhamira ya kusaidia kulikwamua taifa. Ni wakati sasa tukaibuka juu ya siasa za vyama na kuiangalia Tanzania kama Taifa, hasa wakati huu tunapoadhimisha miaka 50 baada ya Uhuru
   
 11. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Kama wananchi wanalia na kulalamika unategemea wanasiasa wanaowapresent wafanyeje? wachekecheke.
  Wakati wa Kampeni DR SLAA alisema hana mpango wa kubadilisha sheria hata moja atakachokifanya
  ni kuzisimamia kwa uadilifu mkubwa sheria zilizopo. bado hapo hauoni utafauti wa kisera na serikali ya
  Jakaya ambayo haiko tayari kusimamia sheria zaidi ya kutuongoza kuzivunja?

  well, Hakuna mtu anategemea tutakuwa na chama perfect kama vile kimeteremshwa kutoka mbinguni.
  CHADEMA wanaweaknesses zao, tuzipima na za CCM ni sawa na kulinganisha harufu ya mavi na ua rose.
  why do you insist comparing these two, by the way, hata tukikomaa kuisafisha CHADEMA mpaka ikawa
  nyeupe kama saruji haitotuletea unafuu kwenye maisha yetu immedietly, haitazuia vifo vya mama wajawazito
  na vichanga vyao kwa kukosekana huduma bora za uzazi wa afya as soon as possible, haitashusha bei ya
  sukari, mkate wala unga, haitaleta solution ya kupunguza ajali za barabarani za kimfumo.

  Its just different, tunategemea katika kuikosoa CCM, ijirekebishe na hivyo kufungua milango ya kuboresha
  maisha yetu, surprisingly this does not happen. so what do we do? remove them.

  Hatutaki kuwa confused na agenda za kutuelekeza kufikiria wala kujishughulisha na issues ambazo
  hazina manufaa kwenye maisha yetu, tumekuwa conviced kwamba kuiondoa CCM madarakani
  ndio solution.
   
 12. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Walioba hana legacy yoyote,na yeye ni gamba tu.mbona ni mweyekiti wa council pale udsm na kuna madudu mengi yanafanyika tu chini yake.TUPA KULE
   
 13. M

  Mpanzi JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 767
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  kwa kufungamana na CCM gazeti la raia mwena ndo linakufa, Ulimwengu hajajifunza kikichomfanya akaikimbia habari corp.
   
 14. m

  mambomoto JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 327
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee aendelee tu kunywa pombe zake kali.
   
 15. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hivi naombeni msaada gongo ukiinywa sana inaongeza uwezo wa kufikiri au inapunguza?
   
 16. r

  rutakolwakolwa Member

  #16
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkubwa umenena tatizo hatutaki kuambiwa ukweli waungwana!!
   
 17. K

  Kasent Member

  #17
  Oct 12, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama Kweli Chadema mnaonesha ni jinsi gani heshima Huyo unaye mtukana na Sawa na baba yako na pia aliwahi kuwa kiongozi Wa nchi hii. Hivi nikweli hakuna alichokifanya alipokuwa madarakani? Au umezaliwa juzi hujuwi tulikotoka? Achani siasa za chuki
   
 18. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Nilkuwa namuheshimu sana Warioba lakini sasa naona anakoelekea atapoteza heshima yake,anazeeka vibaya na hiyo mipombe na umri wake inabidi anywe Casstle lite.
   
 19. m

  marembo JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wimbi laja na tufani hakuna wa kulizuia. Hao wanaotumiwa sasa ndio waliotufikisha hapa kwenye lindi la umaskini. WEacha waongee tu baragumu la mabadiliko limelia na watu wanajifunga kibwebwe kjusonga mbele. Wakijiingiza katika siasa basi walipuliwe hadharani na kukitokea mabadiliko mali zao zitaifishwe. Mungu yupo na waja wake katika mpambano huu. Tuwapuuze hao wanaozuia kusonga mbele,
   
 20. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kwanza atuambie fedha za Meremeta ziko wapi?
   
Loading...